Featured Post

WAKAZI WA UYUI WAPONGEZA SERIKALI KUJA NA BIMA ITAKAYOWAWEZA KUTIBIWA POPOTE HAPA NCHINI

RC
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Tabora , Uyui  Mkoani Tabora wameipongeza Serikali  ya awamu ya Tano kupitia Mfuko  wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuboresha Bima ya Afya ambayo itawahakikishia kupata huduma ya matibabu mwaka mzima mahali popote hapa popote nchini.

Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani Uyui jana  wakati Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri akiwa katika kampeni ya kuwahamassha wananchi kujiunga na Bima ya Afya walisema hatua hiyo itawaweza kuwa na uhakika wa kupata matibabu yoyote hapa nchini kwa gharama nafuu.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Lutende wilayani Uyui Happiness Damian alisema kuwa kujiunga Bima kunasaidia kuwawezesha wananchi kupata huduma ya matibabu hata kipindi ambacho hawa fedha tasilimu.
Alisema sio wakati wote mtu anaweza kuwa na fedha na hivyo uboreshaji wa huduma hiyo utawezesha wananchi kuishi kwa uhakika wakatti wote.
Naye Mkazi wa Kijiji cha Lutende wilayani humo Omary Hamisi alisema kiwango cha shilingi 76,800 kwa wanaushirika kupata Bima ya mwaka mzima kulinganisha na utoaji wa fedha tasilimu ili kupata matibabu.
Alisema mpango huo ulioletwa na Serikali ni mzuri sana na utawapunguzia gharama za kutumia fedha nyingi kupitia mtindo wa kutoa fedha taslimu.
Hamis alisistiza kuwa mtu ukiwa na uhakika wa matibabu mwkaa mzima utakuwa uhuru hata katika shughuli zako za uzalishaji ya kujiongezea kipato.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema uboreshaji wa huduma ya Bima ya Afya utawawezesha wananchi wote watakajiunga kuwa mazingira ya mazuri ya kuwapatia matibabu mwaka mzima kwa gharama kidogo.
Alisema kwa upande wa mkulima atakayejiunga na Ushirika Afya kupitia Chama chake cha Msingi (AMCOS) atakuwa na faida ya kupata matibabu kuanzia katika Zahanati hadi kwenye Hospitali za Rufaa kwa gharama nafuu ikilnganisha na kulipa fedha tasilimu.
Mwanri aliongeza kuwa mwanachama wa chama cha msingi cha ushirika atatakiwa kulipa shilingi 76,800/-  ataweza kupata matibabu ya aina yoyote  matibabu mwaka mzima popote.
Alisema kuwa fedha wanachangia ni kidogo ukilinganisha na gharama halisi za huduma ambazo atanufaika nazo kwa mwaka na kuongeza kuwa kuna vipimo vingine vinagharimu zaidi ya 300,000/- na dawa na matibabu ya baadhi ya magonjwa inafika hadi milioni 6,000,00O/- lakini mkulima kupitia Ushirika akichangia 76,800 atanufaika mwaka mzima.
Mwanri alisema Bima iliyoboresha imekuja kuondoa mzigo huo kwa mwananchi na kumwekea mazingira ya kujiamini na kumwondolea mashaka mwaka mzima kukosa huduma ya matatibu.
“Ndugu zangu wananchi wangu wa Tabora ambao nawapenda Serikali yetu imefanya kitu kizuri cha kutuletea Bima hiyo ambayo utatibiwa popote sio kama ilivyokuwa zamani…unaweza kwenda Nkinga, Kitete , Bugando hata ukiandikiwa rufaa kwenda Muhimbili utatumia kipande hicho hicho kupata matibabu” alisema.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tabora Vedastus Kalungwani alisema BIMA imeona kuwa mwanaushirika anakuwa na uhakika wa matibabu kipindi cha mavuno na baada ya hapo anapokuwa ameshauza mazao yake na kumaliza fedha anapata wakati mgumu kupata matibabu.
Alisema BIMA ya Afya unavyo vituo 6000 nchi nzima vinavyotoa huduma ya matibabu ambapo kama wanaushirika atajiunga chini ya Mpango wa Ushirika Afya naye atapata huduma.
Kalungwani aliongeza kuwa mkulima uwa na msimu mmoja katika mwaka mmoja na unapokwisha ungojea mwaka mwingine ndio apate fedha jambo ambalo linawafanya wauze mali zao kama vile mashamba ili kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Viongozi wa Bima mkoani humo wako katika kampeni ya kuelimisha wanancha ushirika na wananchi wengine kujiunga na Bima ya Afya ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Comments