Featured Post

HATUA TANO ZINAZOFUATWA NA JUMIA FOOD KUWAFIKISHIA WATEJA CHAKULA

Na Jumia Food Tanzania
Endapo wewe ni mkazi wa Dar es Salaam kuna uwezekano mkubwa utakuwa umekutana au
kuwaona madereva wa pikipiki wakiwa wamevalia fulana na mabegi makubwa mgongoni yenye
rangi ya machungwa yakiwa na nembo ya Jumia Food.
Bila ya shaka utakuwa umejiuliza maswali mengi kuwa hawa madereva wanafanya shughuli gani
kuzunguka na mabegi makubwa mgongoni? Kama ulikuwa haufahamu, hao ni wafanyakazi
wa Jumia Food, kampuni inayotoa huduma ya chakula kutoka migahawa mbalimbali
kwa njia ya mtandaoni. Mteja anaweza kuagiza chakula kutoka kwenye mgahawa wake pendwa
mahali popote alipo na kupelekewa mpaka alipo ndani ya muda mfupi.

Nina uhakika utakuwa na maswali mengi juu ya namna wanavyofanya shughuli zao za
kufikisha chakula kwa wateja mpaka walipo. Kwa sehemu kubwa huduma ya chakula kutoka
kampuni hii hutegemea madereva wake wa pikipiki ambao ndio kiungo kikubwa
baina ya migahawa na wateja. Hivyo basi, katika makala haya tungependa kukufahamisha
juu ya hatua tano ambazo hufuatwa na kuzingatiwa na madereva hawa mpaka
wanakalimisha huduma ya kufikisha chakula.

1. Kukubali oda kutoka kwa timu ya Huduma kwa Wateja. Hii ni hatua ya kwanza kabisa
ambayo dereva wa Jumia Food anatakiwa kuifuata mara baada ya timu ya huduma kwa
wateja ya Jumia Food kuwasiliana naye. Hatua hii ya awali ni muhimu sana kwa
sababu ndiyo inayoonyesha taarifa zote zikiwemo: chakula kilichoagizwa na mteja, mgahawa
chakula kilipoagizwa pamoja na taarifa za mteja kama vile jina lake, anuani ya
mahali alipo na mawasiliano yake. Kwa kufanya hivi inaonyesha kuwa tayari huduma
imeshapokelewa na mteja atarajie kupata chakula alichokiagiza. Madereva hufanya hivi
kupitia simu zao za mkononi ambapo kuna mfumo maalumu unaowawezesha kufanya hivi.
Mfumo huu husaidia kampuni na mteja kujua mwenendo mzima wa oda ya chakula ipo
kwenye hatua gani.
 
2. Kuonyesha kuwa dereva amefika mgahawani. Hatua ya pili baada ya dereva kukubali
oda ni kuonyesha tayari amekwishafika mgahawani kwa ajili ya kuchukua chakula kilichoagizwa
na mteja. Dereva anapofika mgahawani hujitambulisha kwa anayehusika na
kupokea oda na kisha chakula huandaliwa ili kupelekwa kwa mteja. Kwa upande wa kampuni
na mteja wote wanaweza kujua hatua hii pia. Mara nyingi maandalizi ya chakula
huchukua muda usiozidi dakika 30.
3.Kuonyesha tayari chakula kimechukuliwa mgahawani. Baada ya chakula kuandaliwa
na kukamilika, dereva huonyesha kwenye mfumo tayari amekwishakichukua na yupo njiani
kuelekea kwa mteja. Hatua hii humjulisha mteja kuwa chakula chake kipo njiani,
hii humsaidia kama alikuwa anafanya shughuli zingine au mahali alipo kujiandaa kukipokea
ndani ya muda mfupi.  

4. Kuonyesha kuwa dereva amefika kwa mteja. Dereva anapofika mahali alipo mteja
aliyeagiza chakula huonyesha kwenye mfumo wake ili kumjulisha mteja aje kupokea huduma yake.
Kwa kuongezea, dereva hupiga simu kwa mteja endapo hakuwa anafuatilia
hatua zote kupitia simu yake ya mkononi. Kama ulikuwa haufahamu unaweza kupakua
App ya Jumia Food kupitia simu yako ya Android au iPhone ambayo imeboreshwa
zaidi na kukuwezesha kuweka oda ya chakula na kufuatilia hatua zote. Hii hukurasishia wewe
mteja kujua chakula chako kiko wapi na muda ambao kitafika mahali ulipo.    

5. Kukamilisha huduma. Hatua ya tano na ya mwisho kabisa ni kumkabidhi mteja chakula
alichoagiza na kisha kupokea malipo kutoka kwake. Kumbuka, malipo ya huduma za Jumia
Food hufanyika pale mteja anapopokea na kuridhika na chakula alichokiagiza.
Baada ya kukamilisha hatua hii, dereva huonyesha kwenye mfumo ili kutumiwa oda za
wateja wengine ili kuwahudumia.  

Ni rahisi kupata huduma za Jumia Food kutoka kwenye migahawa uipendayo hapa jijini
Dar es Salaam ndani ya muda mfupi mahali popote ulipo. Ni huduma yenye uwazi kwani
hatua zote kuanzia oda ya chakula ipopokelewa mpaka mteja anafikishiwa chakula
zinaonekana! Ni rahisi, ya kuaminika na inaokoa muda na usumbufu wa kutoka sehemu
moja mpaka nyingine kufuata chakula. Unaweza kupata huduma zao kupitia tovuti yao
au kwenye App ya simu ya mkononi na kisha kuperuzi orodha ya migahawa yenye vyakula
uvipendavyo karibu yako.  

Comments