- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
TANGU mwaka 1884 fedha zilizotumika Tanganyika zilikuwa ni sarafu, noti zilianza kutumika mwaka 1905 wakati wa utawala wa Mjerumani.Noti hizo zilitolewa katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na 500. Zanzibar mwaka huohuo wa 1905, noti za Rupie za Zanzibar zilitolewa katika thamani za Rupie 5, 10, 20, 50, 100 na 500.Mbali na rupia iliyodumu kwa muda mrefu katika matumizi ya noti nchini, tangu kupatikana uhuru, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekuwa ikibadilisha noti zake kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo sheria inayoiruhusu kufanya hivyo katika kipindi cha miaka mitano mpaka saba.Kutokana na mamlaka hayo, BoT, kuanzia mwaka 1966 imefanya mabadiliko kadhaa ya sura za noti zake pamoja na alama za kiusalama.Pia kutokana na kupanda na kushuka kwa thamani ya shilingi, BoT imekuwa ikitoa noti zenye thamani tofauti tofauti (denomination), kuanzia ile ya Shs. 10 mpaka sasa ambapo noti yenye thamani ndogo ni Shs. 500 huku kubwa ikiwa ya Shs. 10,000.Katika historia ya mabadiliko ya noti, mwanzo kabisa ilikuwa ni mwaka 1966 ambayo yalihusu noti ya Shs. 20 iliyokuwa na sura ya Rais wa Kwanza wa Tanzania na Shs. 100 'Mmasai' pamoja na nyingine iliyokuwa na simba.Ilipofika mwaka 1978, Benki Kuu ilitoa tena noti za Shs. 10 na Shs. 20.Mabadiliko mengine katika sura ya noti yalifanyika miaka ya 1985, 1987, 1989, 1990 kwa kuwa na noti ya Shs. 50 ambayo ilikuwa na sura ya Rais wa Pili Ali Hasani Mwinyi, pundamilia na picha nyingine zilizokuwa zikiashiria mavuno.Noti ya Shs. 1,000 yenye sura ya Rais Mwinyi na tembo iliingia mwaka 1993 na mwaka 1995 ilingia noti ya Shs. 10,000 yenye sura ya Rais Mwinyi na simba.Mwaka 2000 kuliingizwa noti ya Shs. 1,000 ikiwa na sura ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, tembo na mgodi wa makaa ya mawe, wakati mwaka 2003 ilikuja noti ya Shs. 500 ikiwa na picha ya nyati, jengo la Nkurumah lililopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na nyoka.Mwaka huo huo iliingia noti ya Shs. 5,000 ikiwa na faru na mgodi na noti ya Shs. 10,000 ikiwa na jengo la benki na tembo.
Kimsingi mpaka sasa BoT imefanya mabadiliko makubwa ya sura za fedha za Tanzania mara saba, mabadiliko yaliyohusisha rangi, alama (picha) na alama za usalama wa fedha hizo.Mbali na mabadiliko hayo, Desemba 17, 2010 BoT ilizindua noti mpya ambazo zilianza kutumika rasmi kwenye mzunguko wa fedha kuanzia wiki ya kwanza ya Januari mwaka 2011.Wakati wa utambulisho wa noti hizo mwaka 2010, Gavana wa zamani wa BoT, Profesa Beno Ndulu alisema noti hizo mpya zingekuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwemo rangi na alama za utambulisho ambazo zilikuwa na sura za waasisi wa taifa, Mwalimu Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.“Katika noti za sasa, kutakuwa na saini Gavana aliyepo pamoja na Waziri wa Fedha aliyepo madarakani,” alisema Profesa Ndulu.Mabadiliko hayo yalizihusha noti zote na Profesa Ndulu alisema tofauti na za awali, noti za sasa zina alama mpya tatu, zitakazolinda usalama wake dhidi ya watu wanaoghushi ambao alisema uwezo wao unakuwa kila siku kutokana na kukua kwa teknolojia.Alisema alama zilizowekwa ni pamoja na ile iliyojificha ya picha ya Mwalimu Nyerere inayochukua nafasi ya twiga katika noti za viwango vyote.Alama nyingine mpya kabisa katika teknolojia ya utengenezaji fedha ni ile ambayo inaonekana kama inatembeatembea wakati noti inapokuwa ikigeuzwa na nyingine ambayo inabadilika au kugeuka rangi.Kadhalika, alisema mbali na kupunguzwa ukubwa, noti hizo zinatambuliwa kirahisi na walemavu wa macho kutokana na alama maalum zilizowekwa kwa ajili yao katika kila kiwango.Alama hizo ni pamoja na mistari iliyovimba, pamoja na ile ya V ambazo zimewekwa kwa idadi maalum inayoelezea kila kiwango cha noti husika.Mabadiliko mengine yalifanywa katika picha za wanyama simba, nyati pamoja na tembo ambao awali, picha zao zilikuwa zikionyesha miili yao yote, katika noti za sasa ni picha za vichwa vyao tu zinazoonekana.Kitu kingine kinachozitofautisha noti za sasa na zile za zamani ni karatasi zilizotumika kuzitengenezea.Noti za sasa zimetengenezwa kwa pamba kwa asilimia 100 tofauti na noti za zamani ambazo karatasi zake zinatokana na mbao.“Kampuni inayochapisha noti zetu, ndiyo pia inayochapisha baadhi ya denomination (noti) ya Marekani, kwa hiyo karatasi zinazotumika kutengeneza Dola ya Marekani ndizo hizo hizo zinazotengeneza fedha zetu,” alisema Profesa Ndulu.Kwa mujubu wa Profesa Ndulu, mchakato wa kubadilisha noti ulianza Aprili mwaka 2009 na mchakato wa zabuni uliendeshwa na hatimaye makampuni kumi na moja kujitokeza ingawa tisa ndiyo yaliyoingia katika ushindani.Kampuni ya Crane AB ya Sweden ilishinda kutengeneza noti za Shs. 500, Shs. 2,000, Shs. 5,000 na Shs. 10,000 huku kampuni ya Adae La Rue ya Uingereza ikishinda zabuni ya kutengeneza noti za Shs. 1,000.Profesa Ndulu alisema gharama ya uchapishaji vipande 1,000 imeshuka ikilinganishwa na wakati ambao Tanzania ilikuwa ikichapa noti zake katika kampuni ya Giesecke & Devrint ya Ujerumani.“Kama mwanzo tulikuwa tukichapisha vipande 1,000 kwa Shs. 10, sasa tunachapisha kwa Shs. 7,” alisema Profesa Ndulu.Alisema kupungua kwa gharama hizo kunatokana na ushindani katika kupambanisha wazabuni.Anasema kwa kawaida wastani wa noti yoyote kuishi katika mzunguko ni miezi saba na kuwa kutokana na ubora wa noti za sasa, zitaweza kuishi kwa muda huo ili kuipunguzia benki gharama ya kuchapisha fedha mara kwa mara kutokana na uchakavu.Licha ya madai ya kushuka kwa uchumi hivyo kupungua kwa thamani ya shilingi, Profesa Ndulu alisema BoT haina mpango wa kuchapisha noti yenye thamani zaidi ya Shs. 10,000 inayotumika sasa.“Labda mpaka shilingi yetu ifikie pabaya sana, lakini kwa sasa tutaendelea kutumia hizi hizi zilizopo,” alisema Profesa Ndulu.Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Crane AB, Peter Brown, alisema alama za usalama ambazo zimetumika katika utengenezaji wa noti hizo ni teknolojia mpya kabisa ambayo haijawahi kutumiwa na nchi yoyote ya Afrika. Alisema alama hizo ni hatimiliki ya kampuni hiyo ambayo ilitumia miaka mitatu kuzitengeneza.“Kutokana na teknolojia iliyotumika kutengeneza alama za usalama za noti hizo, si rahisi mtu yeyote kuzigushi,” alisema Brown.Pia alisema kutokana na kukua kwa tekinolojia, ni vyema nchi zikawa na utaratibu wa kubadilisha noti zake kila baada ya muda unaoshauriwa kisheria ili kupambana na wimbi la watu waoghushi.Alisema kampuni yake inachapisha noti ya Dola 100 ya Marekani na kuwa teknolojia inayotumika kutengeneza fedha hiyo yenye soko kubwa duniani ndiyo inayotumika pia kutengeneza noti za Tanzania ambazo zinatatengenezwa na kampuni hiyo.
