HARARE, ZIMBABWE Rais wa Zimbabwe,
Robert Mugabe alijiuzulu mwishoni mwa mwaka baada ya kuwa madarakani kwa
karibu miongo minne. Haya ni mambo 10 ambayo yatakufanya uelewe nchi
hiyo imefikia wapi hivi sasa.
Rais mmoja ametawala tangu uhuru Rais
Mugabe aliyeongoza vuguvugu la kimapinduzi , amekuwa madarakani tangu
nchi hiyo ilipojipatia uhuru mwaka 1980.Kwanza alitumikia taifa hilo
akiwa waziri mkuu mpaka alipoanzisha mfumo wa urais mwaka 1987. Lakini
miaka yake ya kuwa madarakani Zimbabwe imekuwa katika mgogoro mkubwa wa
kiuchumi na kutawala kimabavu.Yeyey na wanaomuunga mkono walikuwa
madarakani kwa muda mrefu wakitumia vurugu na mauaji kama njama za
kushinda chaguzi.
Milioni 231% ,kupanda kwa gharama za maisha Julai mwaka 2008 Uchumi wa Zimbabwe umezorota tangu kufanyika mabadiliko ya sera ya ardhi mwaka 2000 Programu
hii ilishuhudia wamiliki wa ardhi wazungu wakinyang'anywa ardhi na
kupewa raia weusi wa Zimbabwe na wale wenye uhusiano mzuri na wanasiasa,
hali hii iliangusha hata uzalishaji nchini humo. Wakati Benki kuu
ya nchini humo ikichapisha pesa kuondoka kwenye mdororo wa kiuchumi,
kupanda wa gharama za maisha kukashika hatamu.
Chati inayoonyesha kupanda kwa gharama za maisha
Ingawa Benki ya dunia haina takwimu za mwaka 2008 na
2009, Takwimu za benki kuu ya Zimbabwe zinaonyesha gharama za maisha
zilipanda na kufikia milioni 231% mwezi Julai mwaka 2008. Maafisa waliacha kuripoti takwimu za kila mwezi baada ya gharama za maisha kupanda maradufu mwezi Novemba mwaka 2008. Zimbabwe
ililazimika kuachana na matumizi ya sarafu yao mwaka mmoja baadae kwa
kiasi cha dola ya zimbabwe quadrillioni 35 kwa dola moja ya Marekani.
$16.3bilioni = GDP mwaka 2016 Kipindi
cha mwaka 2009 na 2012 kilikabiliwa na changamoto kubwa, imesema Benki
ya dunia.Uzalishaji umeshuka kwa wastani wa 8% kutoka mwaka 2009 mpaka
2012, kutokana na biashara kuyumba na ukame. Rais Mugabe wakati
wote amekuwa akilaumu mataifa ya magharibi kuwa matatizo ya kiuchumi ya
Zimbabwe yamesababishwa na nchi za magharibi,wakiongozwa na Uingereza
ambayo alidai kuwa ilipanga kumuondoa madarakani baada ya kuwanyang'anya
wazungu mashamba.
74% ya watu wanaishi kwa chini ya dola 5.50 kwa siku Hali ya kisiasa na uchumi mbaya nchini humo vimesababisha kuwapo kwa viwango vikubwa vya umasikini. Miaka
migumu kati ya mwaka 2000 na 2008 kulishuhudia viwango vya umasikini
kupanda kwa zaidi ya 72%, kwa mujibu wa Benki ya dunia. Moja ya tano ya
idadi ya wakazi waliishi kwenye umasikini uliokithiri. Umasikini uliokithiri, unakadiriwa kushuka tangu mwaka 2009 mpaka mwaka 2014.
Takriban 27% ya watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano wako katika hali baya ya kiafya kwa sababu ya lishe duni, utafiti
wa kiafya nchini humo ulibaini mwaka 2015. Lakini umasikini
nchini Zimbabwe uko chini kuliko nchini ningine zilizo kusini nwa jangwa
la Sahara,ambapo 41% ya watu wanaishi kwa kiwango cha chini ya dola
1.90 mwaka 2013.Kwa mujibu wa data za Benki ya dunia.
