Featured Post

WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA UNUNUZI

indexWaziri wa Fedha na Mipango Dkt.  Khalid Salum  Mohamed amefanya uteuzi wa Wajumbe  wanne wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma Zanzibar .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha na kutiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Waziri Khalidi amewateuwa Bw. Mberik Rashid Mberek, Bi. Khadija Ali Mohammed, Bw. Makame Ali Makame na Bi. Mtumwa Said Sandal anaewakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma Zanzibar.
Wajumbe wawili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka wanakuwa wajumbe kwa mujibu wa nyadhifa zao.
Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango amemteua Bw. Said Aboud Mohammed kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
Bw. Said Aboud Mohammed anachukua nafasi ya Bw. Joseph Abdalla Meza ambe hivi karibuni ameteuliwa kuwa Kamishna wa ZRB  na hivyo kuwa mjumbe kwa dhamana yake.
Uteuzi wote huo unaanza tarehe 15 Mei 2018 na unafuatia kuteuliwa Wenyeviti wa Bodi hizo na Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hivi karibuni.

Comments