Featured Post

UCHUNGUZI WA MATITI WA MARA KWA MARA UNA 'MADHARA KULIKO FAIDA'



LONDON, UINGEREZA
UCHUNGUZI wa mara kwa mara wa ziwa la mama ''unaweza kusababisha madhara kuliko faida'' na kwa wanawake ambao hukosa uchunguzi huo wanastahili kuendelea na maisha yao, madaktari wamesema.
Kundi la madaktari wa afya 15 wameliandikia gazeti la the Times wakisema wanawake hawastahili kuwekwa katika ''hali ya wasiwasi''

Hii ni baada ya wanawake 450,000 kutoka England kukosa mualiko kwa uchunguzi huo wa kila wakati kutokana na hitilafu za kompyuta.
Mashirika ya kutoa msaada kwa wagonjwa wa saratani ya matiti wamesema mpango huo wa uchunguzi unawapatia wanawake ''nafasi bora'' ya matibabu iwapo ugonjwa huo utagundulika mapema.

'Hakuna tofauti'
Kwenye barua hiyo kwa gazeti hilo, kikundi cha wasomi wamesema wanawake wenye umri wa miaka 70-79 ambao huenda kufanyiwa uchunguzi huo wanastahili kutafuta usaidizi iwapo watagundua wanauvimbe wowote ama dalili za ugonjwa huo.
"Wanawake wengi na madaktari sasa wanajiepusha na uchunguzi huo kwa sababu hauna manufaa yoyote ya kusababisha vifo."
Uchunguzi huo wa matiti kwa mara nyingi husababisha madhara kuliko faida, jambo ambalo limeanza kufahamika kimataifa.
Madai ya kuyaokoa maisha ya watu kutokana na uchunguzi huo yanasawazishwa na vifo, madaktari hao wamesema.
Na saratani ambazo ni hatari na zilizo katika kiwango kibaya hazizuiliwi na mpango huo wa uchunguzi , wamesema.
Miongoni mwa waliotia saini barua hiyo ni Susan Bewley, profesa wa wanawake wa chuo cha taasisi cha Kings, na Michael Baum profesa wa upasuaji wa chuo kikuu cha London.
Makosa yaliorodheshwa kutoka mwaka 2009 , yalitolewa wiki iliyopita. Wanawake 270 nchini Uingereza wamefariki kwa kukosa kurudi kwa uchunguzi kwa mara nyengine.
Wanawake 309,000 ambao walikuwa hai watatumiwa barua mwishoni mwa mwezi Mei ya kuwaomba kurudia uchunguzi huo wa matiti.
Mamlaka ya huduma ya afya -NHS imekadiri uchunguzi huo huokoa maisha ya mtu mmoja kati ya 200 ambao wamefanyiwa uchunguzi huo, na huyaokoa maisha ya watu 1,300 kwa mwaka nchini Uingereza.
Lakini kati ya wanawake 200 watatu ambao wamefanyiwa uchunguzi hupatikana na saratani ambayo haihatarishi maisha ya binadamu na kujumuisha wanawake 4,000 kila mwaka hupokea matibabu yasiyostahli.
Muuguzi aliyestaafu Maggie Whyte , 61, kutoka Edinburgh aligundua kwamba alikuwa na saratani ya matiti katika kiwango cha mwanzo alipokuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara.
"Nilikuwa na bahati ilikuwa haijasambaa kwenye tezi," alisema matibabu aliyoyapata yalifanikiwa.
Uchunguzi wa matiti hufanyiwa kila mwaka mara tatu kwa wanawake kati ya umri wa miaka 50-70 nchini Uingereza.
Taasisi ya Madaktari wa Afya wa Uingereza (PHE) wamesema hawakuwa na habari zozote kuhusiana na madhara ya uchunguzi huo hadi mwezi Januari.
Siku ya Jumamosi, PHE ilisema itatoa usaidizi zaidi kwa wanawake ambao wamezidi umri wa miaka 72 ili waweze kufahamu manufaa ya kufanyiwa uchunguzi katika siku zao zijazo maishani.


Comments