Rupie 10
Rupie 50
Rupie 100
Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo wa 1905, noti za Rupee za Kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee 5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia.
5 Zanzibari Rupee
Wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia, Serikali ya Kijerumani ilitoa noti za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana kupatikana picha zake.
1 Rupie
5 Rupien
10 Rupien
20 Rupien
50 Rupien
Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.
Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili baada ya kwa Dar es Salaama wakati wa Serikali ya Kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa inaitwa "Tabora Pound."- 1 Zanzibari Rupee
- 1 EA Rupee5 EA Rupee
10 EA RupeeKatikati ya mwaka 1920, Serikali ya Uingereza ilianzisha sarafu ya pamoja kwa nchi zote za Afrika ya Mashariki iliyojuliakana kama Florin ya Afrika ya Mashariki. Noti za Florin zilikuwa katika thamani za Florin 1, 5, 10, 20, 50, 100 na Florin 500, ambapo noti za kuanzia Florin 10 na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 2, 5, 10 na 50). Kwa vile sarafu hii haikudumu zaidi ya miezi sita, ni noti chache sana zilizotolewa, mifano ya noti hizo ni kama ifuatavyo:
1 EA Florin
5 EA FlorinMwanzoni mwa mwaka 1921, Serikali ya Kiingereza ilianzisha sarafu ya pamoja Afrika Mashariki iliyojulikana kama Shillingi ya Afrika ya Mashariki na hivyo kuondokana na Florin ya Afrika Mashariki. Shilingi ya Afrika Mashariki ilikuwa na thamani ya Shillingi 20 kwa Pound moja na ilikuwa imeegeshwa kwenye Pound kiasi kuwa thamani ya Shilingi 20 kwa Pound haikubadilika. Noti za Shillingi zilizotolewa wakati huo zilikuwa za thamani za Shillingi 5, 10, 20, 100, 1000, na Shillingi 10,000. Noti za Shillingi 20 na kuendelea juu zilikuwa pia na thamani ya Pound (1, 5, 50). Noti hizi zilikuwa zimeandikwa kwa Kiingereza, Kiarabu na Kiamhara kinachotumika Ethiopia. Katika utawala wote wa Kiingereza, kulitolewa mitindo miwili tu ya noti hizo. Mtindo wa kwanza ulidumu kuanzia mwaka 1921 hadi mwaka 1958, ma mtindo wa pili ulidumu kuanzia mwaka 1958 hadi baada ya Uhuru mwaka 1964. Sura ya mbele ya noti zote ilikuwa ikionyesha Mtawala wa Himaya ya Uingereza. Sura ya nyuma kwa upande wa noti za mtindo wa kwanza ilikuwa na simba mmoja wa kiume katika eneo la mlima Kenya. Noti zilizotolewa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Mfalme George wa Tano (1910-1936) ni kama ifuatavyo:
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
1000 EA Shilling(Picha hii ilipingwa wakati pesa imeshafutwa rasmi kwa kutobolewa matundu; noti halisi haikuwa na matundu hayo)
Kwa thamani ya shillingi na uchumi wa watu wakati huo, ni noti chache sana zenye thamani ya Shilingi 1,000 na Shillingi 10,000 ziliingia kwenye mzunguko, na picha ya noti ya Shilingi 10,000 haikuweza kupatikana.Kwa hiyo ilipofika mwaka 1933, serikali ikaamua kusimaisha matumizi ya noti za Shilingi 1,000 ingawa zile za Shilingi 10,000 ziliendelea.
