- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
BRASILIA, BRAZIL
MGOMBEA anayeongoza anaeminika anaweza kushinda uchaguzi
nchini Brazili Jair Bolsonaro, amechomwa kisu wakati wa kampeni zake, mgombea
huyo wa mrengo wa kulia alichomwa kisu katika mkutano mkubwa wenye mkusanyiko
wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki.
Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake juu ya
ubaguzi wa rangi, amepata kura nyingi katika kura za maoni za hivi karibuni.
Kura hizo za maoni zinaonesha kuwa anatafanya vizuri katika
uchaguzi wa urais mwezi ujao na kumpita Mgombea na Rais wa zamani Lula da
Silva.
Tukio hilo lilitokea vipi?
Picha za video zimemuonesha bwana Bolsonaro akinyoosha mkono
kwa wafuasi wake na hapo ndipo alipochomwa na kitu ambacho baadae iligundulika
na kisu.
Baada ya hapo aliinama kwa maumivu na haraka wafuasi wake
walimshusha chini na kumuingiza ndani ya Gari kisha kupelekwa Hospitali.
Baada ya shambulio hilo, mtoto wake aliandika katika mtandao
wa Twitter kuhusu taarifa hiyo lakini baadae masaa mawili mbele alitoa maelezo
kwa kina.
''Kwa bahati mbaya amekua na hali mbaya kuliko tulivyodhani,
amepoteza damu nyingi amefika hospitali na damu 10/3 karibu afariki, lakini
sasa anaendelea vizuri tafadhali tumuombee,'' aliandika katika mtandao wa
Twitter.
Wauguzi wa hospitali baadae walisema kuwa bwana Bolsonaro
amepata jeraha kubwa na limechimba sana kwenye utumbo lakini sasa anaendelea
vizuri.
Alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa
masaa baada ya upasuaji, lakini atasalia hospitali hadi siku kumi.
Polisi wanasema kuwa wamekamata mshukiwa wa tukio hilo
anaitwa Adelio Obispo de Oliveira.
Watu mbalimbali wamekosoa vikali mshukiwa huyo kwa kitendo
alichokifanya.
CHANZO: BBC
Comments
Post a Comment