Featured Post

TUZO YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YAPELEKWA KWA WANANCHI WA MIKOA YA MARA NA SIMIYU

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla akiwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara, Adam Malima na wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati wa kuionesha kwa wananchi wa mikoa hiyo miwili tuzo iliyopata Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya kuwa Hifadhi Bora barani Afrika. Wengine Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu (kulia) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibook (kushoto).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla akizungumza wakati wa sherehe za kuoinesha kwa wananchi wa mikoa ya Mara na Simiyu tuzo iliyopata hifadhi ya Taifa ya Serengeti ya kuwa Hifadhi Bora Barani Afrika.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo katika uwanja wa Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti. 
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika sherehe hizo zilizo udhuliwa na viongozi mbalimbali zikiwemo kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Mara na Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza katika sherehe hizo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loibook akizungumza katika sherehe hizo alipomuwakilisha Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA, Dkt Allan Kijazi.
Waziri wa Malisili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya za mikoa ya Mara na Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wakati akitizama ngoma kutoka kikindi cha wananchi wa jamii ya Maasai wakati kikitumbuiza katika sherehe hizo.
Kamishna Msaidizi - Mawasiliano TANAPA, Pascal Shelutete aakifanya utambulisho wa viongozi mbalimbali waliofika kwa ajili ya sherehe hizo.
Baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali za serikali za mikoa ya Mara na Simiyu walipata fursa uya kupiga picha na tuzo hiyo kabla ya kupelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV.

Comments