Featured Post

POLISI MZUNGU AFUNGWA MIAKA 15 JELA KWA KUMUUA KIJANA MWEUSI



TEXAS, MAREKANI
Ofisa wa Polisi amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kumpiga risasi na kumuua kijana mweusi huko Texas, Marekani.
Roy Oliver, ambaye ni mzungu alifyatua risasi kwenye gari ambalo lilikuwa litoka katika karamu moja huko Dallas mwezi Aprili 2017 na kumuua Jordan Edwards aliyekuwa na umiri wa maiaka 15.

Ni nadra sana polisi kuhukumiwa kifungo kwa kuua. Mawakili wa Oliver wanasema watakata rufaa.
Familia ya Jordan inasema kifungo hicho ni kifupi sana.
"Atakuwa huru baada ya miaka 15 na hicho si cha kutosha wa sababu Jordan hatapata maisha tena," mama wa kambo wa Charmaine Edwards, alisema.

Kipi kilitokea siku ya mauaji?
Usiku wa tarehe 29 Aprili 2017 polisi waliitikia ripoti za watoto waliokuwa wakinywa pombe kwenye karamu moja huko Balch Springs.
Polisi walikuwa ndani ya nyumba walipojaribu kumpata mwenye nyumba wakati waliposikia kile walichoamini kuwa ni sauti za risasi, hali iliyozua hofu nyumbani na kusababisha watu kukimbia.
Kulingana na nyaraka za polisi, polisi mwingine Tyler Gross alijaribu kusimamisha gari lililokuwa limejaa ambao walikuwa wakiondoka kwenye karamu.
Alitembea kwenda kwenye mlango wa abiria wa gari na kugonga kioo, ambacho kilivunjika.
Kisha Oliver akafyatua risasi mara kadhaa kwenda kwenye gari hilo, akampiga Jordan ambaye alikuwa amekaa mbele ya kiti cha abiria, nyuma ya kichwa.
Oliver alisema aliamini kuwa gari hilo lilikuwa linarudi nyuma kwenda kwa polisi mwenzake.
Hata hivyo, kamera ya polisi huyo ilionyesha kuwa gari hilo lilikuwa likiondoka kwa polisi wakati risasi hizo zilipofyatuliwa.
Oliver alifukuzwa kazi muda mfupi tu baada ya mauaji hayo.

Watu wanahisi vipi kuhusu hukumu hiyo?
Jaji huko Texas alimpata Oliver na hatia siku ya Jumanne na Jumatano akahukumiwa miaka 15 jela.
Hii inamaanisha kuwa anaweza kupewa msamaha baada ya miaka saba unusu.
Waendesha mashtaka walikuwa wanataka ahukumiwe kifungo cha miaka 60.
Familia ya Jordan iliangua kilio na kuwakumbatia waendesha mashtaka baada ya kusomwa hukumu.
Baba yake, Odell Edwaerds alisema alikuwa mwenye furaha sana.
Hata hivyo, mama wake wa kambo alisema alitakiwa kifungo kirefu cha miaka 25 hadi 30.
Wakili wa familia ya Edwards Daryl Washington, alisema hukumu hiyo ni ishara kuwa kila Mwamerika mweusi aliyeuawa na polisi hakupata haki.

Comments