- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Idara ya polisi nchini India imewaamuru maafisa wake
kupunguza uzito vinginevyo watasimamishwa kazi.
Mkuu wa idara hiyo katika jimbo la Karnataka ameiambia BBC
kuwa alikuwa na wasiwasi kuhusu ongezeko la maafisa wenye vitambi.
Bhaskar Rao amesema alichukua uamuzi huo baada ya maafisa
zaidi ya 100 kupoteza maisha katika kipindi cha miezi 18 iliyopita kutokana na
maradhi yaliyo na uhusiano na mtindo wa maisha
Maafisa hao watapatiwa usaidizi kwa ajili ya kubadili mfumo
wa maisha na namna ya kula.
Idara ya Polisi katika jimbo hilo lina askari 14,000, ambao
hutazama hali ya usalama wakati wa matukio makubwa na kudhibiti maandamano na
vurugu.
Maafisa wa juu wa kikosi cha KSRP kimekuwa kikiamriwa
kuwatambua maafisa wenye uzito mkubwa na kuwaweka katika mpango wa kufanya
mazoezi ili kupunguza uzito.
''Tumeanza kazi ya kuwafuatilia maafisa kwa kupima sukari na
vipimo vingine miezi sita iliyopita.Hatua hii mpya ya kusimamishwa kazi ni
kitisho kwa wale wasiojali afya zao,'' Rao aliiambia BBC.
Sio kawaida kuwaona Polisi nchini humo wakifanya mazoezi
kuondokana na tatizo la uzito mkubwa.
''Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, polisi 153
walipoteza maisha, kati ya hawa, 24 walifariki kutokana na ajali za gari na
wengine 9 walijiua.Wengine walipoteza maisha kutokana na maradhi
yaliyosababishwa na mtindo wa maisha kama vile maradhi ya moyo na kisukari.Hii
ni tahadhari kubwa kwa kikosi,'' alisema Rao.
Ameongeza kuwa maafisa walikuwa wakila zaidi vyakula vya
kukaanga, walikuwa wakivuta sigara, kunywa pombe na hawakuwa wakifanya mazoezi.
Mafunzo ya kuogelea, Yoga na michezo mingine imeanza
kutolewa kwa maafisa.
''Mafunzo yameanza kutolewa baada ya kufanyika vipimo na
mazoezi yatafanyika kwa kuzingatia ushauri wa madaktari,'' alieleza Rao.
Comments
Post a Comment