90% = Kiwango cha ukosefu wa ajira
Benki ya dunia ilitoa makadirio yake kwa kutazama
data za shirika la kazi duniani iliyoeleza kuwa idadi ya watu wasio na
ajira imefikia 90% mwaka huu. Hata hivyo, Tafsiri ya benki ya
dunia imelenga wale ambao wanatafuta kazi.Wengi wao ambao hawajahesabiwa
huenda wasiwe wanatafuta kazi ingawa wanataka, wanaona kama nafasi za
kazi ni chache au kwa sababu wanakumbwa na vikwazo mbalimbali kama
unyanyapaa, masuala ya kitamaduni na kijamii.
89% = kiwango cha elimu kwa watu wazima Kutokana
na uwekezaji mkubwa uliowekwa tangu uhuru,Zimbabwe ina idadi kubwa ya
watu wazima wenye elimu barani Afrika, kiasi cha 89%, kwa mujibu wa data
za benki ya dunia tangu mwaka 2014. Ulimwenguni kiwango cha elimu ni asilimia 86 mwaka 2016 na nchi za kusini mwa jangwa la sahara 64%(takwimu za mwaka 2015).
Data zinazoonyesha takwimu za kiwango cha elimu Zimbabwe
Karibu wanawake wote na wanaume wenye umri wa miaka
15-49 wana angalau kiwango cha elimu ya msingi, kwa mujibu wa utafiti
uliofanyika nchini humo mwaka 2015.Zaidi ya 70% ya watu walio na umri wa
miaka 15-49 wamesoma mpaka elimu ya sekondari.
13.5% = Idadi ya watu wazima waishio na virusi vya Ukimwi Zimbabwe
ni nchi ya sita kusini mwa jangwa la sahara ikiwa na idadi ya watu
milioni 1.3 waishio na virusi vya ukimwi kwa mwaka 2016, kwa mujibu wa
UNAIDS Hata hivyo, baada ya mwaka 1997, viwango vimekuwa vikishuka.
Chati inaonyesha kupanda na kushuka kwa viwango vya watu walio na virusi vya ukimwi nchini Zimbabwe
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa,haya ni matokeo ya
kampeni zilizofanikiwa kuhamasisha matumizi ya mipira ya kiume pia
programu za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.Matibabu
na huduma kwa walioathirika zimeboreshwa.
60 =Umri wa kuishi Umri
wa kuishi ulishuka miaka ya 1990, watu walipoteza maisha hasa kutokana
na virusi vya Ukimwi.Umri wa kuishi ulishuka kutoka miaka 61.6 mwaka
1986 mpaka 43.1 mwaka 2003.
Chati inayoonyesha umri wa kuishi Zimbabwe
Kwa sasa hali imetengamaa tena, lakini kutokana na
ukosefu wa ajira na umasikini na maambukizi ya Ukimwi, umri wa kuishi
umeendelea kuwa miaka 60 mwaka 2015, kwa mujibu wa Data wa Benki ya
dunia.
Watu 81 kati ya 100 wanatumia simu za mkononi Simu za mkononi hutumika sana kama njia ya mawasiliano na raia wa Zimbabwe Lakini
wakati wengi wakiwa na simu za mkononi, 42% ya nyumba zina redio, 37%
zina televisheni na 10% zina Kompyuta.Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi
ya utafiti, Zimbawe Demographic and Health.
Chati zinaonyesha ongezeko la matumizi ya simu za mkononi nchini Zimbabwe
16.7 million =Idadi ya watu Baada
ya Uhuru mwaka 1980, kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa na
ongezeko la watu wanaopoteza maisha vimefanya kushuka kwa ongezeko la
watu Kutokana na idadi ya watu wengi wanaoondoka nchini humo, bado idadi ya watu haijafikia ile iliyokuwa baada ya uhuru.
Comments
Post a Comment