- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Na Lilian Lundo - MAELEZO,
Dodoma
Serikali
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 53.8 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni
fedha kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu katika
Halmashauri zote nchini ambazo zitagawiwa kwa njia ya mikopo kupitia vikundi
mbalimbali.
Hayo
yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la
mbunge wa Handeni, Mhe. Omar Abdallah Kigoda juu ya kiasi gani Serikali
inasimamia suala la asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya Vijana na
Kinamama.
"Serikali
imeendelea kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga asilimia 10 ya mapato
yake kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Katika mwaka wa fedha
2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 56.8 zilitengwa na Halmashauri zote nchini,
jumla ya shilingi bilioni 17.5 sawa na asilimia 31 zilitolewa kwa vikundi vya
Wanawake na Vijana” amesema Mhe. Kakunda.
Kakunda
ameendelea kusema kuwa, katika mwaka 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 15.6
sawa na asilimia 27 zilikuwa zimetolewa ambapo jumla ya vikundi 8,672 vya
wanawake na vijana vilipatiwa mikopo.
Aidha
amesema kuwa, ili kuongeza uwajibikaji katika kutenga na kupeleka fedha za
mfuko wa Wanawake na Vijana kwa vikundi husika, Serikali itaweka utaratibu
katika sheria ya fedha (Finance Bill) ya mwaka 2018/2019 utakaohakikisha kwamba
Halmashauri zote zinatekeleza kikamilifu agizo hilo.
Comments
Post a Comment