- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NEW YORK, MAREKANI
RAIS Donald Trump wa Marekani amelihimiza jarida la New York
Times kumfichua afisa mkuu wa serikali yake, aliyeandika makala ya gazeti hilo,
akidai baadhi ya wafanyikazi serikalini walikuwa wakifanya kila wawezalo, ili
kutatiza ajenda yake ya maendeleo.
Trump amemtaja mwandishi wa makala hiyo, ambaye jina lake
limefichwa, kama mchochezi, na kuashiria kuwa uchapishaji wenyewe wa makala
hiyo ni kosa la jinai.
Mwandishi huyo asiyetajwa amesifu ufanisi kidogo wa utawala
wake, lakini akasema baadhi ya maamuzi ya Trump yamekuwa yasiyofikiriwa na ya
kipuuzi.
Msemaji wa jarida la New York Times amesema gazeti hilo
linajivunia kuwa lilichapisha makala hayo, ambayo amesema yamesaidia raia
kuelewa kile kinachoendelea katika uongozi wa Rais Trump.
Tayari kumekuw na shinikizohuko White House za kumtafuta na
kumtambua afisa aliyetoa taarifa hizo.
Rais alisema makala hiyo ni hujuma na afisa wa mawasiliano
wa White House Sarah Huckabee Sanders alituma jibu lenye maneno makali.
"Mtu ambaye aliandika makala haya amechagua kumhujumu
badala ya kumuunga rais wa Marekani aliyechaguliwa," aliandika. Haweki
mbele nchi bali maslahi yake ndiyo ameyaweka mbela badala ya watu wa Marekani.
Bi Sanders na Trump wote wamelikosa jarida la The New York Times
kwa kuchapisha makaa hiyo, huku Trump akisema kuwa makampnui yote ya haabri
yatakosa biashara mara atakapoondoka ofisini kwa kuwa hayatakuwa na kitu cha
kuandika.
Hueda kukawa na wito wa kutaka afisa huyo kujifichua.
Comments
Post a Comment