- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MSHUBIRI au msubili ni jina la mimea ya jenasi Aloe katika nusufamilia Asphodeloideae ya familia Xanthorrhoeaceae ambayo ni aina za sukulenti, yaani mimea yenye majimaji.
Huu ni
mmea maarufu sana duniani kutokana na kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi,
na pia unapatikana sehemu nyingi za dunia hasa zile ambazo hazina baridi.
Vipodozi vingi vya ngozi vinachanganywa na mmea huu ili kuvipa uwezo zaidi wa
kutunza ngozi.
Mimea au miti hii ya mishubiri ina shina fupi au haina shina kabisa, isipokuwa
spishi zilizo miti. Majani ni marefu na mapana na yanatoka katika shina karibu
na wenziwe kama yalivyo majani ya mkonge; lakini majani ya mshhubiri yana miiba kingoni mwao.
Maua yana umbo la mrija mfupi na yanaweza kuwa ya rangi
nyekundu, huzurungi,
ya machungwa, njano au nyeupe ambapo mara nyingi ypo mwishoni mwa kikonyo chenye vitawi au bila vitawi.
Utomvu utokao kwenye majani haya ndio hutumika
kutengeneza dawa.
Spishi ambayo inajulikana sana ni mshubirimani (Aloe vera), ambao unapandwa
sana duniani na
hutumika kwa kutengeneza dawa za uganga au
za mitishamba.
Spishi nyingine inayopandwa sana katika Afrika na
nchi nyingine za Tropiki ni mshubiri
mwekundu (A. ferox).
Mmea huu
unatumika zaidi kama majani ingawa shina na mizizi yake nayo ni dawa pia, mmea
huu huwa na umbo la mkonge au mmea wa nanasi ila wenyewe ni mdogo kidogo
na huwa laini zaidi.
Majani
yake yana sehemu mbili, kuna ganda la nje na maji ya ndani (jelly) ganda la nje
lina kemikali za kutibu zaidi na ule utando wa ndani una virutubusho vingi sana
ambavyo ni kinga za mwili.
Mshubiri ni mmea wenye ‘miujiza’
ya kutibu maradhi sugu kama Saratani, Kisukari, lehemu (cholesterol), malaria sugu, ugonjwa
wa kuvimba sehemu ya mwili, vidonda, muwasho wa ngozi na harara, husaidia kusaga chakula,
hupunguza uvimbe, na magonjwa mengine mengi.
Hivi sasa watu wengi wamekuwa
na utamaduni wa kuweka Aloe ndani ya familia zao kutokana na mmea
huo kuwa na faida za kutibu magonjwa mbalimbali.
Si hivyo tu, pia hivi sasa kuna bidhaa nyingi
zinazotengenezwa kwa kuchanganya aloe
vera kama sabuni za kuogea, dawa za meno, mafuta ya kulainisha ngozi
(lotion) na bidhaa nyinginezo nyingi.
Kwa zama
nyingi, jamii mbalimbali katika Tanzania na Afrika zimekuwa zikitumia mshubiri
kwa mambo mengi, hata inapofikia mama anataka kumwachisha ziwa mtoto hupaka
maji maji ya mshubiri kwenye chuchu zake.
Mtoto
anaponyonya na kuonja ladha chungu huwa hawezi kurudia tena kunyonya, na hapo
huendelea kutumia chakula mbadala.
Binafsi
hata mama yangu aliniambia kwamba niliacha nyonyo baada ya kupakaza shubiri,
ambapo kule Dodoma wanauita ‘Litembwe’.
Kama
unasumbuliwa na homa ya malaria mara kwa mara, chukua majani mawili yaliyo
komaa, yaoshe vizuri na kata kata katika vipande vidogo.
Changanya
na maji vuguvugu kisha saga kwa kutumia kisagio au twanga kwenye kinu kidogo,
chuja na kisha ongeza maji hadi upate bilauri nzima, unaweza kuhifadhi dawa hii
kwenye jokofu.
Kunywa
vikombe viwili mpaka vitatu kwa kila siku kwa siku 5 - 7.
Hii itakusaidia kuongeza kinga ya mwili wako maradufu na unaweza kurudia dozi
hii mara baada ya miezi 3 - 4.
Zifuatazo
ni faida lukuki za Aloe Vera, yaani
mshubirimani:
1. Husaidia kukaza uke
Mara kadhaa imeelezwa kwamba kuna
wanawake ambao ‘wananunua bikira’ ili waendelee kuonekana bado kabisa! Lakini
huko walikokuwa wananunua yawezekana kuna watu walikuwa wanatengeneza ama
wanaendelea kutengeneza fedha kwa miti shamba, na mti wenyewe ni mshubiri.
