Featured Post

UBALOZI WA JAPAN WAMUUNGA MKONO WAZIRI UMMY MWALIMU KUJENGA MADARASA SITA YA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA JIJINI TANGA


Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akisaini na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. wanaoshuhudia ni Mstahiki meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida wakionyesha hati za makubaliano ya msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto wakibalishana hati za makubaliano na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.

 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida kulia Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Waziri Ummy akishukuru Ubalozi wa Japani kwa kusaidia juhudi za sekta ya elimu
 Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kulia akiwa na Balozi wa Japan nchini katikati mara baada ya kumalizika makubaliano hayo

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.
SHIRIKA la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga (Tanga Women Development Initiative-TAWODE) chini ya Mwenyekiti wale Waziri Ummy Mwalimu (MB) leo wamewekeana saini ya ujenzi wa madarasa sita ya shule ya msingi kata ya Tanga sisi katika Jiji la Tanga.

Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.

Akizungumza katika halfa hiyo Mh Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida alisema serikali ya Japan imetoa fedha hizo ili kuwasaidia maendeleo ya elimu kwa Jiji la Tanga ili kutatua tatizo la mrundikaano wa wanafunzi madarasani huku akiwataka Tawode kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu na kukamilika kwa wakati.

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aliushukuru ubalozi wa Japan kwa kukubali ombi lao la kufadhili ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Mwakidila ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1400 kulinganisha na madarasa machache yaliyopo na hivyo kusababisha mrundikano mkubwa kwa wanafunzi.

Aidha Waziri Ummy alieleza kuwa ongezeko la wanafunzi limechangiwa na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kutoa elimu bure hivyo wakati serikali ikiweka jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya elimu katika Halmashauri mbalimbali kote nchini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madarasa.

Alisema kutokana na hilo wao kama sehemu ya wana jamii wa Jiji la Tanga waliona wana wajibu wa kutafauta vyanzo vingine vya fedha ili kuwezesha elimu ya msingi mpaka kidato cha nne kutolewa bure bila vikwazo vyoyote.

Waziri Ummy alisema fedha zilizotolewa na ubalozi wa Japan ni za Jamii ya wana Tanga kwa maendeleo ya Tanga hivyo shirika la TAWODE kupitia Halmashauri ya Jiji la Tanga itahakikisha msaada huo unatumika kikamilifu na mradi kukamilika kwa wakati ili kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani.

Naye kwa upande wake,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustapa Mhina Selebosi aliushuruku ubalozi wa Japan kwa kufadhili ujenzi wa madarasa hayo ikiwemo kumpongeza Waziri Ummy Mwalimu kwa kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa Jiji la Tanga hasa katika sekta ya Afya na Elimu.

Hata hivyo pia Mstahiki Meya hiyo alimkaribisha Balozi wa Japan kutembelea Jiji la Tanga ikiwemo shule ya Sekondari ya Japani iliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Comments