Featured Post

DIAMOND: NINAWAZIMIA SANA Q CHILLAH, TID NA BAKHRESSA



Iwapo unazungumzia kuhusu fedha, kuhusu muziki bora, tuzo na ushawishi basi Diamond ndio mwanamuziki mwenye ufanisi Afrika mashariki.
Kifedha msanii huyo wa muziki wa bongo anamiliki mali Tanzania mbali, biashara zilizofanikiwa, na ameteuliwa na kushinda mataji kadhaa ya kimataifa kama vile BET na MTV.

Ushawishi wa msanii huyo unaweza kupimwa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii: Kwa mfano ana mashabiki milioni 4.8 katika mtandao wa Instagram, milioni 2.5 katika mtandao wa facebook na milioni 1.3 katika mtandao wa Youtube mbali na wafuasi elfu 574 katika mtandao wa Twitter.
Na hivi majuzi msanii huyo wa wimbo 'Iyena' na 'sikomi' alichapisha orodha ya watu waliokuwa kiungo muhimu katika ufanisi wake.
Alimuorodhesha mamake Sanura Kassim, AY TID, Dully Sykes, Jay Z , P Diddy, Usher Raymond miongoni mwa wengine kama watu waliochangia sana katika kukuwa kwa muziki wake.

Sanura Kassim
Mamake Diamond Platinumz

AY
Ambwene Allen Yessayah, kwa jina maarufu A.Y. ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania.
Alizaliwa tarehe 5 mwezi July, 1981, mjini Mtwara, Kusini mwa Tanzania.
Alianza usanii na kundi kwa jina S.O.G. mwaka 1996.
Mwaka 2002 aliamua kufanya muziki akiwa pekee.
Amewahi kushinda mataji kama vile Channel O Music Video Awards, Pearl of Africa Music Awards.
Vilevile amewahi kuteuliwa kuwania mataji ya MTV Africa Music nyimbo bora ya Hip Hop.
Aligonga vichwa vya habari baada ya kanda ya video ya wimbo wake 'Zigo' alioimba na Diamond Platinumz kupigwa marufuku nchini Tanzania.
Video hiyo ilipogwa marufuku kutokana na picha zake za utupu.

TID
Ni mwanamuziki wa Tanzania ambaye jina lake kamili ni Khalid Mohamed.
TID ina maana ya 'Top In Dar es Salaam' mjini anakoishi.
Anajulikana sana kwa nyimbo zake 'Zeze' na 'siamini'.
Alianza kuimba mwaka 1994 na kundi kwa jina Black Gangsters.
Alianza kuimba pekee miaka mitano baadaye akiwa na umri wa miaka 21 baada ya kuandikisha mkataba na Poa Records.
Wimbo wake wa kwanza 'Mrembo' ulitolewa 2002.
Aliwahi kuigiza katika filamu ya Girlfriend.

Dully Sykes
Msanii huyo anayejulikana kikamilifu kama Abdul Sykes alizaliwa tarehe 4 mwezi Disemba 1980.
Ni msanii wa Tanzania anayejulikana kuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa bongo fleva nchini humo.
Pia akijulikana kuwa Mr Misifa ama Mr Chicks amezuru Uingereza na ni mmoja wa waanzilishi wa muziiki wa kiswahili wa dance Hall katika maeneo ya maziwa makuu.
Ni maarufu kwa nyimbo zake Julieta, Salome, Historia ya Kweli na Leah.

Mr. Blue
Khery Sameer Rajab alizaliwa tar. 14 Aprili 1987.
Ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania.
Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue.
Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki wa muziki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue' ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.
Mr Blue alikuwa gumzo wa wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na ujanja wa ala ya muziki wenyewe.

Q Chila

Eric Shigongo
Eric Shigongo ni mjasiriamali ambaye alijikita katika uandishi wa vitabu.
Amezaliwa mnamo tarehe 10- 8-1969.
Mpaka sasa ana vitabu vingi kamaː Malkia wa Masokwe, Damu na Machozi, Raisi Anampenda Mke Wangu, Siri Iliyotesa Maisha Yangu na mwisho Maisha ya Mike.

Jay-Z
Akijulikana kwa jina Shawn Corey Carter (alizaliwa mnamo tarehe 4 mwezi Disemba 1969) akijulikana kama Jay-Z.
Ni mwanamuzi wa wa aina ya Rap , mtunzi, mwandishi, mtayarishaji na mfanyibiashara.
Ni miongoni mwa wasanii ambao muziki wao umeuzwa sana duniani na mmoja wa wanamuziki wakubwa wa mtindo wa Rap.
Ameshinda tuzo 21 za Grammy Awards, pamoja na Kanye West..

Joseph Kusaga
Ni mkurugenzi wa Cloud Media nchini Tanzania
Joseph Kusaga ni mjasiriamali mwenye mawazo makubwa na ujuzi aliyependa muziki.
Awali Joe aliwahi kuwa DJ na alishiriki katika hafla tofauti za muziki katika maeneo mengi nchini Tanzania akicheza muziki.

P Diddy
Kwa jina Sean John Combs (alizaliwa mwezi Novembea 4, 1969), kwa jina maarufu kama Puff Daddy, Puffy, P. Diddy, Diddy.
Ni msanii wa Marekani, mwimbaji, mtunzi, muigizaji, mtayarishaji na mfanyibiashara.
Alizaliwa mjini New York na kulelewa katika eneo la Mount Vernon, mjini New York.
Alifanya kazi kama mkurugenzi wa vipaji katika kampuni ya Uptown Records kabla ya kuanzisha kampuni yake ya Bad Boy Entertainment 1993.
Albamu yake ya kwanza No Way Out (1997) iliuza mara milioni saba

Usher Raymond
Usher Raymond IV (alizaliwa mnamo mwezi Oktoba tarehe 14, 1978).
Ni msanii wa Marekani , mwandishi na mchezaji densi. Alizaliwa mjini Dalls, Texas ma kulelewa katika eneo la Chattanooga, Tennessee hadi alipoelekea Atlanta, Georgia.
Akiwa na umri wa miaka 12, alimuigiza katika shindano la kuimba kabla ya kuvutia kampuni ya muziki ya A&R kutoka LaFace Records.
Alitoa albamu yake, Usher (1994) lakini alipata umaarufu miaka ya 90 alipotoa albamu yake ya pili My Way (1997).

Shah Rukh Khan
Shah Rukh Khan (alizaliwa na kupewa jina Shahrukh Khan; tarehe 2 mwezi Novemba 1965).
Akijulikana kama SRK, ni muigizaji wa filamu na mtayarishaji.
Akijulikana katika mtandao kama "Badshah of Bollywood", "King of Bollywood", "King Khan", ameigiza katika takriban filamu 80 na kushinda mataji kadhaa ikiwemo lile la 14 Filmfare Awards.
Khan ana ushabiki mkubwa barani Asia pamoja na nchini India.
Ametajwa kuwa mmojawapo wa waigizaji waliofanikiwa zaidi duniani.

Said Bakhresa
Said Salim Awadh Bakhresa (alizaliwa 1949 Zanzibar). Ni mfanyibiashara wa Tanzania.
Ndio mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni za Bakhresa Group Of Companies.
Ni mfanyibishara nchini Tanzania na kisiwa cha Zanzibar.

Comments