Featured Post

AWESO AWAONYA WAHANDISI WA MAJI NCHINI


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akionyeshwa na wananchi wa Kijiji cha Manolo Kata ya Manolo wilayani Lushoto maji wanayotumia kutoikana na kukabiliana na uhaba wa maji wakati wa ziara yake juzi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mgwashi Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akipata maelekezo wakati wa ziara yake ya akikagua vyanzo vya maji kwenye Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto wakati wa ziara yake katikati ni mhandisi wa maji Halamshauri hiyo Samadu Makau

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji kwenye kijiji cha Mgwashi wilayani Lushoto wakati wa ziara yake


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amewaonya wahandisi wa maji nchini wanaoshindwa kusimamia miradi ya maji kwenye maeneo yao na kupelekeea fedha zinazotolewa na serikali kushindwa kutumika kama iliyokusudiwa badala yake wanazitumia kulipana posho.

Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa juzi wakati wa ziara yake ya kutembelea Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto alipokuwa akikagua miradi ya maji huku akilazimika tena kumsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Samadu Makau kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa Maji Mgwashi wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5 na kupelekea wananchi kukosa maji.

Naibu Waziri ambaye alianza ziara yake mkoani Tanga kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe,Lushoto na Halamshauri zote ndani ya wilaya hizo ambapo alibaini kuwepo kwa ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali katika miradi ya maji tokea mwaka 2012 kutokana na kutokuwepo kwa usimamizi makini wa watendaji wa serikali.

Alisema ubadhirifu na upotevu wa fedha za Serikali inatokana na wahandisi wa maji wa mikoa na wilaya waliopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo na kushauri kushindwa kuwajibika ipasavyo hivyo kupelekea kuingiza hasara na kupelekea wananchi kukosa maji hivyo Wizara kuanza kutilia mashaka taaluma zao.

Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani serikali inapeleka fedha nyingi kwenye miradi ili kuweza kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi huku wahandisi hao wa maji wakishindwa kusimamia kwa waledi miradi hiyo huku Serikali ikiwalipa fedha za mishahara kwa ajili ya kuisadia majukumu hayo.

“Haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa lengo la kuondokana na adha hiyo huku wahandisi waliopo kwa niaba ya Serikali wakishindwa kuisimamia badala yake unapewa taarifa ya ubabaishaji kila maeneo ya miradi unapotembelea”Alisema.

“Kutokana na mradi huu kutumia muda mrefu bila kuwepo kwa mafanikio yoyote ni dhahiri Mhandisi utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo niagize asimame kazi hii kwani haweze kutusaidia kwenye masuala ya maji hivyo ukae pembeni utipishe maana hauna msaada kwetu “Alisema.

Kabla ya kuchukua maamuzi hayo Naibu Waziri Aweso alisema eneo la Mgwashi kumekuwa na changamoto kubwa kutokana na serikali kupeleka fedha nyingi lakini maji wananchi hawajaweza kupata huduma ya maji ili kuweza kuendana na azma ya Rais Dkt John Magufuli ya kumsaidia kumtua ndoo kichwani mwanamama ikiwemo kutokutembea umbali usiozidi mita 400.

“Lakini hata mbunge wenu hapa January Makamba ameniambia kuhusu mradi huu wa Mgwashi umekuwa kama una magumashi umetumia fedha nyingi lakini maji hayaonekani hata yanayopatikana umbali mrefu na kupelekea shida kwa wananchi kutembea umbali mrefu hii sio sawa kabisa”

Naye kwa upande wake,Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Bumbuli,Makau alimueleza Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2009 na ulitakiwa uwe na tanki mmoja la ujazo wa lita 225,000 na matenki mawili ya ukarabati huku moja ya tanki hilo likiwa na lita 225000 lilopo katika kijiji cha Kihitu huku tenki lengine 90 elfu tisini. Alisema mradi huo una vituo 54 vya kuchotea maji kutokana na aina iliyofanyika hivyo mateki ya huku mawili ililoukatabati 225,000 na elfu 90 linatakiwa kuhudumia vituo 45 wakati la huku linatakiwa kuhudumia vituo vyengine vilivyobakia ili kukamilisha idadi husika.

Comments