Featured Post

KENYA, RWANDA ZANG'ARA KWENYE VIWANGO VYA UVUMBUZI DUNIANI



Ripoti ya Global Innovation Index (GII) 2018 Imetolewa mjini New York nchini Marekani, katika toleo lao la 11 ambalo linalenga kuwasaidia watunga sera kuelewa namna ya kuchochea shughuli za uvumbuzi na ubunifu ambazo zinaweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya watu na uchumi.

Ripoti hiyo imetoa orodha ya mataifa yanayofanya vyema kwenye masuala ya uvumbuzi duniani, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini na Mauritius zikiwa nchi zinazofanya vizuri kusini mwa jangwa la Sahara.
Ripoti hii imezitazama nchi 126 duniani kwa kuzingatia viashiria vya mazingira ya kisiasa, elimu,miundombinu, biashara na uchumi.

Afrika Kusini
Ni nchi ya kwanza kwenye orodha hiyo kwenye eneo la kusini mwa jangwa la sahara na nafasi ya 58 duniani.Imeonyesha nguvu yake kwenye sekta ya masoko na biashara, pia katika masuala ya mikopo ya kibenki, ubora katika tafiti mbalimbali za kisayansi kwenye vyuo vikuu vyake hasa Cape Town , Chuo kikuu cha Witwatersrand na Stellenbosch.

Mauritius
Imeifuatia Afrika Kusini, kutokana na nguvu iliyoonyesha kwenye masuala ya kibiashara, mazingira ya ukopeshaji, usalama na uimara kisiasa, pia imekuwa ikiwezesha kusomesha wanafunzi wa sekondari, umahiri katika matumizi ya nishati na biashara.

Kenya
Kenya imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ukiwa ni muendelezo tangu mwaka 2011, ikionyesha mafanikio kwenye utoaji mikopo kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wajasiriamali, usafirishaji wa biashara ya bidhaa zitokanazo na ubunifu kama vile uchongaji na uandishi.
Nchi nyingi za kiafrika hazijaonekana wenye ripoti hii kutokana na changamoto mbalimbali ambazo wataalamu wa masuala ya kiuchumi wameziweka wazi.
Tanzania ni Miongoni wa nchi za Afrika Mashariki ambazo hazimo katika ripoti hii.
''Kwa sehemu kubwa ripoti hizi hutolewa kutokana pia na kasi ya kujitangaza, lakini pia serikali yetu ina wabunifu wengi sana lakini tatizo ni kuwa hawapati nafasi ya kuendelezwa baada ya uvumbuzi , hakuna taasisi zinazowajibika kuwaendeleza watu wanafanya vizuri katika kazi mbalimbali za ubunifu na uvumbuzi na kuwawezesha kwa kuboresha na kutangaza kazi zao ndani na nje ya mipaka ya Tanzania'' ameeleza mchambuzi wa masuala ya kiuchumi na kijamii, Betty Masanja.
''Maendeleo yeyote yanakuja kutoana na tafiti mbalimbali ambazo hufanywa na kufanyiwa kazi na serikali husika ili kusaidia katika kusukuma maendeleo ya nchi husika kwa mfano katika fani za sayansi, uchumi na biashara''.
''Iwapo serikali zetu zitaishia kuweka tafiti hizi kwenye makablasha basi upigaji hatua katika kuyafikia maendeleo utakuwa mgumu'' alieleza.

Comments