Featured Post

TULIKOSEA WAPI AFRIKA KOMBE LA DUNIA 2018?



MOSCOW, RUSSIA
Kuondoka kwa Senegal imeifanya Afrika kuandikisha matokeo mabaya zaidi kwa miaka 36 tangu 1982- wakati Algeria na Cameroon waling'olewa hatua ya makundi, Afrika iliwakilishwa kwenye hatua za mchujo kila mara. Lawama kwa nani? bahati mbaya, VAR, au mipango dhaifu?

Kabla ya Urusi 2018, kulikuwa na matumaini Afrika ingeendeleza maonyesho yake Brazil 2014 wakati wawakilishi wake wawili - Nigeria na Algeria - walitua hatua za mchujo kwa mara ya kwanza.
Badala yake, bara zima litakuwa linajiuliza ni wapi chombo kilikwenda mrama kwani timu za Afrika zimeandikisha ushindi mechi tatu na kufungwa 10 katika vipute vyao 15 kwa jumla.
Mfalme wa Misri Mo Salah kujeruhiwa.
Tunisia iliadhibiwa mechi zake za kwanza Kundi G kabla ya kuifunga Panama waili hao wakifahamu kuelekea nyumbani. Ingawa Nigeria ilifunga Iceland, pia imeondoka Urusi kwa kumaliza wa tatu Kundi D.Shindano hili lilitarajiwa kuwa moja ambalo Misri ingebadili rekodi yake ya Kombe la Dunia kwa kuwa na kikosi kizuri chenye mmoja wa wachezaji bora duniani.
Kwa mtazamo wowote ule, Mohamed Salah alitawala kampeni ya kufuzu kwa Misri - kati ya mabao 10 ya Misri, Mo Salah alifunga saba na kuchangia mengine mawili yaliyowasaidia kushiriki Urusi.
Aliyechukua nafasi ya Salah - Marwan Mohsen - mwenye goli moja mechi 23 ya kimataifa - hakufanya lolote.
Hata iwapo Salah angekuwa hali nzuri ufanisi wa Misri unazidi kutiliwa shaka baad aya kurejea jukwaa la Kombe la Dunia baada ya miaka 28 - walifanya makosa mengi kwenye ulinzi.
Mabeki Ali Gabr na Ahmed Hegazi hawakuelewana vyema licha ya kunolewa na Hector Cuper - Kocha mwenye uzoefu idara ya Ulinzi.
Lakini wadakaji Mohamed El Shenawy na mkongwe Essam El Hadary, 45, aliyeandikisha historia kwa kuwa Kipa mwenye umri wa juu zaidi - walionyesha fomu nzuri katika mechi zao.
Hata hivyo, Misri haijatimiza mahitaji ya wengi kwani kulikuwa na matarajio chungu nzima kwa mabingwa hao mara saba wa Kombe la mataifa bora Afrika.

Simba wa Atlas wakosa kung'ata
Kampeini ya Morocco ilionekana kuzimwa mwanzoni walipofungua Kombe kwa kujifunga wenyewe dakika za mwisho dhidi ya Iran na kulazwa 1-0.
Kocha Herve Renard alitaja ngarambe hiyo "Fainali ya Kombe la Dunia", kwa timu yake licha ya kusubiriwa na Ureno na Uhispania. Uso wake baada ya mechi ulionyesha kuzidiwa na uchungu.
Kufuatia hapo, Morocco iliridhisha kwa pasi nzuri na kuelewana.
Safu butu ya ufungaji iliwalemea kwani hawakuweza kuzitumia nafasi zao mbele ya nyavu za wapinzani.
Mechi yao ya mwisho, Simba hao wa Atlas walikaribia kuilisha Uhispania kichapo chake cha kwanza mechi 23 lakini mabingwa hao wa 2010 waliwalizimisha sare ya 2-2 dakika za mwisho kama ilivyo ada dhidi ya timu za Afrika Kombe hili.
Morocco iliipa somo Uhispania licha ya kuwa na mastaa wanaopiga Real Madrid na Barcelona, na baadhi yao kuichezea Manchester City, Manchester United, Bayern Munich na Atletico Madrid.
"Ni timu bora sana iliyopoteza mechi mbili 1-0, na ilistahili zaidi," alisema kocha wa Uhispania Fernando Hierro baadaye.