Shubiri husaidia kukaza misuli
iliyolegea. Kwamba unaweza kuchukua aloe
vera fresh, chukua jeli yake (maji maji yake) na upakae huko ndani kutwa
mara 2 mpaka 3 kwa wiki 3 mpaka mwezi mmoja hivi utaona matokeo yake
yataonekana.
Wapo wanawake ambao wanaeleza kwamba,
baada ya kutumia ama kupaka aloe vera katika sehemu zao za siri mara nyingi
wanasema maumbile yao hukaza na kurejea kwenye ‘usichana’ kana kwamba bado
wangali bikira.
2. Hutibu maambukizi katika uke
Unaweza kutibu maambukizi katika uke kwa
kupakaa jeli ya aloe vera kwa nje na
kwa kuinywa jeli kupata faida yake ya kutibu fangasi. Mililita 70 mpaka 100 za
jeli ya aloe vera kila siku zinaweza kusaidia kutibu maambukizi na fangasi
katika uke na ikiwa utaendelea kuinywa kwa muda mrefu kunaweza kuzuia
maambukizi zaidi kutokujirudia baadaye.
Pia hutumika kurudishia uke uliolegea,
pakaa tu huko jeli fresh ya aloe vera
kila siku na hutakawia kuwa binti mdogo tena. Dawa nyingine kwa ajili hii ya
kurudisha uke uliolegea ni unga wa mbegu za maembe.
3. Hulainisha sehemu kavu za siri
Aloe
Vera hufanya kazi kama
kilainishi bora kabisa cha asili katika maeneo ya siri kwa jinsia zote mbili na
kutoa unyevunyevu wa asili.
4. Hutibu bawasiri
Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu
uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa
mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri.
Chana tawi la aloe vera freshi na
upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka
tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi
hapo uvimbe huo utakapopotea.
5. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo
Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo
na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa
chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya
kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa robo lita, changanya vizuri
mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo
ya tumbo kama kuum, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.
Madhara
ambayo yameripotiwa kutokana na kunywa aloe vera ikiwa freshi kupita kiasi
ndani ya tumbo ni pamoja na kuharisha na matatizo kwenye figo.
6. Huondoa Makeup
Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye
jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.
7. Husafisha ngozi na kuondoa alama zitokanazo
na kuungua na jua
Chunusi, ukurutu na kuungua kwa ngozi
kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone
umepona kabisa. Mshubiri pia una sifa ya kupoza kama ilivyo menthol ambayo unaufanya mshubiri kuwa dawa ya
asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.
8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya
kunyoa
Aloe
Vera ni dawa ya asili
katika kutibu michubuko asante kwa vimeng’enya vyake ambavyo huwa na kiasi
kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu
pakaa jeli ya aloe vera na hata baada
ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo
na kunyoa.
9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo
zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na
kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe vera na mafuta ya asili ya nazi
utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika
ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji
ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na
unyevunyevu muda wote.
10. Hutibu homa, malaria na mafua
Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mshubiri una viinilishe vingi
sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una
orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine mhimu.
11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama
(Vegans)
Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria
wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria
huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.
12. Huongeza nguvu mwilini
Matumizi mengine ya kitabibu ya aloe vera ni kuongeza usawa wa nguvu
mwilini. Hii ni kutokana na uwepo wa vitamin b 14 na viinilishe vingine ambavyo
husaidia kubadili asilimia kubwa ya chakula katika tumbo lako na kuunda nguvu.
13. Huondoa mba kichwani
Changanya jeli ya asili ya aloe vera na shampoo yako, dakika chache kabla ya kwenda
kulala pakaa vizuri mchanganyiko huo kwenye nywele zako na uache zikauke kidogo
na usafishe nywele zako asubuhi.
14. Huondoa maumivu wakati wa hedhi
Changanya jeli ya Aloe vera na pilipili manga ya unga kidogo, meza kijiko cha chakula
kimoja mara tatu kwa siku kila siku hadi maumivu yatakapoacha.
15. Hulainisha nywele
Jeli ya Aloe vera ni nzuri katika kutibu tatizo la nywele kujisokota na ni
mbadala mzuri kwa bidhaa nyingi za madukani zenye gharama kwa ajili ya nywele.
16. Ni dawa ya asili ya kusafishia mdomo
Changanya jeli ya aloe vera ml 100, vijiko 3 vya chai vya baking soda, maji ml 100 na kijiko 1 kidogo cha juisi ya limao.
Changanya vizuri vyote kwa pamoja na utumie kama dawa yako ya asili ya
kusafishia mdomo.
17. Hutibu matatizo katika mmeng’enyo wa
chakula
Juisi ya Aloe vera ni nzuri sana katika kurekebisha matatizo katika
mmeng’enyo wa chakula, hurekebisha kuvurugika kwa tumbo na kiungulia. Itumie
kama ilivyoelezewa kwenye kutibu matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.
