- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NEW YORK, MAREKANI
RAIS wa Marekani Donald Trump amekana madai ya mwandishi
maarufu Bob Woodward katika kitabu chake kipya kwamba aliamrisha mauaji ya rais
wa Syria, Bashar-al-Assad.
Trump anasema kuwa wazo hilo halikuzungumziwa na maafisa wa
ulinzi.
Waziri wa ulinzi James Mattis pia amekana madai ya maneno
aliyotoa katika kitabu hicho. Rais Trump tayari ameshutumu kazi hiyo mpya kama
'kuwalaghai' raia na ya 'uongo'.
Woodward ni mwandishi wa muda mrefu ambaye alisaidia kuweka
wazi jukumu la rais Richard Nixon katika kashfa ya Watergate 1970.
Siku moja baada ya nakala za kitabu hicho kuchapishwa katika
gazeti la The Washington Post, gazeti jingine la The New York Times
lilichapisha maoni yaliotolewa na afisa mwandamizi katika Ikulu ya Whitehouse
akisema kuwa kiini cha tatizo la utawala wa rais Trump ni ukosefu wa 'maadili'.
Ofisa huyo anasema kuwa maafisa wa serikali walioteuliwa na
Trump waliapa kusitisha amri za rais Trump.
''Huenda kuna baridi nyingi wakati huu lakini raia wa
Marekani ni sharti wajue kuna 'watu wazima' katika chumba hiki," maofisa
hao wanaongeza.
''Tunatambua kinachoendelea. Na tunajaribu kufanya kilicho
sawa hata iwapo Donald Trump hatofanya."
Baadaye siku hiyo, Trump aliuambia mkutano wa maofisa wa
polisi wa kieneo kwamba kitabu hicho kina aibu.
Msemaji wake Sarah Sanders alisema katika taarifa kuhusu
mwandishi huyo ambaye hakutajwa. ''Huyu muoga anafaa kufanya kilicho sawa na
kujiuzulu."
Ni nini kilichosemwa kuhusu Assad?
Kitabu hicho kinasema kuwa bwana Trump aliagiza idara ya
ulinzi nchini humo kupanga mauaji ya rais huyo wa Syria kufuatia shambulio la
kemikali dhidi ya raia mnamo mwezi Aprili 2017 ambalo lililaumiwa kutekelezwa
na serikali ya Syria.
''Twendeni. Tuwaue," Trump aliripotiwa akimwambia Mattis.
Trump alivyosema
kuhusu Assad: Tumuue.
Kitabu hicho kinasema kuwa bwana Mattis alitambua ombi la
Trump lakini baadaye akamwambia msaidizi wake kwamba hawezi kutekeleza hilo.
Lakini akizungumza na waandishi siku ya Jumatano, rais huyo
alisema : Hilo alikutajwa katika mazungumzo yoyote. Aliendelea kutaja kitabu
hicho kuwa 'uongo'.
Ni nini kingine alichosema rais Trump?
Trump alituma misururu ya ujumbe wa twitter siku ya Jumanne
jioni akishikilia maoni yake pamoja na taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya
whitehouse Sarah Huckabee Sanders.
Trump anasema kuwa nukuu zinazodaiwa kutolewa na Mattis na Kelly
ni za udanganyifu na hatua ya kuwalaghai raia.
Anasema kuwa kitabu hicho kilimshusha hadhi yake kwa uongo
mwingi na vyanzo vya uongo, akikana madai kwamba alitumia maneno ya 'mtu punguani'
na 'mjinga' ili kumuelezea mwanasheria mkuu Jeff Sessions.
Taarifa kutoka kwa Mattis zimeelezea kitabu hicho kuwa 'kitu
cha mtu aliyejaa ubunifu mwingi'.
Taarifa hiyo kutoka kwa Kelly inasema: Wazo la kumwita Trump
'mjinga' sio la kweli.... ''kila siku anajua msimamo wangu na yeye pamoja nami
anajua kwamba habari hii ni upuzi mtupu''.
Nini kingine kilichopo ndani ya kitabu hicho?
Woodward anasema kuwa mshauri wa kiuchumi Gary Cohn na
katibu wa ikulku ya whitehouse Rob Porter alitoa stakhabadhi kutoka kwa rais
ili rais Trump asizitie sahihi.
Stakhabadhi hizo zingemruhusu rais kuondoka kutoka katika
biashara huru na mataifa ya Marekani kaskazini pamoja na mkataba wa kibiashara
na Korea Kusini.
''Hii ni sawa na mapinduzi ya kiutawala," alisema
Wooward.
Comments
Post a Comment