Featured Post

RAIA WA UGANDA NDIO 'WANAOFANYA MAZOEZI ZAIDI DUNIANI'



ZURICH, USWISI
SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mabaya, kutokana na sababu ya kutotaka kujishughulisha na afya zao.

Ripoti ya WHO inakadiria kwamba zaidi ya robo moja ya watu duniani- biliioni 1.4 - hawafanyi mazoezi ya kutosha, takwimu ambayo haijaimarika tangu 2001.
Ukosefu wa mazoezi kunaongeza hatari ya kuugua matatizo ya afya, kama matatizo ya moyo, kisukari na pia baadhi ya saratni.
Na imegunduliwa kwamba kati ya kundi hilo, wanawake ndio wasiojishughulisha na mazoezi isipokuwa katika bara la Asia.
Inaarifiwa huenda inatokana na masuali tofuati, ikiwemo majukumu ya kuwalea watoto, na mila na tamaduni katika baadhi ya jamii zilizofanya kuwa vigumu kwao kufanya mazoezi.
Faida kwa wanaoishi katika nchi kama Uganda:
Utafiti huo umebaini hata hivyo kwamba kwa watu wanaoishi katika mataifa yenye kipato cha chini wana faida au ahueni.
Wengi katika nchi kama Uganda au Msumbiji kwa kawaida hulazimika kujishughulisha wakiwa kazini, wanapotembea kwenda kazini au hata kuabiri magari ya uchukuzi wa umma ambayo kwa kiasi fulani kunahesabika kama kufanya mazoezi.
Wataalamu wanasema tofauti katika mataifa yalio tajiri ambapo watu wengi hutafuta kazi zisizo na shughuli nyingi za mwili, mfano kukaa tu ofisini, pamojana kuongezeka kwa matumizi ya usaifiiri wa magari binfasi, huenda inaeleza viwango vikubwa vya ukosefu wa mazoezi miongoni mwao.
Nchi zenye kiwango kikubwa cha watu wasiofanya mazoezi: Kuwait (67%), Samoa ya Amerika (53%), Saudi Arabia (53%), na Iraq (52%).
Nchi zenye kiwango kidogo cha watu wasiofanya mazoezi ni Uganda na Msumbiji ambayo ni asilimia 6.

'Wasiwasi mkubwa'
Utafiti uliofanywa na WHO na kuchapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet Global Health, ambalo lilichambua data iliyotolewa na washiriki milioni mbili umebaini kuwa kuna jitihada kidogo imefanyika kati ya 2001 na 2016.
Shirika hilo limeendelea kutanabahisha kuwa asilimia arobaini ya raia wanaosihi katika mataifa yalioendelea, mfano Uingereza na hata Marekani hawajishughulishi na afya zao na kwamba hali hii ni mbaya zaidi katika nchi ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia na Iraq.

Muongozo wa mazoezi kwa walio na umri wa kati ya 19 - 64

Kiasi gani? 
Angalau dakika 150 wa mazoezi ya wastani ya kunyoosha viungo, au dakika 75 za mazoezi mazito ya aerobic kila wiki; Mazoezi ya kutunisha misuli yote mwilini kwa angalau siku mbili au zaidi kwa wiki; Usikae mahali pamoja kwa muda mrefu jaribu kuinuka na kujinyoosha mwili au kutembea tembea.

Je mazoezi ya wastani ya aerobic ni gani? 
Kutembea haraka; Kuendesha baiskeli katika eneo lenye vilima vidogo au ardhi iliyo sawa tu; Kucheza tenisi; Kukata nyasi kwa kutumia mashine; Kupanda milima; Kuteleza kwa viatu vya magurudumu; Kucheza voliboli; na Kucheza mpira wa kikapu.

Je mazoezi ya uzito ni yepi? Kukimbia, Kuogelea haraka, Kuendesha baiskeli kwa kasi, Kucheza tenisi, Soka, Raga, Kuruka kamba, na Kucheza mpira wa magongo.

Ni mazoezi gani yanayoimarisha misuli? Kunyayua vyuma, kufanya mazoezi kwa kutumia uzito wa mwili wako, kama kukata mafuta ya tumbo 'push-ups' au 'sit-ups', Ukulima, kama kulima na kupiga chepe, na yoga.
Wataalamu wametoa wito kwa serikali kutoa na kuimarisha miundo mbinu inayohimiza michezo na kushinikiza kutembea au kuendesha baiskeli kama mbinu za usafiri.
Waandishi wa ripoti wameonya kwamba kwa hali ilivyo, huenda azimio la WHO kupunguza viwango vya watu kutofanya mazoezi kufikia 2025 kwa 10% lisifikiwe.


Comments