Featured Post

BONDIA MTANZANIA HASSAN MWAKINYO AMTANDIKA MWINGEREZA


 BONDIA Hassan Mwakinyo wa Tanzania, jana alimtwanga kwa Technical Knockout (TKO), sekunde ya 45, raundi ya pili Muingereza, Sam Eggington.
Pambano hilo la aina yake lilifanyika katika Uwanja wa Arena Birmingham, zamani Barclaycard Arena, Mjini  Birmingham, England.
Katika pambano hilo lisilo la ubingwa uzito wa Light Middle, Mwakinyo alimzidi mpinzani wake tangu mwanzo kabla ya kummaliza katika raundi ya nne kabla ya pambano kuu kati ya Muingereza, Amir Khan na Samuel Vargas wa Colombia anayeishi Canada.
Khan aliyeshinda kwa pointi za majaji wote, alimuangusha Vargas mwanzoni mwa raundi ya pili, naye akaangushwa mwishoni mwa raundi hiyo lakini wote waliinuka haraka, kuendelea hadi kumaliza raundi.
Khan aliyemuangusha Vargas raundi ya tatu, kumjeruhi pua kwa ushindi huo, anaweza kupigana na Manny Pacquiao au Kell Brook.
Mwakinyo baaada ya ushindi huo wa jana, atapanda tena ulingoni Oktoba 20, mwaka huu, kuzipiga na mwenyeji Wanik Awdijan, Ukumbi wa Alex Sportcentrum, Mjini  Nuremberg, Ujerumani katika pambano la kuwania taji la vijana la IBF uzito wa Middle.
Pambano la juzi lilikuwa la tatu kwa Mwakinyo kupigana nje ya Tanzania akiwashinda kwa mara ya pili baada ya kumshinda pia kwa TKO Anthony Jarmann wa Namibia Agosti 8, 2017, katika Ukumbi wa Grand Palm Hotel, Mjini Gaborone, nchini Botswana. 
Desemba 2, 2017 Mwakinyo alipoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji, Lendrush Akopian, Ukumbi wa Krylia Sovetov Mjini Moscow, Urusi.

Comments