18. Hushusha lehemu (Cholesterol)
Tafiti zimeonyesha kuwa kunywa juisi ya aloe vera kwa kipindi kirefu kunaweza
kushusha kiwango cha lehemu mwilini. Itumie kama ilivyoelezewa kwenye kutibu
matatizo ya tumbo hapo juu namba 4.
19. Hutibu chunusi
Aloe
Vera huondoa chunusi kwa
kuziondoa seli zilizokufa katika ngozi na hivyo kuvifungua vishimo katika ngozi
na kuondoa mafuta yaliyoganda katika hivyo vishimo. Pakaa jeli ya aloe vera moja kwa moja katika eneo
lililoathirika na chunusi. Pia makovu yaliyoachwa kutokana na chunusi yanaweza
kuondolewa kwa kupakaa jeli ya aloe vera
pekee.
20. Hutibu ukurutu na upele
Ukurutu ambao ni matokeo ya juu ya
tetekuwanga kwa kawaida hutokea kwa watu wazima wenye kinga ya mwili pungufu. Aloe Vera inaweza kutumika kutibu
tetekuwanga zinazosababishwa na kirusi aina ya herpes virus. Kwa kupakaa jeli
ya aloe vera moja kwa moja kwenye sehemu zilizowazi hutanua mishipa ya damu
jambo linalosaidia kutibu vidonda.
21. Huzuia ngozi kuunguzwa na jua (Sunscreen)
Kupakaa jeli ya Aloe Vera katika mwili hulinda ngozi dhidi ya miale yote ya jua
kutua moja kwa moja kwenye ngozi na hivyo kukufanya usizeeke mapema, pia ni dawa
nzuri kwa ngozi inayofubaa.
22. Huziimarisha kucha dhaifu
Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote
juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa
zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.
23. Hutibu vidonda katika mdomo
Mshubiri unazo vitamini na asidi amino
ambazo husaidia kuzitengeneza upya tishu zilizoharibika. Tafiti zimeonyesha
kuwa watu wanaosumbuliwa na vidonda mdomoni waliotumia jeli ya aloe vera walifanikiwa kutibu karibu
asilimia 50 haraka zaidi kuliko wale ambao hawakutumia jeli ya aloe vera.
24. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo
itokanayo na ujauzito
Anza kwa kupakaa majimaji ya mshubiri juu
ya tumbo lako na ufanye kama upunaji (massage)
hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na
baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.
25. Huondoa uvimbe katika jicho
Weka kiasi kidogo cha majimaji ya aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi,
acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza
kuloweka pamba katika majimaji ya mshubiri na kisha jisafishe katika jicho
lenye uvimbe.
26. Husaidia wawindaji
Wawindaji wa wanyama katika barani Afrika
mara kwa mara hupakaa jeli ya aloe vera
katika miili ili kupunguza kutokwa jasho na kuondoa harufu yao ya asili katika
mwili isisikike na wanyama.
27. Suluhisho kwa watafuna kucha
Burashi kucha za mtoto anayependa
kutafuna kucha na jeli ya aloe vera,
ile ladha ya uchungu katika aloe vera
itamfanya aache kuzitafuna kucha zake.
28. Hutumika katika kupunguza uzito
Watafiti wameweza kugundua kuwa kunywa
juisi ya aloe vera husaidia kupunguza
sukari kwenye damu jambo mhimu kwa wale wenye kisukari cha aina ya pili.
Wanasayansi wanaamini kuwa kuweka kiwango cha sukari chini hupunguza uzito.
29. Hutibu upungufu wa damu (Anemia)
Kunywa jeli ya aloe vera kunasaidia uzalishaji zaidi wa seli nyekundu za damu
katika mwili wako na hivyo kutibu tatizo la kupungua kwa damu.
30. Huondoa maumivu ya mishipa
Kutokana na sifa yake ya kutibu uvimbe,
unaweza kutibu uvimbechungu (inflammation) katika maungio yanayopelekea maumivu
katika mishipa kwa kupakaa jeli ya aloe
vera katika eneo unalosikia maumivu.
31. Hutibu maumivu katika sikio
Matone kadhaa ya aloe vera yakinyunyizwa sikioni yanaweza kuleta nafuu kubwa kama
unapatwa na maumivu katika masikio. Hii ni nzuri pia kwa masikio yanayotoa
usaha na maumivu mengine katika masikio.
Hapa chini tazama video juu ya namna ya
kuandaa jeli ya mshubiri nyumbani kwako na kuinywa kama juisi. Ingawa huyu dada
kwenye video analiondoa lile ganda lake la juu lenye rangi ya blue, bado
unaweza kuisaga pamoja na maganda yake (isipokuwa ile miiba yake) na bado ikawa
nzuri zaidi.
Comments
Post a Comment