Featured Post

MALI YA FAMILIA YA MPINZANI WA KAGAME YAUZWA RWANDA


KIGALI, RWANDA
MAMLAKA nchini Rwanda zimeuza mali ya familia ya mwanasiasa aliye kizuizini ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame.

Diane Rwigara alizuiwa kuwania urais mwaka 2017 na baadaye kakamatwa kwa madai ya udanganyifu na kuchochea mapinduzi ya serikali.
Halmashauri ya kukusanya ushuru nchini Rwanda iliuza mashine kutoka kwa biashara ya familia ya tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika hatua ya kulipia kodi, familia hiyo inaripotiwa kudaiwa zaidi ya dola milioni 7.
Familia hiyo inasema hatua hiyo ya kuuza mali na mashtaka dhidi yake imechochewa kisiasa.
Mauzo ya awali ya biashara za familia ya Rwigara ya tumbaku yalileta dola milioni 595.
Rwigara ni mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati alipoamua kuwania urais.
Hakufaulu kuwania na alipigwa marufuku baada ya uchunguzi kubaini kuwa Rwigara alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono kugombea kwake.
Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba 2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali.
Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapinduzi ya serikali.
Rais Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka 2017 kwa asilimia 98.63 ya kura.
Amesifiwa kwa kuleta mafanikio ya kiuchumi nchini humo tangu yafanyike mauaji ya kimbari mwaka 1994.


Comments