Featured Post

KOMBE LA DUNIA: MASHABIKI WA MEXICO WALISABABISHA TETEMEKO LA ARDHI WAKISHEREHEKEA BAO LA USHINDI?

Soccer Football - FIFA World Cup - Group F - Germany v Mexico - Mexico City, Mexico - June 17, 2018 - Mexican fans celebrate at the Angel of Independence monument.
Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionShangwe iliyosababisha tetemeko la ardhi
Mashabiki wa kandanda wa Mexico hawakuweza kuzuia furaha yao wakati Hirving Lozano alifunga bao dhidi ya Ujerumani wakati wa mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.

Lakini ni kweli kuwa shangwe hizo zao zilisababisha tetemeko la ardhi jinsi baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti?
Ujumbe wa twitter kutoka taasisi ya jiolojia umesema hivyo.
Ujumbe huo kutoka taasisi inayochunguza mitetemeko ya ardhi unasema, "Tetemeko la ardhi mjini Mexico kutokana na shangwe kufuatia bao la timu ya Mexico dhidi ya Ujerumani wakati wa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi."

Kipi haswa kilitokea?

Taasisi hiyo inasema kuwa vifaa vyake viwili vya kupima mitetemo ya ardhi vilitambua kutetemeka kwa ardhi mara tu baada ya goli la ushindi kufungwa.
Soccer Football - World Cup - Group F - Germany vs Mexico - Luzhniki Stadium, Moscow, Russia - June 17, 2018 Mexico"s Hirving Lozano celebrates scoring their first goal REUTERS/Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionHirving Lozano hakuamini alifunga bao la ushindi
Inasema kuwa ni vifaa vyenye uwezo wa juu wa kutambua vilivyokuwa karibu na mashabiki vinaweza kutambua shughuli kama hiyo.
Moja ya maeneo ambapo masahabiki walikusanyika haliko mbali sana na moja ya vifaa hivyo zilivyonakili tetemeko hilo la ardhi.

Mashabiki walishangilia kwa njia gani?

Jionee mwenyewe:
Mexico"s fans celebrate their team winning the FIFA World Cup 2018 group F preliminary round soccer match between Germany and Mexico, in Mexico City, Mexico, 17 June 2018Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMashabiki wakiruka kwa shangwe
Soccer Football - FIFA World Cup - Group F - Germany v Mexico - Mexico City, Mexico - June 17, 2018 - Mexican fans celebrate at the Zocalo square.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaelfu walikusanyika huko Zocalo bustani kuu mjini Mexico
Soccer Football - FIFA World Cup - Group F - Germany v Mexico - Mexico City, Mexico - June 17, 2018 - Mexican fans celebrate at the Angel of Independence monumentHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMashabiki
CHANZO: BBC

Comments