Featured Content Slider

..

..

Featured Post

KILIMO BORA CHA MIPAPAI

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Utangulizi: Mipapai ni moja ya miti ya matunda inayolimwa ulimwenguni kote na hapa Tanzania, ...

Wednesday, March 29, 2017

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AZINDUA ZOEZI LA UTHAMINI

 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.

RC SIMIYU MALIZA MGOGORO WA WANAKIJIJI NA WAWEKEZAJI


Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Meatu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo.

WAKURUGENZI NCHINI WACHAGUA VIONGOZI WAO MD KAYOMBO JOHN AWA MWEKA HAZINA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA wa Wakurugenzi nchini.

SHIRIKA LA EfG LAPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA MCHIKICHINI NA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Soko la Ilala Mchikichini, Jumanne Kongogo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kupungua vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya kufanyika kampeni mbalimbali za kupinga ukatili huo zilizofanywa na Shirika la Equality for Growth (EfG) kwa kipindi cha miaka mitatu.

MTANZANIA ALIYEWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MUDA MFUPI AMUANGUKIA WAZIRI MWAKYEMBE

Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.

Tuesday, March 28, 2017

BoT YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA FEDHA

Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi,  Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.

HATIMAYE PAUL MAKONDA AZUNGUMZA BAADA YA KUSAKAMWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amethubu kuongea baada ya kusakamwa kwa muda mrefu na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Na vita yake, ambayo ilianzia tangu wakati ule alipotangaza vita na operesheni dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya kabla ya kupamba moto kuhusu tuhuma za kughushi vyeti na hatimaye kuvamia kituo cha runinga cha Clouds TV, imeonekana kuwa kubwa.

MWANAHABARI GEORGE BINAGI WA LAKE FM MWANZA AUAGA UKAPELA.

Jana March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.

Newsletter

Services