Featured Post

SADIO MANE ATAISAIDIA SENEGAL DHIDI YA POLAND LEO?

Sadio Mane
Haki miliki ya picha
Kocha wa timu ya taifa ya Senegal amesema winga wa Liverpool Sadio Mane ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani.

Senegal watacheza mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia tangu 2002 pale Mane, 26, na wenzake watakapokabiliana na Poland mjini Moscow baadaye leo Jumanne saa kumi na mbili jioni.
Kocha wao Aliou Cisse, alikuwa nahodha wa taifa hilo lilipofika robofainali mwaka 2002, ambapo walikuwa wamewashinda mabingwa watetezi Ufaransa katika hatua ya makundi.
"Mane ni wa kipekee na hawezi kulinganishwa na mchezaji mwingine yeyote wa Senegal. Anaweza kufanya mambo," Cisse, 42, amesema.
"Tayari ni mmoja miongoni mwa wachezaji bora zaidi - huweza kusema yeye hajafika hapo. Huchezea moja ya klabu kubwa zaidi, moja ya klabu bora zaidi Ulaya, na yeye ni nyota miongoni mwao.
"Ni wa kipekee sana kwa sababu hatabiriki, na hilo linamfanya kuwa mtu stadi."
Sadio ManeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMane amefunga mabao 14 katika mechi 49 alizochezea Senegal
Cisse, aliyekaa misimu minne katika Ligi ya Premia akiwa na Birmingham na Portsmouth, anasema Mane ametumia vyema sana nafasi yake tangu alipohamia Liverpool.
Mane amefunga mabao 33 katika misimu miwili tangu alipohamia Anfield kwa uhamisho wa £34m kutoka Southampton.
Aliou CisseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliou Cisse alichukua usukani kutoka kwa Alan Giresse kama kocha wa Senegal Machi 2015
"Licha ya mambo mengi ambayo yamemtendekea kwa miaka miwili iliyopita, hajabadilika - yeye bado ni mnyenyekevu kama alivyokuwa nilipokutana naye mara ya kwanza wakati wa michezo ya Olimpiki ya 2012," Cisse amesema.
"Senegal si Sadio Mane pekee, hata hivyo, ana timu nzuri iliyojengwa kumzunguka na nafikiri ni faida kwake kwamba sisi sote twamuunga mkono."
Cisse amesema ana imani kwamba Afrika siku moja itashinda Kombe la Dunia.
"Nina uhakika Senegal, Nigeria au timu nyingine itafanikiwa kushinda Kombe la Dunia sawa na Brazil au Ujerumani - hatuna cha kutuzuia kufanya hivyo," alisema.
"Unaweza kuwaona wachezaji wa Afrika wakicheza timu bora zaidi Ulaya - tunahitaji tu makocha zaidi wa Afrika."
'Timu ni muhimu kuliko wachezaji binafsi' - Diao
Salif DiaoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDiao alichezea Liverpool mechi 61 na kuwafundia mabao matatu. Alichezea Senegal mechi 39 na alikuwa nao Kombe la Dunia 2002
Salif Diao ambaye alichezea Liverpool na Senegal pia anaamini kwamba Mane na wachezaji wenzake wanaweza kufanikiwa Urusi iwapo watathamini timu zaidi ya nafsi zao.
"Kikosi kina uzoefu na wachezaji wa kutosha wenye vipaji tofauti na kikosi cha 2002, lakini pengine kikosi cha 2002 kilikuwa na ukomavu zaidi," amesema kiungo wa kati huyo wa zamani.
"Umoja ni nguvu. Kufikiria kuhusu timu ya taifa na bendera na familia nyumbani.
"Timu za Afrika zikienda Kombe la Dunia huwakilisha nchi zao na Afrika pia, hivyo shinikizo huwa hata zaidi.
"Huwezi kufanya haya yote ukiwa peke yako, kwa hivyo unahitaji kufikiria kuhusu timu. Timu ni zaidi ya wachezaji binafsi."

Comments