- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI WETU
MAENEO ya mijini yameshatoka kwenye mahitaji ya
mawasiliano ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine na hali hiyo imezifanya shughuli
za mawasiliano kutoa mchango mkubwa kwenye shughuli za uchumi na maendeleo.
Lakini maeneo ya vijijini yamebakia nyuma licha
ya kwamba yapo mawasiliano mazuri ya simu na kufikiwa kwa teknolojia za kisasa
za mawasiliano ya elektroniki kunaweza kuwa ni fursa ya kufikia hatua ya
maendeleo kama ilivyo mjini.
Fikiria kuwa kuna mtandao mkubwa wa barabara
duniani ambazo zinaruhusu magari kuwa kwenye mwendo wa kasi kwa usalama yakiwa
yamebeba mizigo na kuifikisha kwenye maeneo husika bila kukwama.
Hali hiyo inafanya biashara kuendelea kwani
malighafi zinazoagizwa zinawasili kwa haraka, kwa wakati, uzalishaji na huduma
za viwandani zinaenda kwa ufanisi.
Aidha bidhaa zinazozalishwa pamoja na bidhaa
nyingine zinawekwa kwenye orodha ya ushindani wa bei na kufikishwa kwa walaji
sehemu mbalimbali duniani.
Kila mtu iwe mkulima anayeishi mwishoni mwa
barabara au meneja mauzo wa kampuni kubwa ya biashara ambaye yuko karibu
na uwanja wa ndege anaweza kuunganishwa kwenye mtandao huo.
Hata hivyo hili linaonekana kuwa wazi
kinadharia lakini kiutendaji kuna alama za kuchepukia kwenye barabara
hiyo hususani miongoni mwa nchi zinazoendelea.
Kama alama hizo za kuchepukia
zikiondolewa kutakuwa na athari gani kwenye maendeleo vijijini?
'Mtandao wa barabara' unaozungumziwa hapa
ni mtandao wa intaneti na magari yanayosafiri kwa kasi ni mafurushi
ya takwimu za habari.
Faida kubwa ya intaneti dhidi ya njia
nyingine za mawasiliano ni kwamba watu wanaweza 'kuzungumza' na
mwingine bila kujali yeye ni nani na yuko umbali kiasi gani.
Mawasiliano hayo ni rahisi, ya haraka na ya njia
mbili tofauti na redio, televisheni au machapisho mengine na
wingi na habari tofauti ambazo zinaweza kuhamishwa mara moja zinapeperushwa.
Wakati mtu anapozungumza kwa kutumia simu,
sehemu moja ya mfumo wa simu huwa unajielekeza kwenye kuita, ikimaanisha kuwa
pindi watu wengi wanapotaka kutumia mfumo wa simu kwa wakati huo
mmoja uwezo wake unakuwa hautoshi na huwa hakuna njia inayokuwa wazi.
Pindi watu wawili wanapotumia njia moja kwa
mawasiliano ya intaneti mawasiliano hayo hufungwa kwenye vifurushi vidogo
vya takwimu ambavyo hutiririka kama mkondo wa magari kwenye mtandao.
Vifurushi hivi vya takwimu ambavyo
huwa vimejichanganya na takwimu za watu wengine husafirishwa hadi
kwenye njia panda na hata hivyo mawasiliano yanaweza kumegwa kwenye
vifurushi tofauti vya takwimu kila kimoja kikifuata njia yake na mpokeaji
hupokea ujumbe uliokamilika.
Kwa kuwa mtumaji na mpokeaji wanakuwa na
kompyuta, modemu, na vifaa sahihi, njia ya simu na uelewa wa namna ya
kutumia kifaa, wanaweza kubadilishana habari.
Hata hivyo watumiaji pia wanahitaji kufahamu
namna ya kutumia vizuri yale yote yanayotolewa kupitia intaneti.
Wakulima wanaweza kupata habari kuhusu bei za
mazao yao wanayouza nje kuwa ni ya juu kuliko kuuza mazao hayo kwenye soko la
mji jirani.
Wanaweza kutaka kufahamu ni njia gani ya
usafiri itakayotumika kusafirisha mazao hayo na itagharimu
kiasi gani cha fedha na iwapo mtiririko huo utakuwa na faida.
