Featured Post

MBUNGE WA GEITA MJINI, MHE.KANYASU AWAWASHIA MOTO VIONGOZI NA WAZAZI WASIODHIBITI MIMBA SHULENI

Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke kuhusiana na umuhimu wa viongozi pamoja na wazazi katika kushirikiana kwenye vita dhidi ya wanaume wanawapa mimba watoto wa kike wakiwa bado shule.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema atawashughulikia Watendaji Kata wote watakaobainika kushindwa kuchukua hatua kwa Wanaume wanaowapa mimba wanafunzi wa kike wakiwa bado shule.
Pia, Ametangaza vita kwa Waendesha pikipiki (Bodaboda ) kuwa yeyote atakayebainika kumpatia mimba  mtoto wa kike akiwa bado shule hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke Kata ya Bulela mkoani Geita.
Amesema mtoto wa kike anayepata mimba akiwa shule na hivyo kulazimika kukatisha masomo yake haiwezi kuwa Mama bora kwa sababu atashindwa tu kumlea watoto wake ipasavyo.
"Ninyi wanafunzi someni hata ukipata daraja la mwisho baada ya kufika  kidato cha nne ni lazima utakuwa Mama bora" alisisitiza Kanyasu
Amesema maisha ya sasa yamebadilika sana  tofauti na zamani ambapo kwa sasa bila kusoma maisha ni magumu sana
Mhe.Kanyasu amesema haiwezekani Serikali itoe pesa nyingi  kila mwezi katika shule zote nchini ili watoto wa kike waweze kusoma huku idadi ya watoto wakike  wanaoacha shule kwa sababu za kupata mimba ikizidi kuongezeka.
" Nawambieni Watendaji wa Kata mkishindwa kuwachukulia hatua waharibifu wa ndoto za watoto wa kike nitaanza na ninyi" alisema Mhe.Kanyasu.
Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaonya wazazi wanaowalinda Wanaume  wanaowapa mimba watoto wa kike kwa kukubaliana nao kuwa ni jambo lisilokubalika.
" Mimi Mbunge wenu nimekuwa nikihakikisha napigania ujenzi wa shule bora pamoja na walimu bora lakini baadhi ya wazazi mmekuwa  mkiwalinda wanaofanya uharibifu, si jambo zuri"
Amewataka wazazi waache tabia ya kuelewana katika ngazi ya kifamilia kwa wanaume wanaokatiza ndoto za watoto wa kike wakiwa bado shule.
" Nawasihi wazazi mzungumze na Watoto wa kike kuhusu umuhimu wa kusubili huku mkiwasisitiza kuhusu umuhimu wa elimu katika dunia ya sasa" amesititiza Mhe.Kanyasu.
Naye, Diwani wa viti maalum wa Kata ya Bulela,  Mhe, Salome Kitula amesema tatizo la mimba kwa watoto wa shule ni kubwa linahitaji ushirikiano kwa wapenda maendeleo wote.
Amesema jitihada nyingi zimekuwa zikifanyika ikiwa pamoja na kufanya semina na wazazi kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia watoto wakike wakiwa eansonesha mienendo isiyofaa pamoja na kufanya ziara katika shule kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi kuhusu athari za kupata mimba wakiwa bado shule.
Ameongeza kuwa kwa mwaka 2018 takribani wanafunzi zaidi ya kumi walibainika kupata mimba na tayari kesi zinaendelea mahakamani.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  ( wa pili kulia)( akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya ya Geita pamoja na madiwani wa Kata ya Bulela na Shiloleli mara baada ya kuanza mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi wake ahadi mbalimbali alizozitekeleza yakiwemo masuala ya afya, miundombinu pamoja mikopo  tangu walimpomchagua kuwa Mbunge wao.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara akiwaeleza ahadi mbalimbali alizozitekeleza na anazoendelea kutekeleza Mbunge wa Geita mjini, Mhe, Constantine Kanyasu.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Geita mjini, Mhe.Kanyasu wakati wa mkutano wa hadhara katika eneo la  Bulela 
Diwani wa viti maalum wa  Bulela, Mhe, Salome Kitula akizungumza na wananchi wa kata ya Bulela kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na  wananchi.wa kata hiyo
Diwani wa viti maalum wa  Kasamwa, Mhe. Jesca Kalalio  akizungumza na wananchi wa kata ya Kasemwa  kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na  wananchi.wa kata ya Bulela


Comments