Featured Post

TFF KUSHIRIKIANA NA LA LIGA KWA MIAKA MITATU



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka mitatu na Ligi Kuu ya nchini Hipania (La Liga) kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini Tanzania.

Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika juzi, Juni 18, 2018 makao makuu ya La Liga mjini Madrid, Hispania iliyohudhuliwa na Rais wa Laliga, Javier Tebas, Mkurugenz wa Maendeleo ya Kimataifa wa La Liga, Oscar Mayo, mwakilishi wa La Liga nchini Tanzania, Sami Hanane, Rais wa TFF Wallace Karia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, aliwaambia wanahabari jana kwamba, hiyo ni hatua nyingine kwa La Liga kujikita kwenye mpira wa miguu duniani na nia yake ya kushirikiana na taasisi mbalimbali za maeneo mbalimbali.
Ndimbo aliongeza kuwa, kupitia makubaliano hayo, La Liga itaiongoza TFF katika mchakato wa kutengeneza Ligi inayojitegemea.
Pamoja na hayo, LaLiga kwa kushirikiana na TFF watashirikiana kuandaa semina mbalimbali za ukocha, uongozi, uamuzi pamoja na semina za maendeleo ya soka la vijana na wanawake.


Comments