- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Percival Salama aliyevaa koti jeupe.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa
Jimbo la Pangani (CCM)akizungumza wakati akifunga mashindano hayo
KIKOSI cha timu ya Ushirika FC wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya
kuanza mechi hiyo.
TIMU ya TOC FC juzi walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Ushirika FC mabao 4-3 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Kumba wilayani Pangani.
TOC ambao ni mabingwa walikabidhiwa kombe la Ubingwa,Medali na kitita cha sh.milioni 1 kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo (CCM).
Huku mshindi wa pili timu ya Ushirika FC walikabidhiwa kitita cha laki sita na medali wakati mshindi wa tatu akipata laki nne na medali kwenye tukio ambalo lilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.
Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kushindwa kutambiana ndani ya dakika tisini na hivyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndipo TOC walipofanikiwa kuibuka videdea.
Aidha zawadi nyengine zilitolewa ni timu yenye nidhamu ambapo Super Boys ya Sakura ilifanikiwa kuibuka na kukabidhiwa seti jezi moja huku nafasi ya mfungaji bora ikichukuliwea na Twaha Bungala ambaye alikabidhiwa kitita cha sh.50, 000 wakati mwamuzi bora akiibuka Bakari
Juma “Enye” ambaye alipata Jezi ya waamuzi seti moja.
Ligi hiyo ilishirikisha timu 20 ambazo zilichuana vilivyo ili kuwezakumpata bingwa ambaye atapata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mkoa wa Tanga inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Akizungumza mara kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema ataendelea kusapoti michezo kwenye Jimbo lake ili kuweza kuwasaidia vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao sambamba na kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia soka ili waweze kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.
"Ndugu zangu wana Pangani hususani vijana michezo ni ajira hivyo tucheze mpira kwa malengo ikiwemo kujituma kwani hakuna mafanikio yanayoweza kuja bila kucheza kwa kuonyesha uwezo wenu kwa lengo la kufika mbali kisoka"Alisema.
Comments
Post a Comment