Featured Post

HAWA NDIO WANAWAKE MATAJIRI ZAIDI DUNIANI 2017



MFARANSA Liliane Bettencourt, 94 (pichani juu), wa maduka ya bidhaa za urembo L'Oreal, alikuwa ndiye mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na mali ya $39.5bn. Alirithi biashara hiyo.
Lakini alifariki dunia mwezi Machi 2018. Sasa ni nani mwanamke tajiri zaidi duniani?

Nafasi hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya $33.8bn, $1.5bn juu ya mwaka jana. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotanagzwa mapema mwaka huu.
Alice Watson (pichani) ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart, Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani.
Utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.
Yeye ni miongoni mwa wanawake wanne wa familia ya Walton ambao wamo kwenye orodha ya wanawake matajiri zaidi duniani, kwa pamoja utajiri wao ukiwa jumla ya $49.5 bilioni. Wanne hao ni Christy Walton, mjane wa kakake John, na binamu zake Anne Walter Kroenke na Nancy Walton Laurie.
Isabel dos Santos kutoka Angola ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika
Jacqueline Mars, mwenye mali ya $27 bilioni na ambaye babu yake Frank Mars alianzisha kampuni ya pipi ya Mars Inc ndiye mwanamke wa tatu kwa utajiri duniani.
Maria Franca Fissolo anamfuata akiwa na mali ya $25.2 bilioni.
Mumewe marehemu Michele Ferrero alianzisha kampuni ya Ferrero Group. Kampuni ya Ferrero hutengeneza Ferrero Rocher, Kinder Chocolate na Tic Tacs. Kampuni hiyo pia ndiyo hutengeneza Nutella.
Isabel dos Santos kutoka Angola bado ndiye mwanamke tajiri zaidi Afrika, na utajiri wake unakadiriwa kuwa $3.1 bilioni.

Mjane wa Steve Jobs
Mjane wa Steve Jobs, Laurene Powell Jobs, ambaye ana utajiri wa $20 bilioni kutokana na hisa zake katika kampuni za Apple na Disney ni wa tano kwenye orodha hiyo ya wanawake matajiri.
Wengi wa wanawake matajiri duniani walirithi utajiri wao, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini pia wapo wafanyabiashara 15 wa kike ambao hawakurithi mali, sana kutoka Asia.
Mmoja ni Nguyen Thi Phuong Thao kutoka Vietnam anayemiliki kampuni ya safari za ndege ya VietJet.
Marekani, ambayo ina mabilionea wengi wanawake duniani, ina wanawake 74 mabilionea.
Ujerumani na Uchina zinafuata zikiwa na mabilionea 28 na 23 mtawalia.

Wanawake matajiri zaidi duniani 2017
1. Alice Walton - $33.8bn
Utajiri: Wal-Mart
2. Jacqueline Mars - $27bn
Chanzo cha Utajiri: Pipi
3. Maria Franca Fissolo - $25.2bn
Chanzo cha Utajiri: Nutella, chokoleti
4. Susanne Klatten - $20.4bn
Chanzo cha Utajiri: BMW, dawa
Haki miliki ya picha Getty Images
5. Laurene Powell Jobs - $20bn
Chanzo cha Utajiri: Apple, Disney
6. Gina Ronehart - $15bn
Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini
7. Abigail Johnson - $14.4bn
Chanzo cha Utajiri: Usimamizi wa fedha
8. Iris Fontbona - $13.7bn
Chanzo cha Utajiri: Uchimbaji madini
9. Beate Hesiter - $13.6bn
Chanzo cha Utajiri: Maduka ya jumla
10. Charlene de Carvalho-Heineken - $12.6bn
Chanzo cha Utajiri: Heineken
11. Blair Parry-Okeden - $12.2bn
Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari
12. Massimiliana Landini Aleotti - $9.5bn
Chanzo cha Utajiri: Dawa
13. Yang Huiyan - $9bn
Chanzo cha Utajiri: Biashara ya nyumba na ardhi
14. Katharine Rayner - $8.1bn
Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari
15. Margaretta Taylor- $8.1bn
Chanzo cha Utajiri: Vyumba vya habari
16. Zhou Qunfei: - $7.4bn
Chanzo cha Utajiri: Skrini za simu za kisasa
17. Pauline MacmMillan Keinath - $6.8bn
Chanzo cha Utajiri: Cargill
18. Sandra Ortega Mera - $6.7bn
Chanzo cha Utajiri: Zara
19. Carrie Perrodo - $6.3bn
Chanzo cha Utajiri: Mafuta


Comments