Kwenye biashara nyingi jinsi kiwango cha
kuhabarishwa kinavyokuwa kikubwa ndivyo muuzaji anavyokuwa na fursa nzuri
ya kupata bei nzuri.
Mkulima wa matunda anaweza kutaka ushauri
wa kiufundi ili aweze kuamua ni kipindi gani cha kuvuna mazao yake.
Watafiti wa kilimo wanaweza kuhitaji
habari inayohusiana na kazi zao na ambayo wanajua itapatikana tu kwenye vyuo
vikuu sehemu nyingine duniani.
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotaka kurudi vyuoni
kuendelea na shahada ya juu kwenye vyuo vya ng'ambo wanaweza kuwa na
mawasiliano na wakufunzi au wasimamizi wao ili waweze kumalizia kazi zao za
utafiti au maprofesa wa vyuo hivyo vikuu wanaweza kuhitaji kujifunza
kutoka kwa waliokuwa wanafunzi wao.
Intaneti pia inatoa fursa za mafunzo ya
elimu-masafa kupitia sifa rasmi ambazo zinaweza
kutumika kujisomea nyumbani kwa kutumia mafunzo kwa njia ya
intaneti.
Rambaza au zama
Intaneti ni lazima ichukuliwe kama
miundombinu ya mawasiliano na kwa kuitumia kwa njia mbalimbali huduma
kadhaa zinaweza kupatikana kama vile mtandao mpana duniani (www),
barua-elektroniki na habari.
Mtandao mpana ni huduma kuu ya kutumia katika
kujitafutia habari binafsi. Barua- elektroniki (barua pepe) inatumika
kuwasiliana na mtoa habari moja kwa moja, kuliko ilivyo kwa simu au faksi
ambazo hutumwa kwa mtu binafsi au shirika.
Kupatikana kwa habari kwa namna moja ni
kama ubao wa matangazo ambapo mtu yeyote, mahali popote
anaweza kuangalia na ambapo mtu yeyote anaweza kubandika tangazo
lake. Ni njia ya kuuliza na kujibu maswali kutoka kwa watu
wanaotaka kuelewa kuhusu jambo husika.
Watu wengi wanaweza kufaidika na huduma hii kama
mashirika ambayo yanafikia mtandao wa intaneti yanatawanya habari kwa
wale ambao hawana namna ya kufikia habari hizo kwa kuchapishwa au
kupitia redio.
Thamani ya habari inategemea na mwenendo wake na
hivyo thamani ya swali ambalo inatarajiwa kujibu. Kama swali limejibiwa
kwa usahihi hatua hiyo kidogo inaonekana kama ya kimashine jambo ambalo
linaifanya kompyuta kuwa ni njia nzuri katika kazi hiyo.
Kama unatuma maswali kwenye makundi ya majadiliano
kwenye mtandao kwa mfano unaweza kupata jibu zuri na sahihi. Kuuliza swali
sahihi kunahitaji stadi zaidi, uelewa na ueledi kuliko kutuma maswali tu.
Kwa mfano katibu wa chama cha wakulima anaweza
kuulizwa na wanachama wake kuperuzi kuhusu matumizi ya mbolea ya chumvi
chumvi kwa kipindi cha msimu wa mazao ya mahindi.
Jibu linaloweza kutolewa ni kilo 50 za Naitrate
kwa hekta, Oksaidi ya fosiforasi kilo tano kwa hekta, Potasiamu kilo 50 kwa
hekta; ambapo habari inayotakiwa ni 'kila baada ya wiki
tatu'.
Kompyuta ni nzuri katika kutoa majibu lakini ni
mbaya katika maswali ya kubuni. Katika kutafuta jibu kwenye mtandao mpana
(www) kwa mfano utatoa majibu mengi na njia mbadala ya kupata majibu
shughuli ambayo inaweza kuwa ya kuchosha na hivyo kuachana nayo.
Kuwepo kwa njia ya simu ambayo kwa vyovyote ni
muhimu katika kupata intaneti ni vyema kwa katibu huyo kupiga simu
kwa duka la pembejeo lililopo karibu na kuulizia ni lini mbolea
itapatikana na gharama yake itakuwa ni kiasi gani.
Kama ilivyo kwa njia nyingine za mawasiliano ni
muhimu kufahamu namna ya kufafanua ni habari ipi unayoihitaji na namna
gani ya kuwasiliana au kuwasilisha matakwa yako.
Comments
Post a Comment