Featured Post

KOMBE LA DUNIA 2018: MAMBO MUHIMU KUHUSU WALIOFUZU, NA WALIOTUPWA NJE



MOSCOW, RUSSIA
MICHUANO ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi inazidi kupamba moto ambapo sasa tayari zimefahamika timu ambazo zimefika hatua ya muondoano, yaani raundi ya 16 bora.

Kumekuwa na matokeo ya kushangaza ikiwemo kuondolewa kwa mabingwa watetezi Ujerumani na pia kuondolewa kwa mataifa yote ya Afrika yaliyokuwa yanashiriki michuano hiyo.
Senegal waliondolewa kutokana na kuwa na kadi nyingi za manjano baada ya kutoshana kwa alama na mabao na Japan.
Kwa nini Ubelgiji huenda ikashinda Kombe la Dunia
Ubelgiji na England nao wakicheza mechi yao ya mwisho baada ya kufuzu, walionekana kila mmoja kutotaka kushinda mechi hiyo kwa kuhofia uwezekano wa kukutana na Brazil katika hatua ya robofainali. Mechi hiyo ilimalizika kwa ushindi wa Ubelgiji wa 1-0.
Hapa ni maelezo zaidi kuhusu mataifa yaliyofuzu hatua ya 16 bora, na yale yaliyoondolewa.

WALIOFIKA 16 BORA
Urusi (mwenyeji)

Ustadi: Vijana hao chini ya Stanislav Cherchesov wamekuwa timu ya nne kutoka Urusi kucheza Kombe la Dunia. Mara ya kwanza walishiriki Marekani '94 - ingawa kama Muungano wa Usovieti na walimaliza nambari nne mwaka 1966.
Walianza kwa ushindi wa kushangaza wa 5-0 dhidi ya Saudi Arabia na kisha wakawafanikiwa kuwalaza Misri. Hata hivyo walicharazwa na Uruguay.

Ndio wenyeji
Kikosi chote cha wachezaji wa Urusi waliocheza Kombe la Mabara mwaka 2017 Urusi walikuwa huchezea klabu za nyumbani
Mchezaji nyota: Kipa wao mkongwe Igor Akinfeev amechezea nchi hiyo zaidi ya mechi 100 na uzoefu wake ni muhimu kwa kikosi hicho.
Akinfeev, 31, amechezea CSKA Moscow maisha yake yote ya uchezaji soka ya kulipwa. Huenda akawa nahodha wa Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja.
Mkufunzi? Cherchesov ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Muungano wa Usovieti na Urusi. Lengo lake ni kuwafikisha nusu fainali.

Ubelgiji

Ustadi: Hawakufuzu kwa michuano miwili iliyotangulia lakini Brazil 2014 walifika robofainali, ambapo waliondolewa na Argentina. Mwaka 1986 walimaliza wa nne.
Wamemaliza hatua ya makundi wakiwa na alama tisa ambapo walifanikiwa kuwalaza Panama, Tunisia na England. Wamepangiwa kukutana na Japan hatua ya 16 bora.
Mchezaji nyota: Eden Hazard ambaye pia ndiye nahodha
Wachezaji Ligi ya Premia: Michy Batshuayi, Thibaut Courtois, Eden Hazard (wote wa Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool), Toby Alderweireld, Moussa Dembele, Jan Vertonghen, (wote wa Tottenham), Kevin de Bruyne, Vincent Kompany (wa Manchester City), Marouane Fellaini, Romelu Lukaku (wa Manchester United), Steven Defour (Burnley), Nacer Chadli (West Brom), Kevin Mirallas (Everton), Christian Benteke (Crystal Palace), Divock Origi (Wolfsburg, kwa mkopo kutoka Liverpool), Christian Kabasele (Watford).
Mkufunzi? Roberto Martinez aliyesaidia Wigan kushinda Kombe la FA mwaka 2013

England

Ustadi: Tangu waliposhinda Kombe la Dunia 1966, England wamefika nusu fainali mara moja pekee - mwaka 1990, ambapo walimaliza wa nne. Miaka minne iliyopita, waliondolewa hatua ya makundi. Ilikuwa mara yao ya mwisho kukosa kupita hatua ya makundi tangu 1958.
Urusi, walifanikiwa kuwashinda Panama na Tunisia lakini wakawashindwa na Ubelgiji mechi ya mwisho, hatua iliyoonekana kama ya kutafakari michuano itakayofuata ambapo iwapo wangeshinda kungekuwa na uwezekano wa kukutana na Brazil hatua ya robofainali.
Watakutana na Colombia hatua ya 16 bora.
Mchezaji nyota: Harry Kane amefunga magoli 13 akichezea klabu ya taifa Septemba na kwa sasa ni miongoni mwa washambuliaji wanaofunga mabao sana. Mwaka 2017 amefunga mabao 27 ambapo amepitwa tu na Lionel Messi, anayemzidi kwa magoli tisa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Kikosi chote cha England hucheza EPL
Mkufunzi? Gareth Southgate anaongoza timu kwa mara ya kwanza katika michuano mikubwa.

