Featured Post

SANAMU YA 'AJABU' YA CRISTIANO RONALDO YABADILISHWA URENO



LISBON, URENO
SANAMU ya awali ya mchezaji nyota wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ilipataa umaarufu sana duniani, lakini kwa sifa ambazo walioiandaa hawakutarajia.

Ilizua mjadala kutokana na hali kwamba wengi wa mashabiki wa nyota huyo waliamini haikuwa inafanana na Ronaldo.
Wengi hata walidhani ilimfanya aonekana mwenye tabasamu la ajabu, au hata kama kibonzo.
Sanamu hiyo ilikuwa imewekwa kwenye kisiwa cha Madeira, alikozaliwa CR7.
Iliwekwa kwenye uwanja wa ndege wa kisiwa hicho ambao pia ulipewa jina lake baada ya Ureno kushinda Euro 2016.
Sasa, sanamu nyingine imewekwa na hiyo ya zamani kuondolewa.
Hii ya sasa inaonekana kidogo kukaribia kufanana na Ronaldo.
Lakini bado Cristiano hajasema anapendezwa na sanamu gani kati ya hizo mbili.
Aliwika akicheza dhidi ya Hispania katika mchezo wa Kombe la Dunia mwishoni mwa wiki ambapo aliwasaidia Ureno kutoka sare ya 3-3 kwa kufunga mabao yote matatu ya taifa lake.


Comments