- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MBALIMBALI IKIWE MO UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA KATIKA ZIWA VICTORIA MKOANI MWANZA
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini
Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo,
ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati
ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni
tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd
na KTMI Co Ltd.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika
Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba
mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati
wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya
Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni
tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd
na KTMI Co ltd.
Mfano wa Meli mpya
itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa
Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo
tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka
mkoa wa Kagera.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa
Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge
mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment