- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
JUBA, SUDAN KUSINI
MAHAKAMA ya kijeshi imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya
kati ya miaka saba na maisha kutokana na ghasia ambapo mwandishi wa habari
aliuawa na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu kubakwa.
Mahakama imeiamrisha serikali ya Sudan Kusini kumlipa kila
muathiriwa wa ubakaji dola 4,000 kama fidia.
Uhalifu huo ulitokea wakati wa shambulizi lililofanywa
katika hoteli ya Terrain kwenye mji mkuu Juba mwaka 2016.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliwalaumu walinda amani kwa
kushindwa kuitikia msaada wa waathiriwa.
Wanajeshi wa Sudan Kusini wamelaumiwa kwa kuendesha uhalifu
mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 lakini hili
ndilo lilikuwa shambulizi baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni.
Hii ndiyi mara ya kwanza wanajeshi wameshukiwa kwa kuendesha
uovu Sudan Kusini, taifa janga zaidi duniani ambalo lilipata uhusu wake mwaka
2011.
Kipi kilifanyaika
mahakamani?
Mahakama iliiamrisha serikali iilipe familia ya mwandishi wa
habari John Gatluak ngombe 51 kama fidia.
Alikuwa akichukua hifadhi kwenye hoteli hiyo wakati aliuawa.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi akikaguliwa alipowasili kuhukmiwa
Wanajeshi wawili walipatikana na hatia ya kumuua na
kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Wengine watatu walipatikana na hatia ya kuwabaka wafanyakazi
wa kuto misaada, wanne kwa dhuluma za kingono na mwingine kwa wizi wa kutumia
nguvu.
Walihukumiwa kati ya vifungo vya miaka 7 na 14 jela.
Shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mapigano makubwa mjini
Juba kati ya vikosi vya serikali na vile vya waasi.
Zaidi ya watu 70 wakiwemo wakiwemo walinda amani wawili wa
Umoja wa Mataifa waliuawa wakati wa mapigano ya siku tatu.
Watoa misaada wa kigeni walibakwa wakati wanajeshi walivamia
hoteli hiyo.
Watu wamesema nini
kuhusu hukumu hizo?
Wakili aliyewakilisha waathiriwa wa ubakaji Issa Muzamil
Sebit alisema wateja wake hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
Fidia waliyopata ilikuwa ya aibu, aliongeza.
Naye wakili wa washtakiwa Peter Maluang Deng alisema
alishangazwa na hukumu hiyo akisema atakata rufaa.
Hata hivyo Amnesty International imekaribisha hukumu hizo.
Kesi hii ina maana
gani
Serikali ya Afrika Kusini itatumia fursa hii kudai kuwa
inapambana na dhuluma zilizofanywa na wanajeshi.
Lakini hiki kilikuwa ni kesi cha kiwango cha juu ni nadra
kuona wanajeshi wakiletwa mbele ya hukumu kwa dhuluma walizotendea raia wa
kawaida.
Jeshi katika pande zote mbili za mzozo zinaonekana kuwa na
wakati mgumu kudhibiti wanajesi wao.
Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu
yamewalaumu kwa kuendesha uhalifu wa kvita
Mwaka 2015 Muungano wa Afrika ulitoa wito wa kubuniwa kwa
mahaka,a maalum kuwahukumu washukiwa wa uhalifu wa kivita. Lakini hilo bado
halijafanyika.
Comments
Post a Comment