Featured Post

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MIUNDO MBINU YA BARABARA KUWAWEZESHA WAKULIMA KUYAFIKIA MASOKO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kujenga miundo mbinu ya barabara hasa za ndani kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kuyafikia masoko. 


Makamu 
wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika 
kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa 
ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. “Serikali 
imetoa shilingi bilioni 6 kujenga barabara ya Rujewa – Ubaruku inajengwa 
kwa kiwango cha lami”.
Makamu wa Rais ameipongeza kampuni ya 
Kapunga Rice Project Ltd kwa kujenga kituo cha afya kitakacho hudumia 
watu zaidi ya elfu kumi na kulaza wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Aidha 
Makamu wa Rais amesema migogoro yote itafanyiwa kazi kuhakikisha haki 
inapatikana kwa kila mmoja. 
Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la 
Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed ameahidi kuwalipia deni la shilingi 
milioni 800 wakulima wanaodaiwa deni waliokupa kununulia power tiler
. Mbunge huyo wa Mbarali amesema kuwa Serikali ya awamu imetoa shilingi 
milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. 
Akizungumza 
na Wananchi wa Kapanga katika mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge la 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameahidi kutoa mifuko 
200 kutoka kwenye Taasisi yake ya Tulia Trust kusaidia ujenzi wa Wodi ya 
Wazazi katika kituo cha Kapunga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu 
Hassan akiangalia mchele unaozalishwa na kampuni ya Kapunga Rice Project 
Ltd, kulia ni Mkuu wa kampuni hiyo nchini Bw. Nillard Chawdry akimpa 
maelezo Makamu wa Rais namna wanavyotumia teknolojia ya kisasa katika 
kukoboa na kufungasha mpunga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu 
akihutubia wananchi wa kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya. 
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika 
kituo cha afya Kapunga,pichani kushoto ni Mkuu wa kampuni ya Kapunga 
Rice Project Ltd Bw. Nillard Chawdry. Kituo hicho kimejengwa na Kapunga 
Rice Project Ltd kitakacho hudumia watu zaidi ya elfu 10 na kulaza 
wagonjwa 42 kwa wakati mmoja. Kituo cha Afya Kapunga ambapo Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi. Sehemu ya Wakazi wa kijiji cha Kapunga waliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Comments