Featured Post

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPIGIA DEBE WASANII NA WABUNIFU AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harson Mwakyembe akizungumza wakati wa kufunga rasmi kongamano la Pili la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji lilokuwa la siku mbili  leo Oktoba 12, 2018, Jijijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harson Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa msanii wa sanaa za kuchora wa Nchini Uganda, Msanii Tibirusya Rolands ambaye alichora mchoro maalum unaoonesha taswira ya Sanaa kwa nchi za Afrika Mashariki.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harson Mwakyembe akitia saini kwenye  mchora wa ubunifu wa Msanii wa sanaa za kuchora kutoka Nchini Uganda, Msanii Tibirusya Rolands ambaye alichora mchoro maalum unaoonesha taswira ya Sanaa kwa nchi za Afrika Mashariki.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na  washiriki wakati wa kufunga rasmi kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji lilokuwa la siku mbili  leo Oktoba 12, 2018, Jijijini Dar e Salaam.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwakilishi wa Waziri wa Utamaduni wa Sanaa wa Uganda, Bi. Eunice Tumwebaze wakati wa kufunga rasmi kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji lilokuwa la siku mbili  leo Oktoba 12, 2018, Jijijini Dar e Salaam.
Na Andrew Chale, Dar
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Mhe. Dkt Harson Mwakyembe ameziomba sekta za uwezeshaji na mashirika kujitokeza kwa wingi kusaidia juhudi za Wabunifu wa kazi za Sanaa ili kukuza sekta hiyo kwa Nchi za Afrika Mashariki.
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo jana jioni Oktoba 12, 2018 wakati wa kufunga rasmi Kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji  (2nd Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’
Akitoa neno la kufunga kongamano hilo, Dkt. Mwakyembe amebainisha kuwa, sekta ya ubunifu Afrika Mashariki imekuwa kwa haraka sana  na inawahusisha Vijana wengi sana kwa sasa lakini Ukanda wa Afrika Mashariki hawakujiandaa vizuri kisheria, kimfumo kiasi hata kukosa takwimu sahihi za kazi za wabunifu.
Akijibu baadhi ya hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika kongamano hilo, Dkt. Mwakyembe amebainisha kuwa, kasi za vijana wabunifu na haki zao zinapitia kwenye changamoto kubwa sana hivyo endapo watapata wadau wa kuwasaidia basi sekta hiyo itakuwa kubwa zaidi na yenye faida licha ya changamoto hizo za kisheria, kimfumo na masuala mengine yenye changamoto kwao.
“Niwapongeze waandaaji wa kongamano hili kwani mumeona mbali na nina hakika wabunifu hawa watatoka na kitu cha kujifunza licha ya changamoto wanazokumbana nazo.
CDEA na COSOTA  nawashauri mwakani mkutano unaofuata ufanyikie Arusha ili washiriki wengi zaidi kutoka Afrika Mashariki wafike kwa wingi lakini pia muwaalike pia wadau wengine Waziri wa Fedha na Mipango, TRA na wengine kwa pamoja tujadili kwa kina namna ya kuwapatia mitaji wabunifu wetu.
Aidha, Dkt. Mwakyembe ameonesha kusikitishwa na vijana namna wanavyodurufu kazi za wabunifu wengine pasipo makubaliano na wahusika.
“kwa sasa kazi za DVD na CD hailipi. Kuna vijanawanaishi kwa kunyonya kazi za sanaa kwa kutumia vitu mbalimbali ikiwemo ‘flash disc’, wewe pita tu Kariakoo na utawaona wamerundikana hapo huku wakijiona ni haki yao kufanya hiyo kazi.” Alieleza Dkt. Mwakyembe
Na kumalizia kuwa, Afrika ya Mashariki wanatakiwa kufanya kazi ya pamoja katika uwekezaji kuwasaidia wabunifu.
Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki  la  (Culture and Development  East Africa - CDEA), kwa kushirikiana na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), pia OSIEA na British Council.
Kongamano hilo linatarajiwa hapo baadae kuwa na suluhisho juu ya wabunifu kupata mikopo kutoka kwa wadau wenye mitaji.
Pia washiriki wengine waliojumuika kwenye kongamano hilo ni pamoja na Wadau wanaoshughulikia masuala ya haki miliki kutoka serekalini na  mashirika kama CISAC, wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wizara zinahohusika na haki miliki toka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,
Benki ya Maendeleo  Afrika Mashariki, Benki za kiuchuni, wawekezaji wa Afrika mashariki, mawakili wa haki miliki, vyombo vya hakimiliki vya Afrika Mashariki na wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wameudhuria kongamano hilo.

Comments