Ufaransa

Ustadi: Ufaransa walishinda Kombe la Dunia walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo 1998 na walifika fainali miaka minane iliyofuata ambapo walishindwa na Italia. Walifika robofainali Brazil 2014. Walimaliza wa pili Euro 2016.
Walionekana kutatizika katika baadhi ya mechi hatua ya makundi. Waakutana na Argentina hatua ya 16 bora.
Mchezaji nyota: Antoine Griezmann. Mshambuliaji huyu wa Atletico Madrid alikuwa mfungaji bora wa Ufaransa ambapo aliwafungia mabao sita na kuwawezesha kufika fainali Euro 2016.
Alifunga bao la pili kuwawezesha kulaza Belarus 2-1 na kufuzu 10 Oktoba.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Laurent Koscielny, Alexandre Lacazette and Olivier Giroud (wote wa Arsenal), Tiemoue Bakayoko na N'Golo Kante (wote wawili Chelsea), Yohan Cabaye (Crystal Palace), Eliaquim Mangala na Benjamin Mendy (wote wawili Manchester City), Anthony Martial na Paul Pogba (wote wawili Manchester United), Kurt Zouma (Stoke, kwa mkopo kutoka Chelsea), Hugo Lloris na Moussa Sissoko (wote wawili Tottenham).
Mkufunzi wao? Didier Deschamps alichezea Ufaransa mechi 103 na aliwasaidia kushinda Kombe la Dunia 1998 na ubingwa wa Ulaya 2000. Amekuwa mkufunzi wao tangu Julai 2012. Aliwafikisha fainali Euro 2016, aambapo walilazwa na Ureno 1-0.

Ureno

Ustadi: Ndio mabingwa wa sasa wa Ulaya, ambapo walilaza Ufaransa 1-0 fainali. Ufanisi wao zaidi Kombe la Dunia ulikuwa walipomaliza wa tatu mwaka 1996. Walifika pia nusufainali 2006 lakini Brazil 2014 waliondolewa hatua ya makundi.
Mwaka huu katika Kundi B walimaliza wa pili nyuma ya Uhispania, ambayo walikuwa wamtoka sare ya 3-3 nao siku ya kwanza ya mechi, mabao yao yote yakifungwa na Cristiano Ronaldo.
Mchezaji tegemeo: Nani mwingine? Cristiano Ronaldo. Ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne, na amechezea taifa lake mechi nyingi zaidi. Aidha, anashikilia rekodi ya ufungaji timu yake ya taifa. Ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne.
Alifunga mabao 15 akichezea Ureno mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Wachezaji Ligi ya Premia: Adrien Silva (Leicester), Bernardo Silva (Manchester City), Cedric Soares (Southampton), Renato Sanches (Swansea, kwa mkopo kutoka Bayern Munich), Jose Fonte (West Ham).
Mchezaji wa Championship: Nelson Oliveira (Norwich)
Mchezaji Ligi Kuu ya Scotland: Bruno Alves (Rangers)
Meneja? Fernando Santos alichukua hatamu Septemba 2014 na kuwaongoza kushinda Euro mara ya kwanza 2016. Alikuwa pia meneja wa Ugiriki Kombe la Dunia 2014 ambapo aliwafikisha hatua ya 16 bora lakini wakashindwa na Costa Rica.

Uhispania

Ustadi: Walikuwa namba moja duniani kuanzia 2008 hadi 2013. Walikuwa mabingwa wa dunia 2010 na mabingwa wa Ulaya 2008 na 2012.
Uhispania walimaliza kileleni Kundi B wakiwa na alama sawa na Ureno, lakini mbele kwa kufunga mabao mengi, baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare mara mbili. Waliwashinda Iran lakini wakatoka sare ya 3-3 na Ureno na 2-2 na Morocco.
Mchezaji nyota: Kiungo wa kati mshambululiaji wa Real Madrid Isco amekuwa kwenye fomu nzuri sana mechi za kufuzu. Amefunga mabao sita mechi saba za karibuni zaidi za Uhispania. Amefunga mabao saba mechi 23 za kimataifa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Juan Mata (Manchester United), Nacho Monreal (Arsenal), Alvaro Morata (Chelsea), David de Gea (Manchester United), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Ander Herrera (Manchester United), Pedro (Chelsea), David Silva (Manchester City).
Mkufunzi? Julen Lopetegui aliteuliwa Julai 2016 na hajashindwa mechi 13 ambazo amewaongoza.

