Featured Post

ASKARI WAWILI WAMEFUKUZWA KAZI KWA FEDHEHA HII NI BAADA YA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI


  • MWANAMKE MMOJA MTAWA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KILE KINACHODAIWA KUJIRUSHA TOKA GHOROFA YA PILI YA HOSPITALI YA BUGANDO HADI CHINI WILAYANI NYAMAGANA.
  • ASKARI WAWILI WAMEFUKUZWA KAZI KWA FEDHEHA HII NI BAADA YA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
KWAMBA TAREHE 27.08.2018 MAJIRA YA SAA 05:00HRS ALFAJIRI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO ILIYOPO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA MTAWA AITWAYE SUZANA BATHLOMEO, MIAKA 48, MKURUGENZI WA MIPANGO NA FEDHA WA HOSPITAL YA RUFAA YA BUGANDO, ALIJIRUSHA TOKA GHOROFA YA PILI YA HOSPTALI YA RUFAA YA BUGANDO NA KUDONDOKA CHINI. MTAWA HUYO AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO YA TAREHE 28.08.2018, WAKATI AKEIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO, NA KUPELEKEA KUUMIA  MAENEO YA KIUNO NA MGONGO, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
CHANZO CHA TUKIO HILO BADO TUNACHUNGUZWA, HATA HIVYO UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA KUWA KATIKA OFISI ALIYOKUWA AKIIFANYIA KAZI  MAREHEMU AMBAPO YEYE ALIKUWA KIONGOZI ZIPO TUHUMA ZA UPOVU WA FEDHA ZAIDI YA MILIONI MIA TATU, AMBAZO ZILIPELEKEA BAADHI YA WATUMISHI WENZAKE KUSIMAMISHWA KAZI ILI KUPISHA UCHUNGUZI NA WENGINE KUFUKUZWA KAZI.
AIDHA POLISI BADO WAPO KATIKA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI JONATHAN SHANA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOONA WAMEKWENDA KINYUME NA TARATIBU ZA KAZI KAMA VILE KUJITOA UHAI AU KUJIJERUHI KWANI NI KOSA KISHERI. AIDHA SAMBAMBA NA HILO ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE 23.08.2018 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA MTAA WA NYAMHONGOLO WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAWILI AMBAO NI 1.H.5461 PC ENOCK WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MWANZA NA ASKARI 2.H.4165 D/C ROBERT WA KIKOSI MAALUMU, WALIKAMATWA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI AMBAZO NI MENO MAWILI YA TEMBO, KISHA JANA TAREHE 27.08.2018, ASKARI HAO WALIFUKUZWA KAZI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI ZILIPATIKANA TAARIFA KUWA WAPO WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA MENO YA TEMBO, NDIPO TAARIFA HIZO TULIZIFANYIA KAZI KWA KUSHIRIKIANA NA KIKOSI CHA TAIFA CHA KUPAMBANA NA UJANGILI KANDA YA ZIWA NA BAADAE TULIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA TAJWA HAPO JUU HUKU WAKIWA NA MENO HAYO MAWILI YA TEMBO. ASKARI HAO TUNATARAJIA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 31.08.2018.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI JONATHAN SHANA ANATOA WITO KUWA SHERIA NI MSUMENO, SHERIA NI KWA WATU WOTE, SHERIA HAINA DINI, HAINA KABILA, SHERIA HAINGALII KAZI AU CHEO CHA MTU, YEYOTE AMBAE NI MHALIFU MKONO WA SHERIA LAZIMA UCHUKUE HATUA DHIDI YAKE. HIVYO TUTAWASAKA WALE WOTE MASWAHIBA WAO AMBAO WALIKUWA WANANUNUA NA KUUZA MENO HAYO.

Comments