- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA LULU A. SANGA, BBC SWAHILI
NINAPOTAJA masoko makubwa ya nguo za ndani za mitumba, hapa
nazungumzia Mwenge, Ilala, Tandika na hata Manzese.
Wanawake ndio watumiaji wa kubwa kwani kwa upande wa wanaume
nguo zao kubwa za ndani ni kaoshi, soksi na taiti.
Lakini kwa upande wa wanaweke hupendelea zaidi kutumia
sidiria, nguo za kulalia, taiti na hata chupi.
Nguo hizi za ndani za mtumba, hupendwa zaidi kwasababu
baadhi husema ni imara na zina dumu lakini pia hupatikana kwa bei raisi sana,
zingine huuzwa miatano au elfu moja na zipo za mpaka elfu kumi na zote ni za
mtumba.
Pamoja na urahisi huo, watumiaji wanafahamu nini juu ya
madhara ya kuvaa nguo hizi za ndani zilizo valiwa na watu wengine ambao
hatuwajui? Hatujui afya zao na wala magonjwa ambayo huenda wanayo.
BBC imezungumza na baadhi ya watumiaji wa nguo hizo za ndani
baadhi wanaonyesha kuto jua lolote kama yanaweza kuwepo madhara.
"Mi hayo madhara hata siyajui ila napata zangu nguo kwa
bei poa na napendeza kama kawaida. Kama kuna madhara haya," anasema bi
Aisha wa soko la karume.
Hata hivyo Ally Saleh mtumiaji wa nguo za ndani za mitumba
anasema yeye huangalia zilizo mpya mpya.
"Mimi huwa nachukua ule mtumba wa grade A na zangu
zinakuwa mpya mpya hazijatumika sana, ila kuhusu madhala labda zile zilizo
chakaa kupita kiasi. Mie singlendi zangu ata boksa napata kali mtumbani,"
Ally anaiambia BBC.
Wengine wanafurahia ubora hali inayopelekea kufumbia macho
juu ya elimu waliyo nayo.
"Mie naambiwa tu kwamba zina madhara lakini ukiziona
zinaonekana bora na nzuri kuliko za dukani yaani ukivaa sidiria ya dukani
inafanya matiti yanakuwa mama ni bebe, wakati ya mtumba kwa raha zangu kitu
talk to me inakamata muruaa," Nola Almasi anaiambia BBC.
Hata hivyo kumekuwa na maoni mbali mbali juu ya madhara ya
nguo za ndani za mitumba wengine husema zinaleta saratani, fangasi na baadhi
huamini zinaharibu kizazi. Pamoja na yote yasemwayo baadhi yetu hufumbia macho
na huamini kuwa ni propaganda za ushindani wa kibiashara.
Hata hivyo katika nguo hizo za ndani za mitumba zipo nyingi
ambazo hazijatengenezwa kwa mali ghafi ya pamba, zimetengenezwa kwa polyista
malighafi ambayo hainyonyi maji. Hali inayopelekea baadhi kupatwa na muwasho
sehemu za siri.
Daktari Fredrick Mashili wa hospitali ya taifa Muhimbili ili
kufahamu zaidi juu ya ukweli wa madhara ya nguo za ndani za mitumba.
"Kunakuwa na uwezekano wa kuwepo madhara kiafya na mara
nyingi ni matatizo ya ngozi zaidi ndo yanaweza kusababishwa na hizo nguo,
kutokana na ukweli kwamba huenda aliyekuwa anazitumia hizo nguo anatatizo flani
la ngozi.
Kwa mfano ukiongelea vitu kama fangasi ambavyo vinauwezo wa
kukaa kwenye mazingira magumu na kuishi kwa muda mrefu sana, kwa maana hiyo
hata kama zilikuwa zimesafirishwa kwa muda fulanikwenye hali ya ukavu na nini
bado kunakuwa na uwezekano wa kuwepo kwa vimelea au vitu fulani ambavyo ni
sehemu ya fangasi ambavyo baadae mtu mwingine akivaa anauwezo wa kupata hilo
tatizo," Daktari Mashili anaiambia BBC.
Hata hivyo, daktari huyo anasisitiza kuwa upo uwezekano wa
kuwepo kwa magojwa mengine ya ngozi ambayo haya sababishwi na fangasi na hii
inategemea ni muda gani tangu nguo hizo zimetoka kwa mtumiaji wa awali na
kuanza kutumiwa na mtumiaji wa sasa.
Daktari Mashili amesisitiza kuwa, kama kuna ulazima wa
kuzitumia nguo za ndani za mitumba ni vyema mtu akazisafisha na dawa zile kali
ambazo zinaweza kusaidia kuuwa viji dudu kuliko kufua tu kawaida na kisha
kuivaa.
Tangu mwaka 2009, Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
lilipiga marufuku uuzaji wa nguo za ndani za mitumba na kutoa kipindi cha ukomo
kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo. Baada ya kipindi cha mpito kuisha, TBS
walifanya maamuzi ya kukamata na kuchoma nguo hizo za ndani za mitumba ili
kutekeleza agizo la sheria ya mwaka 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani
zilizokwishatumika.
Hata hivyo harakati hizo hazikufua dafu kwani mpaka sasa
nguo za mitumba bado zipo katika takribani kila soko la nguo za mitumba
Tanzania.
Comments
Post a Comment