Featured Post

BOSI WA SOKA GHANA AJITETEA DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA



ACCRA, GHANA
Mwandishi wa habari za uchunguzi Anas Aremeyaw Anas, kutoka nchini Ghana, amekataa aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, Kwasi Nyantakyi, kwamba mtu fulani alimfuata na kumdai rushwa ya dola za Kimarekani 150,000 kwa lengo la kuzuia uchapishwaji wa taarifa ya ripoti ya ubadhirifu wa fedha na rushwa.

Katika taarifa ya utetezi wake binafsi, bosi huyo wa zamani wa GFA amedai kwamba mwanasheria aliye karibu na Anas alimfuata na kudai kiwango hicho cha fedha ili kufanikisha zoezi la kuzuia uchunguzi wa waraka huo.
Kama hiyo haitoshi, Nyantakyi amedai kuwa, mwandishi huyo wa habari za uchunguzi na timu yake walidukua barua pepe zake.
Lakini ameongeza kudai pia kuwa kiasi cha fedha za Marekani dola 65,000 ambazo alionekana akiziingiza kwenye mfuko katika mkanda uliorekodiwa kwa siri hazikuwa za ushawishi bali dola 40,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu kwa gharama za malazi katika zoezi zima la jitihada za Morocco kutaka kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2026.
Katika taarifa ya kukabiliana na Anas Aremeya Anas amekataa madai hayo akidai kwamba bosi huyo wa zamani amepokea dola 65,000 kama rushwa, na kuongeza kuwa barua pepe za bosi huyo hazikusitishwa kwa muda kumfikia na mtu yeyote wa upande wake.
Wafanyakazi wengi wa tasnia ya soka na viongozi walikamatwa kwa siri kwenye mkanda wa video wakipokea zawadi za fedha inaarifiwa katika waraka wa uchunguzi na kuwaacha wa Ghana walio wengi katika mshangao kutokana na hali hiyo.
Kwesi Nyantakyi, baada ya madai hayo kuibuliwa amejiuzulu nafasi yake ya raisi wa soka la GFA, mjumbe wa FIFA, Umoja wa Soka Afrika Magharibi na hata CAF.
Lakini vita vya maneno baina ya Nyatakyi na Anas vinaendelea na huenda vikasababisha mvutano mkubwa na mrefu sana kisheria.

Comments