Brazil

Ustadi: Washindi mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002, Brazil walilazwa 7-1 hatua ya makundi na Ujerumamni mwaka 2014.
Mwaka huu Urusi walifika hatua ya 16 bora kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Costa Rica na Serbia. Walikuwa wametoka sare ya 1-1 na Uswizi mechi yao ya kwanza.
Waakutana na Mexico hatua ya 16 bora.
Mchezaji nyota: Neymar. Alinunuliwa £200m na Paris St-Germain na amekuwa akifunga bao na kusaidia kila mechi tangu wakati huo. Pele amesema Neymar, 25, ndiye mchezaji bora zaidi wa taifa hilo na anaamini atashinda Ballon d'Or.
Wachezaji Ligi ya Premia: Ederson, Fernandinho, Gabriel Jesus (wote wa Manchester City), Philippe Coutinho, Roberto Firmino (wa Liverpool), Willian (Chelsea).
Mkufunzi? Tite alichukua nafasi ya Dunga wakiwa nafasi ya sita, theluthi ya mechi za kufuzu zikiwa zimechezwa. Lakini mkufunzi huyo wa zamani wa Corinthians, 56, amewasaidia kuwa alama 11 mbele ya Colombia kileleni zikiwa zimesalia mechi tatu.

Argentina

Ustadi: Argentina wameshinda Kombe la Dunia mara mbili - 1978 na 1986 - na wamemaliza wa pili mara tatu mwaka 1930, 1990 na nchini Brazil 2014, ambapo walishindwa 1-0 na Ujerumani fainali.
Walianza Urusi kwa wasiwasi kwa kutoka sare ya 1-1 na Iceland na wakachapwa 3-0 na Croatia.
Hata hivyo, walifanikiwa kuwashinda Nigeria 2-1 na kumaliza wa pili kwenye Kundi D nyuma ya Croatia.
Mchezaji nyota: Lionel Messi. Messi, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne na alifunga hat-trick mechi za kufuzu dhidi ya Ecuador kuwafikisha Argentina michuano hiyo ya Urusi.
Wachezaji wa ligi ya premia: Sergio Aguero na Nicolas Otamendi (wote wawili Manchester City), Sergio Romero (Manchester United), Manuel Lanzini (West Ham).
Meneja: Meneja wa zamani wa Chile Jorge Sampaoli, aliyeongoza Chile Copa America mwaka 2015, aliteuliwa meneja wa Argentina Mei 2017. Alifanikiwa kibarua chake cha kwanza, kuhakikisha wanafuzu kwa Kombe la Dunia.

Colombia

Ustadi: Colombia walifanikiwa zaidi Brazil 2014 walipofika robofainali lakini wakashindwa 2-1 na Brazil.
Mwaka huu, walianza kwa kushindwa 2-1 na Japan lakini wakawashinda Poland 3-0 na kisha wakawalaza Senegal 1-0 na kumaliza kileleni Kundi H wakiwa na alama 6.
Mchezaji nyota: James Rodriguez. Mshambuliaji kiungo wa kati aliye Bayern Munich kwa mkopo kutoka Real Madrid, alishinda tuzo ya Kiatu cha Dhahabu kwa ufungaji mabao mengi zaidi Kombe la Dunia 2014. Alifunga mabao sita michuano hiyo.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: David Ospina (Arsenal), Jose Izquierdo (Brighton), Davinson Sanchez (Tottenham)
Meneja: Jose Pekerman ameongoza Colombia tangu 2012 na alishinda tuzo ya Kocha wa Mwaka Amerika Kusini mara tatu tangu wakati huo.

Uruguay

Ustadi: Uruguay walishinda Kombe la Dunia mara ya kwanza 1930 kisha tena 1950 lakini walifika hatua ya 16 bora pekee Brazil 2014. Walianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri kisha wakawalaza Saudi Arabia 1-0 na hatimaye kuwachapa wenyeji 3-0 25 Juni.
Watakutana na Ureno hatua ya 16 bora.
Mchezaji nyota: Luis Suarez. Nyota huyu wa Barcelona ndiye mfungaji mabao bora zaidi wa uruguay na alifunga mawili mechi yao ya mwisho ya kufuzu dhidi ya Bolivia.
Mchezaji wa Championship: Abel Hernandez (Hull)
Meneja: Oscar Tabarez amekuwa kwenye usukani Uruguay tangu 2006 na kuwaongoza kushinda Copa America mwaka 2011.

Mexico

Ustadi: Mexico wamefika hatua ya muondoano kila michuano ya Kombe la Dunia sita iliyochezwa. Walifika robofainali wakiwa wenyeji mwaka 1986. Walianza Urusi kwa kuwashangaza mabingwa watetezi Ujerumani kwa kuwachapa 1-0 na kisha wakawashinda Korea Kusini 2-1.
Hata hivyo, walichapwa 3-0 na Sweden waliomaliza wa kwanza kwenye Kundi F wakiwa na alama 6. Mexico walikuwa pia na alama sita lakini tofauti ya mabao ya -1 ukilinganisha na Sweden waliokuwa na +3.
Mchezaji nyota: Hirving Lozano amefunga mabao matatu mechi tatu kati aihame Pachuca na kwenda PSV Eindhoven majira ya joto.
Lozano, 22, ameanza kuwa nyota timu ya taifa ambapo alifunga bao la ushindi dhidi ya Panama.
Alimpendeza hata Diego Maradona akicheza mechi yake ya kwanza Eredivisie.
Wachezaji Ligi ya Premia: Javier Hernandez (West Ham).
Mkufunzi? Meneja msaidizi wa zamani wa Manchester City, Juan Carlos Osorio, ndiye anayewaongoza. Alikuwa awali amepigwa marufuku mechi sita na Fifa kwa kumtusi mwamuzi Kombe la Mabara. Ni raia wa Colombia aliyesomea stashahada ya sayansi na soka kutoka chuo kikuu cha John Moores cha Liverpool.

Japan

Ustadi: Wameshiriki tangu 1998, Japan na walikuwa wamepita hatua ya makundi mara mbili awali, ikiwa ni pamoja na 2002 walipokuwa wenyeji wenza na Korea Kusini. Mwaka huu, walifanikiwa kufuzu wakiwa wa pili nyuma ya Colombia Kundi H baada ya kuwashinda Colombia 2-1 mechi ya kwanza na kutoka sare ya 2-2 na Senegal ingawa walichapwa 1-0 na Poland siku ya mwisho.
Mchezaji nyota: Keisuke Honda, Shinji Kagawa na nyota wa Leicester Shinji Okazaki wamekuwa wachezaji nyota. Lakini kuna kinda wa Arsenal Takuma Asano ambaye tayari amefungia cnhi yake mechi tatu na alisaidia Stuttgart kupanda daraja Bundesliga msimu uliopita akiwa kwa mkono kutoka kwa Gunners. Wenger amemweleza kama mshambuliaji mwenye kipaji na mwenye matumaini siku za usoni.
Wachezaji Ligi ya Premia: Maya Yoshida (Southampton), Shinji Okazaki (Leicester City), Takuma Asano (Stuttgart, kwa mkopo kutoka Arsenal).
Mkufunzi? Vahid Halilhodzic, ingawa huenda akaondoka kwani kuna fununu kuhusu mzozo kwenye timu.
Aliongoza Algeria kufika hatua ya muondoano mara ya kwanza 2014.
Ni mchezaji wa zamani wa Yugoslavia ambaye amewahi kuwa mkufunzi wa Paris St-Germain, Dinamo Zagreb na Ivory Coast.

WALIOTUPWA NJE
Morocco
Ustadi: Morocco walikuwa wanacheza mara yao ya kwanza katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia katika kipindi cha miaka 20. Mwaka 1998 nchini Ufaransa, walishinda mechi moja, wakatoka sare moja na kushindwa mechi moja na kushinda kusonga kutoka hatua ya makundi.
Walifaulu kusonga hatua ya makundi mara moja pekee katika fainali nne walizoshiriki, mwaka 1986 nchini Mexico walipofika hatua ya 16 bora. Waliondolewa na Ujerumani Magharibi kwa kulazwa 1-0, ambao mwishowe walimaliza wa pili.
Mchezaji tegemeo: Beki wao Medhi Benatia hajakuwa akianza sana mechi katika klabu yake ya Juventus msimu uliomalizika majuzi (zaidi kutokana na ushindani mkubwa) lakini anathaminiwa sana na mabingwa hao wa Italia.
Alinunuliwa na Juve kwa mkataba wa kudumu mwaka jana kutoka Bayern Munich baada ya kufana akiwa nao kwa mkopo. Mchezaji huyo wa miaka 30 ndiye nahodha wa Morocco na amewachezea mechi 52 za kimataifa, tano katika mechi za kfuuzu kwa Kombe la Dunia 2018 ambapo hawakufungwa. Aidha, alifunga katika mechi waliyoshinda 2-0 dhidi ya Ivory Coast na kujithibitishia nafasi ya kucheza Urusi.
Katika michuano ya Urusi walipata alama moja pekee kwa kutoka sare na Uhispania.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Sofiane Boufal (Southampton)
Wachezaji wa Championship: Romain Saiss (Wolves)
Mkufunzi wao? Mfaransa Herve Renard amekuwa akihama kutoka taifa moja hadi jingine tangu alipostaafu uchezaji mwaka 1998. Alianza kwa kuwa mkufunzi wa Cambridge United, aliojiunga nao 2004 lakini akaondoka baada ya kuwaongoza mechi 25 na kuwaacha wakiwa nafasi ya pili kutoka mwisho League Two. Tangu wakati huo, ameshinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, akiwa na Zambia 2012 na akiwa na Ivory Coast 2015. Baada ya kutofanikiwa akiwa mkufunzi wa klabu ya Lille ya Ufaransa, alichukua mikoba Morocco mwaka 2016.

Senegal
Ustadi: Hii ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kwa Senegal kufuzu kwa Kombe la Dunia tangu 2002, na mara yao ya pili katika historia. Mwaka 2002, waliwasisimua wengi kwa kufika robo fainali, ambapo walilazwa 1-0 na Uturuki.
Mwaka huu, walicheza vyema kwa kuwalaza Poland 2-1 lakini walitoka sare na Japan 2-2 na mechi ya mwisho wakachapwa 1-0 na Colombia.
Mchezaji nyota: Sadio Mane ndiye mchezaji nyota zaidi katika kikosi hicho na pia mwenye uzoefu mwingi. Amechezea timu ya taifa mechi 48 na kuwafungia mabao 14 tangu alipoanza kuwachezea 2012. Mwaka 2015, aliweka rekodi ya kufunga hat-trick ya haraka zaidi Ligi ya Premia kwa kutumia muda wa sekunde 176 pekee wakati wa mechi ya Southampton na Aston Villa ambapo waliwachapa Villa 6-1.
Alipohamia Liverpool mwaka 2016, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Afrika kuuzwa bei ya juu zaidi katika historia kufikia wakati huo, uhamisho wake ukigharimu £34m.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Cheikhou Kouyate (West Ham), Diafra Sakho (West Ham), Idrissa Gueye (Everton), Sadio Mane (Liverpool).
Wachezaji wa Championship: Alfred N'Diaye (Wolves), Cheikh N'Doye (Birmingham City),
Mkufunzi wao ni nani? Aliou Cisse ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal na klabu za Pompey na Birmingham City. Mkufunzi huyo wa miaka 41 mwanzoni alikuwa kocha wa muda baada ya kufutwa kwa Amara Traore mwaka 2012 kwa kipindi kifupi.
Kisha, alipewa kazi ya kuwa mkufunzi wa timu ya Senegal ya vijana wa chini ya miaka 23 mwaka 2012-2013 kabla ya kupewa kazi ya kocha wa timu kuu ya taifa kwa mkataba wa kudumu.

Tunisia
Ustadi: Mwaka huu ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Tunisia kuwa katika fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Wakati huo hawakufanikiwa kujitoa hatua ya makundi.
Katika fainali tatu walizokuwa wamecheza awali - 1978, 1998 na 2002 - pia hawakufika hatua ya muondoano.
Mchezaji nyota: Beki wao wa kati Aymen Abdennour ana uzoefu mkubwa na kipaji na ni ngome katika safu ya ulinzi ya Tunisia. Amekuwa katika klabu ya Marseille ya Ufaransa kwa mkopo kutoka Valencia ya Uhispania.
Alikuwa amechezea taifa mechi 57 na kuwafungia mara mbili kufikia wakati wao wa kufuzu.
Awali alikuwa amehusishwa na kuhamia Ligi ya Premia klabu za Everton na Chelsea, na majuzi mchezaji huyo wa miaka 28 alidaiwa kutafutwa na Watford.
Urusi, walishindwa na Ubelgiji na England lakini wakafanikiwa kuwalaza Panama 2-1 na kuepuka aibu ya kumaliza wakiwa wa mwisho Kundi G.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja
Wachezaji wa Championship: Wahbi Khazri (Sunderland, yupo kwa mkopo Rennes)
Mkufunzi wao ni nani? Nabil Maaloul anahudumu kama kocha wa Tunisia kwa kipindi cha pili.
Kipindi cha kwanza aliwaongoza mechi saba pekee mwaka 2013 ambapo alijiuzulu baada ya kushindwa kuwawezesha kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014.
Alirejea Aprili 2017, baada ya kufanya kazi labu ya El Jaish SC nchini Qatar na kuhudumu katika timu ya taifa ya Kuwait. Kabla ya hapo, alikuwa msaidizi wa kocha Roger Lemerre mwaka 2004 Tunisia waliposhinda Kombe la Mataifa ya Afrika na aliwaongoza ES Tunis kushinda vikombe vitatu vya nyumbani mwaka 2011. Alichezea Tunisia mechi 74 za kimataifa wakati wa uchezaji wake kama kiungo wa kati miaka ya 1980 na 1990 na aliwawakilisha katika Michezo ya Olimpiki ya Seoul mwaka 1988.

Ujerumani
Ustadi: Ni mabingwa watetezi, wameshinda Kombe la Dunia mara nne na walikuwa wameorodheshwa kuwa timu bora zaidi duniani na Fifa kufikia wakati wa michuano.
Hata hivyo, walishindwa na Mexico mechi yao ya kwanza ingawa walifanikiwa kuwashinda Sweden mechi ya pili kupitia bao la dakika za mwisho la Toni Kroos.
Walichapwa 2-0 na Korea Kusini mechi yao ya mwisho na kuyaaga mashindano.
Mchezaji nyota: Toni Kroos. Kando na Thomas Muller na Mesut Ozil, kiungo huyo wa Real Madrid ndiye mchezaji mzoefu zaidi kwenye kikosi.
Alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2014, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili, La Liga mara moja na Kombe la Dunia la Klabu mara mbili.
Wachezaji Ligi ya Premia: Shkodran Mustafi (Arsenal), Antonio Rudiger (Chelsea), Emre Can (Liverpool), Ilkay Gundogan (Manchester City), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Manchester City).
Meneja? Joachim Low. Alikuwa mkufunzi msaidizi wa Jurgen Klinsmann 2004 hadi 2006, alipochukua hatamu. Aliwaongoza kushinda Kombe la Dunia mwaka 2014 na pia alishinda Kombe la Mabara mwaka huu. Hata hivyo hajashinda Euro. Walimaliza wa pili mwaka 2008 na nafasi ya tatu 2012.

Iceland
Ustadi: Iceland walikuwa wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa baada ya ushindi wao dhidi ya Kosovo tarehe 9 Oktoba kuwahakikishia nafasi.
Wamekuwa wakifanikiwa sana karibuni. Walifika Euro 2016, na kulaza England raundi ya pili kabla ya kulazwa 5-2 na wenyeji katika robofainali.
Walifanikiwa kutoka sare ya 1-1 na Argentina mechi ya kwanza lakini baadaye wakalazwa na Croatia na Nigeria na kumaliza wa mwisho Kundi D.
Mchezaji muhimu: Ni vigumu kumtazama mchezaji mwingine ila Gylfi Sigurdsson wa Everton. Mchezaji huyo wa miaka 28 aliwafungia bao la kwanza dhidi ya Kosovo na ni mshambuliaji hatari sana, hasa kwa makombora ya mbali.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Gylfi Sigurdsson (Everton), Johann Berg Gudmundsson (Burnley).
Wachezaji Championship: Birkir Bjarnason (Aston Villa), Horour Bjorgvin Magnusson (Bristol City), Jon Dadi Bodvarsson (Reading).
Mkufunzi? Heimir Hallgrimsson, 50, ni daktari wa meno aliyekuwa anasimamia timu hiyo kwa pamoja na Lars Largerback wa Sweden wakati wa michuano ya ubingwa Ulaya nchini Ufaransa. Hallgrimsson alichukua usukani kamili baada ya Euro 2016 na kuwasaidia kufana mechi za kufuzu.

Poland
Ustadi: Poland hawajawahi kushinda Kombe la Dunia lakini mwaka huu wanaamini wana kikosi stadi zaidi. Ufanisi wao awali ulikuwa kumaliza nafasi ya tatu, mwaka 1974 na 1982.
Waliondoka kutoka Kundi H na alama tatu baada ya kulazwa na Senegal na Colombia lakini wakafanikiwa kuwalaza Japan 1-0 siku ya mwisho.
Mchezaji nyota: Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski alikuwa amefunga mabao 16 katika mechi tisa za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na Poland. Anashikilia nafasi ya tatu kufunga mabao mengi historia ya Poland. Ndiye nahodha na amefunga mabao 51 mechi 91 za kimataifa.
Wachezaji Ligi ya Premia: Lukasz Fabianski (Swansea), Grzegorz Krychowiak (West Bromwich Albion), Kamil Grosicki (Hull City)
Wachezaji Championship: Pawel Wszolek (Queens Park Rangers)
Mkufunzi? Adam Nawalka amewaongoza tangu Novemba 2013 mechi 39. Mkataba wake unafika mwisho Desemba lakini aliwafikisha robo fainali Euro 2016, miaka miwili baada yao kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2014.

Serbia
Ustadi: Mwaka huu ilikuwa mara ya 12 kwa Serbia kucheza Kombe la Dunia. Hawakufanikiwa kupita hatua ya makundi mwaka 2006 na 2010, na mwaka huu vile vile.
Walimzaliza nafasi ya tatu Kundi E wakiwa na alama tatu zilizotokana na ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Costa Rica.
Mchezaji nyota: Branislav Ivanovic anakaribia kuchezea taifa lake mechi 100 na ni mchezaji muhimu sana kwao. Ndiye nahodha na kiongozi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Nemanja Matic (Manchester United), Aleksandar Mitrovic (Newcastle), Lazar Markovic (Liverpool), Dusan Tadic (Southampton).
Mkufunzi? Slavoljub Muslin, aliyeteuliwa Mei 2016, ni mkufunzi ambaye amesafiri kwingi. Anafanya kazi ya kuwa mkufunzi wa timu ya taifa mara ya kwanza na hajawahi kuongoza timu katika michuano mikubwa. Lakini amefanikiwa ligini Bulgaria.

AMERIKA KASKAZINI NA KATI na CARIBBEAN

Costa Rica
Ustadi: Urusi 2018 ilikuwa mara ya tano kwa Los Ticos kucheza michuano ya Kombe la Dunia.
Brazil walimaliza kileleni mwa kundi lililokuwa na Uruguay, Italia, na England. Waliondolewa robofainali kwa mikwaju ya penalti na Uholanzi.
Katika Kundi E walianza kwa kushindwa 1-0 na Serbia na ya pili wakachapwa 2-0 na Brazil.
Walijiondolea aibu kidogo kwa kutoka sare ya 2-2 na Uswizi ingawa bado walimaliza wa mwisho kwenye kundi.
Mchezaji nyota: Beki wa Bologna Giancarlo Gonzalez alikuwa kwenye kikosi bora cha wachanganuzi wa BBC wa Kombe la Dunia mwaka 2014 lakini ufanisi wa sasa wa Costa Rica unatokana na kipa Keylor Navas, 30. Alicheza vyema sana 2014 kiasi cha Real Madrid kumnunua na sasa ndiye kipa wao nambari wani.
Ameshinda La Liga na makombe mawili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Wachezaji Ligi ya Premia: Joel Campbell wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Real Betis.
Mkufunzi? Oscar Ramirez ambaye alikuwa mchezaji Costa Rica walipocheza Kombe la Dunia mara ya kwanza 1990. Alichukua usukani 2015 baada ya Paulo Wanchope kujiuzulu.

Panama
Ustadi: Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kufika Kombe la Dunia baada ya ushindi wao dhidi ya Costa Rica mechi yao ya mwisho. Walimaliza wa pili Kombe la Dhahabu la Concacaf mwaka 2013. Lakini Urusi mambo hayakuwaendea vyema. Walianza kwa kuchapwa 3-0 an Ubelgiji, wakatwangwa 6-1 na England na mechi yao ya mwisho wakashindwa 2-1 na Tunisia. Walifunga mabao mawili pekee.
Walimaliza wa mwisho kwenye Kundi G.
Mchezaji nyota: Luis Tejada. Ana miaka 35 lakini ndiye mfungaji mabao bora wao ambapo amewafungia mabao 42. Ndiye aliyekuwa tegemeo lao kuu kwa mabao Urusi, ingawa katika kujilinda walimtegemea sana nahodha wao Roman Torres.
Wachezaji wa Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja. Ni wachezaji watatu pekee wa kikosi chao huchezea soka Ulaya.
Meneja wao? Raia wa Colombia Hernan Dario Gomez amekuwa mkufunzi kimataifa kwa muda mrefu, ambapo amewaongoza Colombia mara mbili. Hii ilikuwa mara yake ya pili kuongoza timu Kombe la Dunia baada ya kuwafikisha Colombia michuano ya 1998 ambapo walilazwa na England 2-0 kwenye Kundi G.

ASIA
Iran
Ustadi: Ilikuwa ni mara ya tano Iran kufuzu Kombe la Dunia.
Mechi pekee waliyoshinda awali ilikuwa ni 2-1 dhidi ya Marekani michuano ya Ufaransa '98. Lakini Urusi walifanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Morocco siku yao ya kwanza, wakachapwa 1-0 na Uhispania na wakatoka sare ya 1-1 na Uhispania na kumaliza wa tatu kundini na alama 4 mbele ya Morocco.
Mchezaji nyota: Mshambuliaji Sardar Azmoun ambaye kimsingi ndiye mshambuliaji bora zaidi Asia baada ya raia mwenzake Ali Daei, ambaye amefunga mabao mengi kimataifa kuzidi mchezaji mwingine yeyote wa kiume. Azmoun, 22, ni stadi sana kwa miguu na kwa kichwa. Huchezea Rubin Kazan ya Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja
Mkufunzi? Carlos Queiroz amekuwa mkufunzi kwa muda mrefu na ana tawasifu ya kupendeza. Amukuwa mkufunzi Sporting Lisbon, Afrika Kusini, Real Madrid na alikuwa msaidi wa Sir Alex Ferguson Manchester United.
Na amehudumu mara mbili Ureno.
Amekuwa mkufunzi wa Iran kwa miaka sita iliyopita.

Saudi Arabia
Ustadi: Saudi Arabia walishinda mechi zao pekee Kombe la Dunia mara yao ya kwanza 1994, waliposhinda mechi mbili za hatua ya makundi na kufika raundi ya pili.
Ushindi wao mechi ya pili, 1-0 dhidi ya Ubelgiji, ulitokana na moja ya mabao yanayokumbukwa zaidi - Saeed Al Owairan alipokimbia kutoka nusu yao ya uwanja na kuwachenga nusu ya walinzi wa Ubelgiji kisha kufunga.
Mwaka huu walifanikiwa kupata ushindi mwingine walipofanikiwa kuwalaza Misri 2-1, ingawa walichapwa 5-0 na wenyeji Urusi na 1-0 na Uruguay.
Mchezaji nyota: Mshambuliaji mkongwe Nasser Al Shamrani atakuwa na mchango muhimu.
Ni mchezaji bora wa mwaka Asia mwaka 2014.
Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja
Mkufunzi? Bert van Marwijk, ambaye amekuwa kwenye usukani tangu 2015. Mholanzi huyo wa miaka 65, aliwaongoza Uholanzi kufika fainali Kombe la Dunia 2010. Amekuwa pia mkufunzi wa Borussia Dortmund, Feyenoord na Hamburg.