Nigeria - Timu ya siku zijazo
Kufungwa dakika za mwisho na Argentina imeiumiza Nigeria na kuvutia shtuma dhidi yake kutoka nyumbani, wengi wakistaajabu kwa nini ngome yao haikupigwa jeki dakika za mwisho, lakini kampeini ya Super Eagles Urusi ni ya matumaini bora siku za usoni. Ilikuwa na wachezaji 18 wenye umri mdogo walioshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya Kwanza.
Licha ya kujumuishwa "Group of Death", walibakisha tu dakika nne kufuzu hatua ya mchujo kabla ya bao la Marcos Rojo.
Nigeria ilikosa kuwasumbua wapinzani wake kipindi cha kwanza.
Tofauti na makala ya awali ya Kombe la Dunia, Nigeria haikukumbwa na sakata za malipo ya wachezaji, mambo hayo yalishughulikiwa miezi kadhaa kabla ya Kombe la Dunia.

Tunisia bure
Tunisia haikuwa na nafasi ya kufuzu kutoka kundi ngumu lenye Uingereza na Ubelgiji.
Tunisia iliadhibiwa mechi zake za kwanza Kundi G kabla ya kuifunga Panama waili hao wakifahamu kuelekea nyumbani. Ingawa Nigeria ilifunga Iceland, pia imeondoka Urusi kwa kumaliza wa tatu Kundi D.
Tunisia maarufu Carthage Eagles walilazwa na Uingereza dakika za mwisho, Sawa na mataifa mengine ya Afrika, waliathirika kutokana na mabao ya kuchelewa na mipira ya juu.
Ingawa kutokuwepo kwa nyota wao Youssef Msakni, imetajwa kuwaumiza, mchango wake pia haungeweza kuwazuia walipobomolewa na Ubelgiji 5-2.
Mbali ya yote, Tunisia wameacha shindano wakiwa wafungaji bora wa Afrika - mabao matano kutoka mechi tatu.
Mnamo 1978 walikuwa timu ya kwanza ya Afrika kushinda mechi ya kwanza Kombe la Dunia.

Mhimili wa mwisho waanguka
Senegal, iliyoonekana Kombe la Dunia tangu ilipofika robo fainali 2002, ilisajili alama nne mechi mbili zake za kwanza Kundi H baada ya kuifunga Poland na kutoka sare na Japan.
Imekuwa ni pigo kubwa kwa bara hili na ni kurudi nyuma hatua moja kubwa kwani kuondoka kwa Senegal imeifanya Afrika kuandikisha matokeo mabaya zaidi kwa miaka 36 amesema Drogba.
Senegal ni wa kwanza kuchujwa Kombe la Dunia kutumia sheria za 'nidhamu' baada ya kulazwa na Colombia.
Simba hao wa Teranga walihitaji sare kufuzu wakichuana na Colombia, na beki wake Kalidou Koulibaly alinukuliwa kabla ya mechi ugani Samara akisema "bara zima lilikuwa nyuma ya Senegal".
Lakini mlinzi wa Colombia, Yerry Mina, aliitoa Senegal Kombe la Dunia kwa kupiga kichwa hadi kimiani dakika ya 74 na kuwavunja moyo mashabiki wa Senegal ugani Samara.

'Hatukustahili kufuzu'
"Hatujafuzu kwa kuwa hatukustahili kufuzu," alisema Aliou Cisse, kocha wa Senegal na kiungo mstaafu wa timu za Birmingham City na Portsmouth.
"Pointi za nidhamu ni mojawapo za sheria na hizi sheria zimewekwa kwenye mashindano kufuatwa. Tunafaa kuheshimu hilo.
"Tungechagua kutolewa kwa namna tofauti lakini ndiyo inavyofanya kazi na tulijua ndio taratibu.
"Nimevunjika moyo, kwa kizazi hiki, na kwa wachezaji hawa wanaolipigania taifa kila siku."

VAR iliifunga Afrika?
Mengi yanasemekana kuwa mtambo huo wa teknolojia Virtual Assistant Referee (VAR) imewaumiza wengi.
Lakini Misri na Mohamed Salah walipata Penalti dhidi ya Saudi Arabia kufuatia uamuzi wa VAR.
Hata hivyo, siyo Waafrika wote wameondoka Urusi.
Marefa kutoka Afrika wataliwakilisha bara hili kwa kusimamia mechi zinazoendelea za hatua zilizosalia.

Comments