- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAMIA YA WANANCHI WA MUSOMA MKOANI MARA BAADA YA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI HUMO
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa Musoma waliokusanyika
katika viwanja vya Mukendo vilivyopo Musoma mjini kwa ajili ya kumsikiliza mara
baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiangalia dawati ambalo alikuwa akilitumia kujisomea Baba
wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi
Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma
shule hapo elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo
uliofanyika Musoma mjini katika viwanja vya Mukendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Stephanie Mouen wakanza kulia mwenye wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Musoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa
wakisikiliza maelezo ya mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika
manispaa ya Musoma mjini Mkoani Mara kabla ya kuuzindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimshukuru Stephanie Mouen mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
la Ufaransa AFD Agence Francaise De Development waliosaidia katika mradi huo wa
maji Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa
barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Isaack Kamwelwe mara baada ya kufungua barabara ya kutoka Mpakani mwa
Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Musoma mjini (hawaonekani pichani)
katika viwanja vya Mukendo Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akitoka katika bweni alilokuwa akilala Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati
Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu
ya Msingi kuanzia tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936…PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment