Featured Post

KOCHA ETIENNE NDAYIRAGIJJE NDIYE MRITHI WA PLUIJM SINGIDA UNITED

etienne-ndayiragije-kocha-wa-mbao-fc

TIMU ya Singida United imemthibitisha Mrundi, Etienne Nayiragijje kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm anayeondoka. 
Pluijm anaondoka Singida United baada ya msimu mmoja na taarifa zinasema Mholanzi huyo anahamia Azam FC ambao wanajipanga upya baada ya msimu huu mbaya kwao chini ya Mromania, Aristica Cioaba ambaye tayari amekwshaondoka.
Msimu huu, Ndayiragijje aliingia kwenye mtafaruku na uongozi wa klabu hiyo ya Mwanza baada ya mzunguko wa kwanza tu wa Ligi Kuu na kuondoka, nafasi yake ikichukuliwa na mchezaji wa zamani wa Pamba SC, Fulgence Novatus.
Pluijm yeye aliichukua Singida United baada ya kupanda Ligi Kuu, kufuatia kufukuzwa Yanga SC na amefanikiwa kuifikisha fainali ya ASFC ambako itamenyana na Mtibwa Sugar Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. 

Comments