Featured Post

WACHEZAJI 7 MAARUFU WALIOTARAJIWA KUJIUNGA NA KLABU MPYA JANA USIKU


 
LONDON, ENGLAND
DIRISHA la uhamisho la klabu za Uingereza linafungwa leo Ijumaa lakini BBC michezo inaangazia makubaiano ambayo huenda yakakamilishwa barani Ulaya.

Timu zilizopo nje ya Uingereza zinaweza kufanya makubaliano ya uhamisho hadi saa moja usiku saa za Afrika mashariki , huku madirisha ya uhamisho ya Uhispania, Ujerumani na Ufaransa pia yakifungwa siku ya leo.
BBC Michezo inaangazia baadhi ya wachezaji wa Ulaya ambao huenda wakamia klabu mpya.

Ivan Rakitic (Barcelona)

Kiungo huyu mwenye miaka 30 alikuwa anahusishwa na klabu ya Paris St-Germain.
Kuwasili kwa Arturo Vidal na Arthur kunatoa ushindani mkubwa kwa Ivan rakitric katika safu ya kati ya klabu ya Barcelona.
Huku hatma ya mchezaji wa Ufaransa Adrien Rabiot ikiwa haijulikani katika klabu ya Paris St-Germain, klabu hiyo ya Ligue 1 inamnyatia kiungo huyo wa kati wa Croatia na wanataka kuimarisha kitita cha uhamisho wake cha Pauni milioni 112.

Jerome Boateng (Bayern Munich)
Ni mlinzi mwenye umri wa miaka 29, ambaye pia anahusishwa na klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa.
Uwezekano wa beki huyo wa Ujerumani Boateng kusalia na mabingwa hao wa Bundesliga uko nusu nusu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City alihusishwa na uhamisho wa Manchester United msimu huu, lakini klabi hiyo ya ligi ya dara la kwanza huenda ndiko anakoelekea.

Shinji Kagawa (Borussia Dortmund)
Ni kiungo Mjapani mwenye umri wa miaka 29 ambaye anahusishwa na klabu za Sevilla ya Hispania na Olympique Marseille ya Ufaransa.
Kiungo wa kati wa zamani katika klabu ya Manchester United, Kagawa hakushiriki katika mechi ya ufunguzi wa klabu ya Dortmund dhidi ya RB Leipzig na ameripotiwa kutokuwa miongoni mwa mipango ya meneja mpya Lucien Favre.
Huku mchezaji mpya aliyesajiliwa Axel Witsel na Thomas Delaney wakitarajiwa, mchezaji huyo wa Japan alitarajiwa kuondoka katika Uwanja wa Westfalenstadion katika siku ya mwisho ya uhamisho.

Claudio Marchisio (Huru)
Ni kiungo Mtaliano mwenye umri wa miaka 32 ambaye anahusishwa na klabu za Porto na Benfica ya Ureno.
Kandarasi ya kiungo wa kati wa Italia, Marchisio katika klabu ya Juventus ilikatizwa kutokana na makubaliano kati ya pande zote mbili na sasa anatafuta klabu mpya.
Porto na Benfica wamehusishwa ijapokuwa klabu nchini Ureno zina hadi tarehe 21 Septemba kufanikisha makubaliano yao.

Lazar Markovic (Liverpool)
Kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 24 ambaye anahusishwa na PAOK ya Ugiriki na Anderlecht ya Ubelgiji.
Ni kweli kwamba bado ni mchezaji wa Liverpool. Raia huyo wa Serbia alijiunga na Liverpool kwa dau la Pauni milioni 20 kutoka benfica 2014, lakini hajaichezea klabu hiyo tangu 2015.

Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)
Kiungo wa kati  mwenye umri wa miaka 22 ambaye anahusishwa na klabu ya Monaco ya Ufaransa na Schalke 04 ya Ujerumani.
Loftus-Cheek alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace, ambapo mchezo wake ulimfanya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza cha Kombe la Dunia kilichokuwa Urusi mwaka huu.
Huku Jorginho, N'Golo Kante, Ross Barkley na Mateo Kovacic wakiwa mbele yake katika wachezaji wanaotarajiwa kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu katika klabu ya Stamford Bridge, Loftus-Cheek huenda akaanza kutafuta klabu mpya.

Mario Hermoso (Espanyol)
Beki huyo wa Espanyol ya Hispania mwenye umri wa miaka 23 anahusishwa na klabu ya Real Madrid.
Kuna kila uwezekano kwamba Real Madrid huenda ikaanza kumtafuta kiungo wa kati anayetumia mguu wa kushoto iwapo Jesus Vallejo na Hermoso watalengwa.
Hermoso alijiunga na Espanyol kwa dau la Pauni 360,000 msimu uliopita na Real ina fursa ya kumnunua tena mchezaji huyo kwa dau la Pauni milioni 13.5.

Comments