Featured Post

KAGERA UMEFANIKIWA KUJENGA VIWANDA 91 AMBAVYO VIMETOA AJIRA 672


RICHARD MWANGULUBE/BUKOBA
Mkoa wa Kagera umefanikiwa kujenga viwanda 91 katka kipindi cha   mwezi Disemba 2017 na Juni  mwaka 2018 ambapo  kati ya hivyo 38 ni  Viwanda  vidogo   ambapo ka ujumla wake vimefanikiwa  kutengeneza ajira kwa  watu 672.

Ujenzi huo wa viwanda unatokana na mkakati wa ‘Mkoa   huo wa kujenga  viwanda  vipatavyo 100’ kwa mwaka mkakati  ambao kitaifa  uliozinduliwa mjini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo  Oktoba mwaka jana 2018.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera(RAS) Diwani Athumani aliieleza alipozungumza na Gazeti la Tanzanite One  Ofisini kwake mjini Bukoba katika mahojiano maalumu kwamba Viwanda hivyo ni vya kuchakata nafaka na mafuta ya alizeti, viwanda vya matofali,useremala,ushonaji nguo, kukoboa kahawa pamoja na  viwanda vya sabuni.
Diwani Athumani Alisema pamoja na viwanda vidogo vinavyoendelea kujengwa lakini tayari kuna  Viwanda vikubwa vitano  alivyovitaja kuwa ni Kiwanda cha  KADERES Plc kilichopo wilaya ya Karagwe kilichoanza uzalishaji mwezi juni mwaka huu   2018  kinachohusika na  uchakataji wa maharage kwa kuyachambua kuondoa mawe, kusafisha, kuyapanga katika madaraja na kuyafungasha tayari  kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
Athumani alitaja viwanda kingine kuwa cha usindikaji kahawa cha Amir Hamza (T) Ltd ambacho kimejengwa katika wilaya ya Bukoba eneo la Kibuye na  Kiwanda cha maji ya kunywa cha Bunena Dev Co Ltd kilichopo katika Manispaa ya Bukoba.
Viwanda vingine vilivyoko katika hatua ya mwisho ya ujenzi ni  Mayawa kilichoko katika Manispaa ya Bukoba ambacho kitazalisha maji ya matunda,mvinyo na maji ya kunywa,Kiwanda cha usindikaji wa nyanya na pilipili  cha Victoria Edibles Limited  kinacojengwa Bukoba Vijijini na  Kiwanda cha Vinywaji Vikali cha Ambiance (T) Distilleries Limited kinachojengwa katika Manispaa ya Bukoba eneo la Miembeni.
Aidha Athumani alisema  Wawekezaji watano wameonyesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vikubwa ambao ni Kampuni ya Gesap Agro Farming Co Ltd ya Morogoro kwa kujenga kiwanda cha maziwa katika wilayani Missenyi na Kampuni ya BenBuild Investment Limited iliyoanza ujenzi wa Kiwanda cha Vigae eneo la Kihanga wilayani Karagwe.
Wawekezaji wengine ni KADERES PLC anayetarajia kujenga kiwanda cha kahawa wilayani Muleba,Sying Investment Company Limited ya nchini China inayotarajia kujenga kiwanda cha nyama katika wilaya ya Missenyi na Kampuni ya Ndyanga Co Limited ya Muleba kujenga kiwanda cha maji wilayani Muleba. 
Viwanda vikubwa vya muda mrefu vilivyoko mkoani humo ni pamoja na cha sukari cha  Kagera Sugar kilichobinafishwa mwaka 2001.
Viwanda vya uchakataji samaki vya Kagera Fish Co Ltd kilichopo eneo la Kemondo wilaya ya Bukoba na Supreme Perch Ltd kilichopo Nyamukazi wilaya ya Bukoba.
Kiwanda cha Chai Kagera kilichopo Maruku wilaya ya Bukoba kilichobinafishwa na Serikali mwaka 2000 kutoka iliyokuwa Mamlaka ya Chai Kagera.
Vingine ni viwanda vya kahawa vya  TANICA kilichopo Manispaa ya Bukoba ,BUCOP kilichopo katika wilaya ya Bukoba eneo la Custom kilichoanzishwa mwaka 1935 na Kiwanda cha Olam (T) Ltd kilichopo katika wilaya ya Missenyi eneo la Bunazi.
"Mkoa wa Kagera  wenye  Halmashauri nane ambazo ni Biharamulo,Bukoba Vijijini,Manispaa ya Bukoba,Kyerwa,Karagwe,Missenyi,Muleba na Ngara  umefanikia kutekeleza maelekezo ya Rais Dakta John Pombe Magufuli katika suala zima la ujenzi wa Viwanda kwa kila Mkoa" .Alisisitiza Diwani Athumani.
Pia  amevitaja Viwanda vingine kuwa ni Kiwanda cha chai Kagera (Kagera Tea  Co.Ltd ambacho kipo eneo la  Maruku Wilaya ya Bukoba  ambacho kilibinafisishwa na Serikali mwaka 2000 na kukabidhiwa  kwa mwekezaji ambaye ni mzawa.
Pia  kuna Kiwanda cha  TANICA ambacho kipo katika Manispaa ya Bukoba  na ambacho kilibinafisishwa  na Serikali na kukabidhiwa Chama cha  Ushirika cha Mkoa (KCU 1990).  Ameeleza Diwani Athumani.
Alifafanua kwamba Mkoa wa Kagera bado unazo fursa  nyingi na muhimu kwa  ajili ya kuvutia  wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambao unaweza kufanywa katika sekta  za Kilimo,Viwanda, Utalii, Uvuvi, Ufugaji ambapo Mkoa tayari umetenga zaidi ya hekta 58,000.
Hata  hivyo  alitaja baadhi ya changamoto  zilizopo katika fursa za uwekezaji kuwa maeneo mengi  ya uwekezaji na ujenzi wa Viwanda hayajapimwa, urasimu na mlolongo mrefu na ukiritimba katika upimaji wa ardhi na kukosekana kwa mfumo mzuri na wa haraka  katika upimaji wa ardhi ilikuvutia zaidi wawekezaji
Pia Changamoto nyingine ni upungufu wa watumishi  katika halmashauri  za  Wilaya za Mkoa huo  alieleza Diwani Athumani Katibu Tawalawa Mkoa huo wa Kagera.


Comments