- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NEW DELHI, INDIA
MAHAKAMA ya Upeo nchini India imefanya maamuzi ya
kihistoria, toka leo, kushiriki mapenzi ya jinsia moja si kosa la jinai nchini
humo.
Hukumu ya leo inatengua maamuzi yaliyofanywa mwaka 2013
ambayo yalidumisha matumizi ya sheria ya kikoloni, maarufu kama kanuni ya 377
ambayo ilitia hatiani vitendo vya ushoga.
Mahakama sasa imeamua kuwa kuwabagua watu kutokana na
mahusiano yao ya kimapenzi ni ukiukwaji wa haki za binaadamu.
Wapigania haki za ushoga walilipuka kwa furaha na wengine
walishindwa kuyazuia machuzi pale hukumu hiyo ilipokuwa ikisomwa.
Ijapokuwa maoni ya wengi kwenye miji mikubwa ya India
yamekuwa yakiunga mkono ushoga, kuna upinzani mkali kutoka katika makundi ya kidini
na wahafidhina hasa maeneo ya vijijini.
Majaji wote watano wa mahakama hiyo wakiongozwa na Jaji Mkuu
wa India, Dipak Misra, walikubaliana kuwa ushoga sio kosa la jinai.
Jaji Misra amesema kutia hatiani mapenzi ya jinsia moja ni
kinyume cha katiba ya India. Jaji mwengine wa mahakama hiyo Indu Malhotra,
amesema anaamini historia inabidi iiombe radhi jamii ya mashoga kwa
kuwanyanyapaa.
Jaji DY Chandrachud amesema serikali haina haki juu ya
maisha binafsi ya mashoga na kuwanyima haki yao ya kufanya mapenzi ni sawa na
kuwanyima faragha.
Hukumu hiyo sasa inaruhusu mashoga kufanya mapenzi kwa
faragha.
Kanuni ya 377 ilipitishwa na wakoloni wa Kiingereza miaka
157 iliyopita na kutia hatiani matendo yote ya ulawiti, mapenzi ya jinsia moja
na kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo.
Vuguvugu la kuiondoa kanuni hiyo lilianza mwaka 2001 na
mwaka 2009 suala hilo lilitua mahakamani jijini Delhi ambapo mahakama kuu ya
jiji hilo iliamua kuifuta kanuni hiyo.
Hata hivyo, makundi ya kihafidhina, na kidini yakidini
yaliweka msukumo kwa kurudishwa kwa sheria ya kuharamisha ngono ya watu wa
jinsia moja na mwaka 2013 mahakama ya upeo ikarudisha kanuni 377.
Hatua hiyo haikuwavunja moyo wanaharakati wa haki za mashoga
ambapo waliiomba mahakama ya upeo kupitia upya maamuzi yake wakisema hyakuwa ya
haki. Mwaka 2016 mahakama hiyo ilikubali ombi hilo na leo maamuzi ya mwisho
yameamuliwa.
Mwanaharakati Harish Iyer ameiambia BBC kuwa: "Nina
furaha isiyokifani. Ni kama tumeshinda mapambano ya pili ya ukombozi na
hatimaye tumeiondosha sheria ya Mwingereza nchini mwetu…"
CHANZO: BBC
Comments
Post a Comment