- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS wa China, Xi Jinpingamesema China itatoa jumla ya dola
bilioni 60 za Marekani kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na
Afrika katika shughuli za maendeleo.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 03 ,2018)
wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika
(FOCAC) unaofanyika jijini Beijing nchini China.
Rais Jinping ameahidi kuwa nchi yake itatoa ushirikiano ili
kuhakikisha kwamba amani ya kudumu inapatikana Barani Afrika, hatua
ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.
Maeneo mengine ambayo Rais huyo ameahidi kuwa China italisaidia
Bara la Afrika ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya
biashara na huduma za afya.
Kadhalika, Rais Jinping amesema China itatoa nafasi za mafunzo ya
kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaam kutoka nchi za Afrika
ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi.
Amesema hivi sasa anaamini kwamba China na nchi za Bara la Afrika
wako karibu zaidi na wanashirikiana vizuri sana katika shughuli za kimaendeleo
ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Mkutano huo ulianza kwa sherehe ya ukaribisho na baadae
viongozi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Antyonio Geterres walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na
mwenyeji wao Rais wa China.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais Dkt. John
Magufuli katika mkutano huo alisalimiana na Rais Jinping baada ya
ufunguzi. Mkutano huo utaendelea kesho ambapo viongozi wengi kutoka Bara
la Afrika watapata nafasi ya kuzungumza.
Comments
Post a Comment