- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Na Daniel
Mbega
JUNI 11,
2016 Yanga ilifanya uchaguzi uliomrudisha madarakani mwenyekiti wake Yussuf
Mehboob Manji, ambaye ametangaza kuachia ngazi hivi karibuni.
Kulikuwa na
mvutano mkubwa wakati wa kuelekea uchaguzi huo ambapo hatimaye Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) likasema kwamba uchaguzi wa klabu hiyo ungefanyika chini ya
katiba iliyosajiliwa Msajili wa Vyama na Klabu wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT).
Lakini klabu
hiyo kongwe kabisa nchini Tanzania ilipata katiba yake ya kwanza mwaka 1968
kabla ya kuwepo kwa hizi ambazo zimekuwa zikilumbaniwa.
Katiba hiyo
iliandaliwa na Mzee Mangara Tabu Mangara, mtu muhimu katika historia ya klabu
hiyo ambaye hata hivyo alitimuliwa na kundi la wanachama lililojiita ‘Yanga
Bomba’ mwaka 1976 baada ya kuvuliwa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati na
klabu ya Luo Union ya Kenya.
Mangara,
pamoja na wachezaji waliofukuzwa Yanga, wakaenda kuanzia klabu ya Pan African
na ndio ukawa mwanzo na asili ya Yanga-Raizoni na Yanga-Kandambili.
Hii hapa
ndiyo katiba ya kwanza ya Yanga yam waka 1968:
Comments
Post a Comment