Wakati wa utawala mfupi wa Mfalme Edward wa VIII mwaka 1936, hazikutolewa noti zozote. Noti nyingine zilitolewa wakati wa utawala wa Mfame George wa VI 1936-1952), ambapo noti ya Shilingi 1 ilianzishwa. Noti hizo zilikuwa kama ifuatavyo.
1 EA Shilling
5 EA Shilling
10 EA Shilling[/
20 EA Shilling[/
100 EA Shilling[/
Kutokana na uadimu wake, picha ya noti za Shilingi 10,000 haikupatikana. Hata hivyo miaka 11 ndani ya utawala wa Mfalme George wa VI, iliamuliwa kufuta noti hizi za Shillingi 10,000 ambazo zilikuwa hazitumiki sana.
Baada ya kifo cha Mfalme George wa VI mwaka 1952 na binti yake Malkia Elizabeth wa II kuchukua usukani, noti zilizotolewa zilikuwa zinafanana na zile zilizokuwapo mwazoni isipokuwa aliondoa noti ya Shilingi 1 kwenye mzunguko.
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling Hata hivyo mwaka 1958, noti hizo zilitengezwa upya katika mtindo tofauti na zile zilizokuwapo mwanzo. Noti mpya zilikuwa na rangi nyingi huku zikionyesha mazao mbali mbali ya uchumi yaliyokuwapo Afrika ya Mashariki.
Noti ya Shilingi 5 ilionyesha pamba na karafuu; noti ya Shilingi 10 ilionyesha mkonge na chai; noti ya Shilingi 20 ilionyesha kahawa na alizeti, na mwisho noti ya Shilingi 100 ilionyesha minazi, miwese na pareto.
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Noti hizi ziliendelea hadi baada ya uhuru ingawa mwaka 1961 zilifanyiwa marekebsihao madogo kwenye sura ya mbele ili kuweza kuonyesha sahihi sita za wajumbe wa bodi ya fedha ya afrika mashariki ambapo wakati huo walikuwa wameongezeka na kuwa sita kutoka watano waliokuwapo mwaka 1958. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling
Baada ya nchi zote za Afrika ya Mashariki kuwa huru, noti za kwanza zilizotolewa mwaka 1964 zilifanyiwa mabadiliko makubwa sana. Kwanza, noti hizi zilikuwa zimeandikwa katika kiingereza, kiarabu na kishwahili; halafu sura ya mtawala wa uingereza iliondolewa na badala yake kuwekwa mashua. Sikuweza kufahamu mara moja kwa nini waliamua kutumia mashua. Sura za nyuma za noti ziliendelea kuonyesha mazao mbalimbali ya Afrika ya Mashariki ingawa kwa mpangilio tofauti kama inonekanavyo katika picha hizi.
5 EA Shilling
10 EA Shilling
20 EA Shilling
100 EA Shilling- Inaelekea kuwa kuanzia hapo, Shilingi ya Afrika Mashariki iliacha kubebeshwa kwenye Pound kwa vile noti mpya hazikuwa na thamani ya Pound tena.
- Baada ya kuvunjwa kwa Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania ilitoa noti za kwanza zenye thamani hizo hizo za Shilingi 5, 10, 20 na Shilingi 100.
- Upande wa mbele wa noti hizi kulikuwa na sura ya Mwalimu Nyerere wakati wa kupata Uhuru, na upende wa nyuma ulionyesha mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
- Noti ya Shilingi 5 ilikuwa na Mlima Kilimanjaro, noti ya Shilingi 10 ilikuwa na shamba la mkonge, wakati noti ya Shilingi 20 ilikuwa inaonyesha mgodi wa almasi wa Mwadui.
- Noti ya Shilingi 100 ilikuwa inaonyesha Morani wa Kimasai akichunga ng'ombe.
