Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki
wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa
ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel.
Maafisa
wa uhamiaji wameiambia BBC kuwa alihojiwa wiki iliyopita kwenye ubalozi
wa Israel mjini Moscow. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza
nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa
kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi. Mzozo huo ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal. Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati. Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa. Viza
yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki
kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli
yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'. Kucheleweshwa kwa utoaji
wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa
kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu
kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza. Bwn
Abramovich hakuhudhuria fainali za Kombe la FA katika uwanja wa
Wembley mapema mwezi huu wakati Chelsea ilipoichapa Manchester United
1-0. Vyombo vya habari vya Israeli vinasema kuwa tayari amepewa
kitambulisho cha uraia nchini Israeli chini ya sheria ya kurudi
nyumbani, ambayo inawawezesha wayahudi popote pale walipo duniani kurudi
na kuwa raia wa Israel. Gazeti la The Times nchini Israeli limeandika kuwa Bw Abramovich aliwasili Israeli Jumatatu na kwamba amehamia nchini humo. Ni mtu ambaye amekuwa akiitembelea Israeli mara kwa
mara na alinunua hoteli mjini Tel Aviv mnamo mwaka 2015 ambayo
inasemekana ameigeuza kuwa makazi yake. Wamiliki wa pasipoti ya Israeli wanaruhusiwa kuingia Uingereza kwa siku chake bila kuwa na visa. Bw Abramovich ana utajiri wa thamani ya dola bilioni $11.5bn (£8.6bn), kulingana na jarida la Forbes. Kuhamia
kwake Israel kunaweza kumsaidia kifedha kwa sababu kama raia mpya wa
Israeli ataweza kuondolewa ushuru unaolipwa na wawekezaji wa kigeni kwa
muda wa miaka 10.
Roman Abramovich ni nani?
Haki miliki ya pichaReutersImage caption
Mr Abramovich (right) has often been spotted at Chelsea's Stamford Bridge ground
Ni miongoni mwa watu tajiri zaidi Urusi, aliinunua klabu ya Chelsea FC mwaka 2
Inadaiwa aliuza midoli (wanasesere)
kabla ya kuwekeza katika mafuta miaka ya 1990 baada ya kusambaratika kwa
uliokuwa Muungano wa Usovieti
Bw Abramovich alikuwa wakati mmoja
mshirika wa kibiashara wa tajiri wa zamani marehemu Boris Berezovky,
rafiki wa rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin
Wakosoaji wanasema wafanyabiashara hao
wawili walitumia ukaribu wao na ikulu ya Kremlin kujipatia umiliki wa
mashirika mengi ya serikali kwa 'bei ya kutupa'
Bw Abramovich alihudumu kama gavana wa jimbo la Chukotka, Urusi
Anaaminika kuwa na urafiki wa karibu na rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin
Comments
Post a Comment