Featured Post

SERIKALI YATUMIA TEHAMA KUOKOA MABILIONI YA SHILINGI


1
 Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali akisisitiza jambo kwa  washirki wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa Epicor 10.2 jijini yanayoendelea jijini   Mbeya.
2
 Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka  PS3 Bw. Desderi  Wengaa akisisitiza jambo kwa Meneja wa Fedha  PS3  Perpetua Ngogo wakati wa mafunzo ya mfumo wa Epicor 10.2 leo jijini  Mbeya.
3
 Afisa Usimamizi  Fedha Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Mmaka Mwinjaka akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo wa EPICOR 10.2 leo jijini Mbeya kwa wahasibu na waweka hazina wa mikoa ya Njombe, Songwe, Katavi na Mbeya.
4
Sehemu ya awamu ya pili ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa EPICOR 10.2 yanayoendelea Jijini Mbeya ikiwa ni siku ya tatu ya mafunzo hayo.n(Picha  zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Frank Mvungi- MAELEZO, Mbeya
Serikali inaokoa takribani shilingi bilioni moja kutokana na kutumika kwa mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kuwachagua na kuwapingia shule wanafunzi   wanaojiunga na kidato cha tano katika shule zote hapa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Mbeya, Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais , Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick  Kitali amesema kuwa mfumo huo umejengwa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ukilenga kuondoa changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo malalamiko kutoka kwa wanafunzi wakati wa kupangiwa shule kulingana na ufaulu wao.
“Kwa sasa Serikali inatumia watumishi wasiozidi 20 wakati awali walitumika zaidi ya 300 katika kuwapangia wanafunzi shule za kidato cha tano hali ambayo imepelekea kupungua kwa gharama za uendeshaji wa mchakato huo kwa kiasi kikubwa.” Alisisitiza Kitali.
Akifafanua Bw. Kitali amesema kuwa mfumo huo tangu uanze kutumika umeondoa malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo wakati wa kuwapangia wanafunzi shule kwa kuwa kinachozingatiwa ni sifa za mwanafunzi husika na mchepuo anaotaka kuchukua anapojiunga kidato cha tano na si vinginevyo.
Aliongeza kuwa kutokana na kupungua  kwa gharama za uendeshaji wa mchakato huo sasa Serikali inatumia fedha zinazookolewa katika kuimrisha huduma za afya na elimu kwa  kuimarisha miundo mbinu ya sekta hizo.
Faida nyingine za mfumo huo ni pamoja na kupunguza muda wa uendeshaji wa mchakato huo kutoka miezi miwili au mitatu hadi mwezi mmoja na nusu kwa kutumia mfumo huo. 
Juhudi za Serikali hazijaishia katika mifumo ya PlanRep, FARRS, EPICOR 10.2, WISN, POA, TISS, bali zimeendelea zaidi katika sekta ya elimu ambapo mfumo wa kuchagua wanafunzi na kuwapangia shule kwa kidato cha tano (form five selection) kwa kuzingatia sifa za mwanafunzi husika  umechangia kwa kiwango kikubwa kuimarisha sekta ya elimu na kupunguza gharama za uendeshaji wa mchakato huo.

Comments