5 Tz Shilling
10 Tz Shilling
20 Tz Shilling
100 Tz Shilling
Kwa waliotumia noti hizo wanakumbuka kuwa noti ya Shilingi 10 ilikuwa inajulikana pia kama jani la katani, wakati ile ya 100 ilikuwa inajulikana pia kama Masai au Pink kutokana na rangi yake. Kwa muda mrefu noti ya Shilingi 20 imeendelea kujulikana kama Pound au "Mbao" kutokana na historia kuwa mwanzoni ilikuwa ina thamani ya Pound 1.
Hata hivyo sura ya Masai kwenye noti ilileta mjadala kidogo kiasi kuwa Benki Kuu iliamua kuzibadilisha. Ilipofika mwaka 1969, wakatoa noti za Shillingi 100 ambazo zilikuwa na wanyama katika mbuga ya serengeti kama ionekanavyo hapa chini
100 Tz Shilling
Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 1978 zilipofanyiwa mabadiliko makubwa hasa ili kuondoa sura ya kitoto ya Nyerere na kuweka picha ya Nyerere akiwa mtu mzima. Noti mpya zote zilikuwa zimendikwa kwa Kiswahili tu, na vile vile noti ya Shilingi 5 ilisimamishwa. Upande wa nyuma wa noti zote kulikuwa na ramani ya Tanzania pamoja na sura mbalimbali zihusuzo Tanzania. Noti ya Shilingi 10 ulikuwa na Mlima Kilimanjaro, kinyago cha kimakonde na mnara wa Azimio la Arusha; noti ya Shilingi 20 ilikuwa na kiwanda cha nguo kuashiria kuwa nchi ilikuwa inasonga mbele kiviwanda, na ile noti ya Shilingi 100 ilikuwa tasisi za elimu kuanzia shule za msingi na vyuo vikuu kuashiria juhudi za nchi kupambana na adui ujinga. Vile vile shughuli za elimu ya kujitegemea zimeonyeshwa kwa wanafunzi kulima kwa jembe la mkono.
10 Tz Shilling
20 Tz Shilling
100 Tz Shilling
Miaka saba baadaye, mwaka 1985 (muda mfupi sana kabla Nyerere hajastaafu) noti zilifanyiwa mabadiliko tena kwa kuondoa noti ya Shilingi 10 na kuwekwa kwa noti ya Shilingi 50. Noti hizi zilikuwa na sura ya Nyerere akiwa ameanza kuzeeka, na zilitumia rangi nyingi sana kuliko zilizotangulia. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, noti ya Shilingi 100 ilibadilishwa rangi kutoka "pink" na kuwa ya bluu. Noti ya Shilingi 20 ilionyesha shughuli mbalimbali za baadhi ya viwanda vyetu, wakati Shilingi 50 ilionyesha shughuli za kujitolea kujenga mashule. Noti ya Shillingi 100 ilionyesha wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaama na baadhi ya majengo ya chuo hico. Nadhani ilikuwa pia kuonyesha kuwa nchi imepiga hatua katika upande wa elimu ya juu.
20 Tz Shilling
50 Tz Shilling
100 Tz Shilling
Mwishoni mwa mwaka 1985 Nyerere alirudi kijijini kwake Butiama na kuiacha Ikulu mikononi mwa Mwinyi. Noti mpya zilizotolewa mwishoni mwa mwaka 1986 zilikuwa sawa kabisa na zile zilizoachwa na Nyerere isipokuwa zilikuwa na sura ya Mwinyi ukiacha tu noti zile za Shilingi 100 ambazo ziliendelea kuwa na sura ya Nyerere kama Baba wa Taifa. Vile vile noti mpya ya Shilingi 200 ilianzishwa ikiwa inajulika wakati huo kama "Double Cabin." Nyuma ya noti hizi za Shilingi 200 kulikuwa na wavuvi wanaodhaniwa kuwa walikuwa wa Zanzibar kwa vile kuna karafuu inayoonekana kwa pembeni.
20 Tz Shilling
50 Tz Shilling
100 Tz Shilling
200 Tz ShillingIlipofika mwaka 1988, kufuatia kushuka kwa thamani ya shilingi, ilikuwa ni muhimu kuwepo kwa noti zenye thamani kubwa zaidi ili kuwapunguzia watu mzigo wa pesa. Hivyo Benki Kuu ikaanzisha noti mpya za Shilingi 500, ambao zilijulikana kama "Pajero." Noti hizi za Shilingi 500 zilikuwa na sura tofauti kabisa na zile nyingine. Nembo ya Taifa ilikuwa ya rangi, halafu zilikuwa na nembo ya waziwazi ya Benki Kuu ya Tanzania. Nyuma yake zilionyesha akina mama wakivuna zao la kahawa au karafuu.
500 Tz Shilling
Kasi ya kupungua kwa thamani ya shilingi ilikuwa kali sana kiasi kuwa miaka miwili baadaye, Benki Kuu ililazimika kuingiza noti mpya ya Shilingi 1,000 ambayo ilikuwa na sura kama ile ya Shilingi 500 isipokuwa ngao ya taifa haikuwa ya rangi. Vile vile ilikuwa na maandishi ya ndani kwa ndani kuonyesha 1,000. Nyuma yake kulikuwa kiwanda cha nyama cha Tanganyika Packers cha Kawe.
1000 Tz Shilling
Noti zetu wakati huo zilikuwa pana sana na zilikuwa zinaongezeka upana kadiri thamani yake inavyopanda. Ilipofika mwaka 1992, Benki Kuu ilifanya mabadiliko makubwa katika noti zetu. Kwanza zilipunguzwa sana upana halafu zote zikatengezwa upya kuwa na sura inayofanana. Noti ya Shilingi 20 iliachishwa na badala yake zikaongezwa noti mbili za Shilingi 5,000 na Shilingi 10,000 kama ifuatavyo:
50 Tz Shilling100 Tz Shilling
200 Tz Shilling
500 Tz Shilling
1000 Tz Shilling
5000 Tz Shilling
10,000 Tz Shilling
Noti hizi ziliendelea kutumiwa hadi mwisho wa utawala wa Mwinyi mwaka 1995.- 500 Tz Shilling
1000 Tz Shilling
5000 Tz Shilling
10000 Tz Shilling
Hata hivyo baada ya kifo cha Mwalimu Nyerere mwaka 1999, iliamuliwa kuwa sura yake iwe ya kudumu kwenye noti ya Shilingi 1000, hivyo noti hiyo ilisanifiwa upya na kuwa kama ifuatavyo:
1000 Tz Shilling
Noti hizi ziliendelea kutumika hadi mwaka 2003 zilipofanyiwa mabadiliko ya kuongeza usalama zaidi. Vile vile kutokana na manunguniko ya kichinichini kutokea zanzibar kuhusiana na mtumizi ya Twiga ambaye alikuwa mnyama wa Tanganyika, iliamuliwa kutotumia twiga tena. - Badala yake sura za wanyama wakubwa mbalimbali wa Tanzania zilitumika ingawa sura ya Nyerere iliendelea kubaki kwenye noti za Shillingi 1000. Vile vile noti mpya ya Shillingi 2000 ilianzishwa. Upande wa nyuma wa noti hizi ulionyesha shughuli mbalimbali za uchumi, sehemu za kihistoria na harakati za kukuza elimu.
- Kwa mara nyingine tena kuanzia mwaka 1978, noti hizi ziliandikwa kwa Kiingereza na Kishwahili tena. Noti hizi ndizo zinazotumika hadi leo, sura zake ni kama ifuatavyo
500 Tz Shilling
1000 Tz Shilling
2000 Tz Shilling
5000 Tz Shilling
10000 Tz Shilling - UZALENDO DAIMA!
Comments
Post a Comment