HARUSI YA FLORA MBASHA NA DAUDI APRILI 30 MWANZA, MAANDALIZI YAKAMILIKAFlora Mbasha 'Madame Flora'
NDOA ya pili ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha maarufu kama ‘Madame Flora’, inatarajiwa kufungwa Jumapili ya Aprili 30, 2017 jijini Mwanza ambapo maandalizi yanaendelea vizuri.

 Flora Mbasha na mumewe wakati wa mgogoro wao wa ndoa.
Taarifa zinaeleza kwamba, mwimbaji huyo, ambaye alishinda kesi yake ya talaka dhidi ya mumewe Emmanuel Mbasha katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, hivi sasa anatarajiwa kufunga ndoa na mtu aliyefahamika kwa jina moja la Daudi.
Hata hivyo, wakati zimesalia siku chache, tayari mwanamama huyo mwenye watoto wawili wa baba tofauti ni mjamzito kwa mujibu wa habari za ndani kutoka kwa watu walio karibu naye.
Wakati ambapo Emmanuel Mbasha, ambaye naye ni mwimbaji wa Injili, alikuwa akimbembeleza mkewe warudiane licha ya mkewe huyo kuzaa nje ya ndoa, inaonekana Flora alikuwa amedhamiria kuachana kwa hali na mali na hakuweza kusikiliza upatanisho wowote uliofanywa baina yao.
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha enzi za furaha ya ndoa yao.
Ugomvi baina ya Emmanuel na Flora uliibuka mwaka 2014 baada ya mumewe kumtuhumu kwamba alikuwa na uhusiano na Askofu Josephat Gwajima na akamtuhumu kwamba ndiye chanzo cha kuparaganyika kwa ndoa yake.
Wakati mumewe akiendelea kumtuhumu mkewe huku kukiwa na ugomvi wa ndani, ghafla Emmanuel Mbasha akadaiwa kumbaka shemeji yake, binti yatima ambaye walikuwa wakiishi naye. Wakati huo Flora alikuwa amekimbia nyumbani na Mbasha akadai kwamba alikuwa nyumbani ama alihifadhiwa mahali na Gwajima.
Hofu hiyo iliongezeka baada ya kunasa miamala katika akaunti ya mkewe ambaye alikuwa ameingizwa zaidi ya Shs. 9 milioni katika benki tofauti na watu tofauti.
 Familia ya Mbasha ilipokuwa na furaha tele.
Mbasha alimtuhumu Gwajima kwamba yeye ndiye aliitia najisi ndoa yao na akasema askofu huyo aliwahi kusafiri na mkewe kwenda naye Uingereza.
Ni katika kipindi hicho ambapo ilifahamika pia kwamba Flora alikuwa mjamzito, mimba ambayo Mbasha alisema siyo yake na aliendelea kudai kwamba ni ya Gwajima.
Flora, ambaye anajiandaa kufyatua albamu yake ya sita, inadaiwa kwamba baada ya kutengana na Emmanuel alikuwa na uhusiano na mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Peter, ambaye vyanzo vingine vinasema ndiye baba wa mwanaye wa pili.Hata hivyo, uhusiano wao huo unadaiwa ulivunjika mwishoni mwa mwaka 2016 na ndipo zikaibuka habari za uchumba mpya na mtu anayeitwa Daudi, ambaye ndiye watakayefunga naye ndoa.Haijajulikana kama kuachana kwake na Peter kumesababishwa na mchumba huyo mpya au la.
MaendeleoVijijini ilijitahidi kumtafuta Flora kwa simu kuzungumzia maandalizi ya harusi yake pamoja na suala la mimba, lakini mara zote simu hiyo ilionekana kuwa imezimwa.
Eti kawaida yake!
Kuna taarifa zinadai kwamba, mwimbaji huyo wa Injili amekuwa na tabia ya kuwakimbia wachumba wake kama hii hapa iliyochapishwa mwaka 2014 wakati wa kilele cha ugomvi wake na mumewe ambayo bado inaendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii:
“Flora Mbasha alikuwa na mchumba anaitwa Imma Lugisha huko Mwanza kabla hajaja Dar. Akiwa amechumbiwa tayari, wiki mbili kabla ya kufunga ndoa Flora akapata safari ya kwenda UK ambako wenyeji wake walimshauri kwamba kwa uzuri wake atapata mume Mzungu mwenye pesa kuliko Imma yule wa Mwanza.
Ili kumkimbia Imma, Flora na familia yake wakamtengenezea ishu Imma mchumba wake kwamba ana Ukimwi, kwa hiyo Flora hawezi kuolewa naye. Mpaka leo Imma hajawahi kuoa tena na wala hana hamu. Kumbe hili la kumsingizia mumewe kumbaka mdogo wake hakuna jipya kwa wanaomjua vizuri ila ilikuwa tu the matter of time kabla hanaswa!!”