Korea Kusini
Ustadi: Ndiyo timu ya Asia yenye rekodi nzuri michuano ya kimataifa Hufahamika kwa jina la utani Mashujaa wa Taegeuk. Walifuzu kwa michuano yao ya 10 kwa sare dhidi ya Uzbekistan. Urusi ilikuwa mara yao ya tisa mtawalia kushiriki.
Lakini waliondolewa baada ya kuchapwa 1-0 na Sweden na 2-1 na Mexico.
Waliondoka kwa fahari hata hivyo baada ya kuwashinda mabingwa watetezi Ujerumani 2-0.
Mchezaji nyota: Son Heung-min alionyesha ustadi wake Tottenham na aling'aa pia Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Ki Sung-yueng (Swansea), Son Heung-min (Tottenham)
Mkufunzi? Shin Tae-yong ambaye amepewa jina la utani 'Mourinho wa Asia' amekumbwa na shinikizo kutokana na kutofanikiwa sana mechi za kufuzu. Hata hivyo, alichukua usukani Julai na huenda akapewa muda zaidi. Ana miaka 48 na alicheza Ligi Kuu ya Korea Kusini miaka 12 na mechi moja ligi kuu Australia kabla ya kustaafu 2005.

AFRIKA
Misri
Ustadi: Hawakufuzu michuano ya 2010 na 2014 baada ya kushindwa mechi za muondoano za kufuzu baada ya hatua ya makundi.
Walifuzu kwa bao la ushindi kutoka kwa Mohamed Salah wa Liverpool dhidi ya Congo 8 Oktoba lakini nyota wao huo aliumia mwezi Mei.
Ufanisi wao mkubwa karibuni ni mwaka 2010 waliposhinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara yao ya saba.
Misri walitarajiwa kufanya vyema Urusi lakini hilo halikufanyika na walianza kwa kushindwa 1-0 na Uruguay bila Mo Salah na wakachapwa tena 3-1 na Urusi. Hata Mo Salah aliporejea, walishindwa 2-1 na Saudi Arabia mechi yao ya mwisho na kuondoka wakiwa hawana alama yoyote Kundi A.
Mchezaji nyota: Mohamed Salah, aliyenunuliwa na Liverpool majira ya joto, ndiye mchezaji mwenye kipaji zaidi Misri. Ana kasi sana nakufikiwa wakati wa kufuzu alikuwa amefunga mabao 32 mechi 56 za kimataifa, zikiwemo tano mechi za kufuzu kwa Urusi.
Wachezaji Ligi ya Premia: Mohamed Salah (Liverpool), Mohamed Elneny (Arsenal), Ahmed Hegazy (West Brom), Ramadan Sobhi (Stoke),
Wachezaji Championship: Ahmed Elmohamady (Aston Villa)
Wachezaji League One: Sam Morsy (Wigan),
Mkufunzi? Raia wa Argentina Hector Cuper, ambaye amewahi kuwa mkufunzi waValencia na Inter Milan, alichaguliwa kuwa mkufunzi mkuu Machi 2015.
Alikuwa pia mkufunzi wa Georgia kati ya 2008 na 2009.
Michuano yake mikubwa kuongoza timu ilikuwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 ambapo Misri walilazwa 2-1 kwenye fainali na Cameroon.

Nigeria
Ustadi: Hii ilikuwa mara ya sita kwa Nigeria kushiriki fainali za Kombe la Dunia, na mara yao ya tatu mtawalia.
Wallikuwa wamefika hatua ya 16 bora mara tatu - 1994, 1998 na 2014 - lakini hawajawahi kupita hatua hiyo. Mwaka huu walichapwa 2-0 na Croatia ingawa waliwalaza Iceland 2-0 mechi ya pili.
Walimaliza wa tatu baada ya kuchapwa 2-1 na Argentina.
Mchezaji nyota: Nahodha wao John Mikel Obi, ndiye mchezaji wao mwenye uzoefu zaidi kikosini, ambapo amechezea taifa mechi 80 na atakuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Super Eagles Kombe la DUnia Urusi.
Itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea kushiriki michuano hiyo.
Mikel, 30, aliwasaidia kufika hatua ya muondoano 2014 kwa mara ya kwanza tangu 1998.
Kwa sasa yeye huchezea klabu ya Tianjin Teda ya China.
Wachezaji Ligi ya Premia: Alex Iwobi (Arsenal), Victor Moses (Chelsea), Kelechi Iheanacho (Leicester City), Wilfred Ndidi (Leicester City), Ahmed Musa (Leicester City) na Ola Aina (kwa mkopo Hull City kutoka Chelsea).
Mkufunzi? Gernot Rohr ambaye amefanya kazi ya ukufunzi nchi nyingi duniani ndiye mkufunzi wao kwa sasa.
Amewahi kuwa mkufunzi Nice hadi Gabon , Burkina Faso hadi Nigeria.
Mjerumani huyo wa miaka 64 ana tajriba ya hali ya juu.
Rohr alichezea Bayern Munich na Bordeaux.
Kisha alikuwa mkufunzi wa Bordeaux waliposhindwa fainali ya Kombe la Uefa mwaka 1996 na Bayern.
Klabu alizowahi kuwa mkufunzi ni pamoja na Nantes ya Ufaransa, Young Boys Berneya Uswizi, Etoile du Sahel na pia amewahi kuwa mkufunzi Niger.

Comments