Featured Post

SALAMU ZA MHE.UMMY MWALIMU , WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI WA SIKUKUU YA EID EL FITRI

Tukiwa tunaelekea kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri, napenda kuchukua fursa hii kuwatakia Waislam na Watanzania wote kwa ujumla Sikukuu njema ya Eid El Fitri. Ninawaomba wazazi, walezi na jamii tuitumie Sikukuu hii kukaa na watoto wetu kuwaasa ili kuwa na maadili mema na kuzingatia masomo yao.

Aidha , tutumie kipindi hiki kutafakari mambo mema ambayo Mungu ametutendea kwa mwaka huu. Kadhalika, ninawaasa watoto msherehekee  siku hii kwa uangalifu na utulivu mkubwa mkiwa na uangalizi wa wazazi na walezi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Ninawapenda watoto na ninawatakia Sikukuu njema yenye amani na furaha.
Eid El Fitri.

Comments